9. Khutbah

Khutbah kwaurefu: Ziokoeni Nafsi Zenu…

WAISLAMU nchini wametakiwa kujikita zaidi katika kuwapeleka watoto wao kusoma elimu ya #dini lengo ikiwa ni kutambua #elimu ya ALLAH SWT ambayo itawasaidia katika Maisha ya hapa duniani na kesho akhera.

Nasaha hizo zimetolewa na Imamu msaidizi wa Msikiti al #Haqq Sheikh Ally Mussa wakati akitoa Khutba ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa katika msikiti huo uliyopo mtaa wa karume ndani ya Manispaa ya #Morogoro.

“Allah SWT) ametujaalia familia na hii ni Neema Adhwim Sana, Na Neema hii mtu hawezi akaihisi ila kwa yule iliyomtoka Neema hii, Allah Tabaraka Wataalah Amemjaalia amepata Mke; Hatimaye akawa Nguvu Anazo, Lakini. Kwa Bahati mbaya Hakumjaalia kizazi,Huyu ndiye anakumbuka Thamani ya Neema Hii ya kizazi, lakini kwa sisi ambao tumejaaliwa kupewa vizazi, kiukweli kabisa wengi wetu Thamani hii hatuikumbuki, Na lazima tujue Allah Tabaraka wataalah atakuja kutuuliza siku ya Qiyama, Kama Alivyosema katika Quran “Kisha mtakuja kuulizwa siku hiyo ya Qiyama kwa Neema mbali mbali ambazo mmeneemeshwa”

Katika Neema ambayo ni Adhwim Sana kuliko zote ni Neema ya kizazi, Miongoni mwa Neema zilizo kubwa. Baada ya Allah Tabaraka Wataalah kutuneemesha Neema hii ya kizazi Hakutuacha tu sisi hivi hivi bila Mpangilio, Hivyo akatuwekea utaratibu na akatuhadharisha, Ndipo pale aliposema katika Quran

” Enyi mlioamini ziokoeni Nafsi zenu na Nafsi za Jamaa zenu na Moto” Surat-Tauba 66:06

Katika Maudhi hii Jamaa wa kwanza kabisa wanaozungumziwa ni watoto na wake zako, Napia na wale waliopo katika Milki yako kwa upande wa Malezi, Hakuna wa kuulizwa ila ni wewe.
Kadhia ya Malezi ni Kadhia ambayo Mtume wetu ameiona ni kadhia Muhimu sana, Na ndo maana alikua akiwaombea Dua kabla hata hawajatoka katika migongo au mifuko ya wazazi wao;
Mtume alipokwenda Taif Aliomba Dua hii

“Nataraji mimi katikati yamigongo ya watu hawa kukatika kizazi ambacho kinamuabudu Allah Tabaraka Wataalah na wala hawamshirikishi Allah Tabaraka Wataalah”

Hii yaonyesha Mtume anavyojali familia za Ummah wake na kuwatakia kheiri.

Ally ibnu Abutwalha ibnu Abass alisema¬†” Wafundisheni watoto twaa’ ya kumtii Allah Tabaraka Wataalah,Na wakingeni na kumuasi Allah Tabaraka Wataalah,Na waamrisheni watu wenu kwa kumtaja Allah Tabaraka Wataalah,Kwa hilo litawaokoeni na Adhabu ya Moto”

Mtume SAW alisema¬†“Hakuna mja wa Namna yeyote ile anayetawalishwa na Allah Tabaraka Wataalah, Hatimaye Mauti yakamjia hali ya kuwa amewafanyia khiyana au wale raia wake anaowatawala”

Chaajabu zaidi tumejikita katika kuzihudumia familia katika maswala ya kijamii ila tumeanguka katika Malezi ya kiimani,Na tumeona ni jambo la khiyari na kuwaachia maustadhi na masheikh, Jamii yaporomoka kwa kukosa maadili.

Aidha Shekh Ally Mussa ameongeza kuwa ni vyema kwa kila muislamu kuhakikisha anatumia fursa aliyo nayo katika malezi ya #watoto wake kuwasomesha dini ya ALLAH SWT.
Katika hatua nyingine imamu huyo hakusita kutoa wito kwa jamii ya kiislam kuwa makini katika malezi ya watoto wao kufuata Elimu zote mbili ya hapa Duniani na kesho akhera kwa kupanga muda vizuri katika kuwasomesha vijana wao. Pia amewaomba wazazi kuutumia huu muda wa watoto wao waliomaliza darasa la saba kuwapa maarifa ya Dini ya kiislam kwani hakuna kizazi salama bila maarifa ya kumtambua Allah Tabaraka Wataalah.
Pia wazazi wamehusiwa kufanya Uadilifu juu ya maswala ya kuwapatia Elimu watoto wao na kutokupuuzia Elimu ya maarifa ya kiislam.
Allah Tabaraka Wataalah Anasema” Huwanyanyua watu kupitia kitabu chake kitukufu na wengine waporomoshwa daraja kwa kukidharau kitabu hiki” yaani kwa kutambua maarifa ya Dini ya kiislam watu hupata kufanikiwa juu ya mahitajio yao.

Kila mmoja ataulizwa kwa alichokichunga na hatoacha mtu kutupiwa lawama na kizazi chake kwa kutowapatia maarifa ya Dini ya kiislam,Tumeifanya Dini kua jambo la ziada sana na tumejisahau,Elimu ya Dini tunainyima haki yake na tusitaraji watoto wetu watakua watoto wema na kizazi chake kitakua hivyohivyo na siku zote wataridhishana na kutokua na Khofu ya Allah Tabaraka Wataalah.

Watu wengi sasa hawajui kuisoma vyema Quran na hata watoto wao pia,na pia tuwacheni kuwadharau walimu maana mwalimu ndiye mwenye Elimu ana anayepaswa kuheshimiwa sababu ndiye anayeweza kuibadili jamii yetu ya Kiislam, Watu waona wivu kwa kuwaona watoto wa wenzao ni wasomaji wazuri Wa Quran na amehifadhi hadithi vizuri, na ndipo mtu ajisikia vibaya na wivu ila amesahau kua na yeye atakiwa kuwafinza wanawe DINI”

ALLAH SWT ANASEMA “ALLAH HABADILISHI YALIYOPO KWA WATU MPAKA WATU WENYEWE WABADILISHE YALE YALIOPO KATIKA NAFSI ZAO”

TUTENDEE HAKI KATIKA KUWAPATIA WATOTO WETU ELIMU YA DINI YETU TUKUFU YA KIISLAM.

WABILLAH TAQFIQ

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close