9. Khutbah

Khutbah: Utukufu wa Masjid Aqswa

WAISLAMU nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya waislamu nchini palestina kwani nchini hiyo ni moja kati ya nchi yenye historia kubwa ya dini tukufu ya kiislamu.
Kauli hiyo imetolewa na imamu mkuu msikiti wa Haqq sheikh Ibrahim Twaha wakati akitoa Khutba ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa katika msikiti huo uliyopo ndani ya manispaa ya Morogoro.
Aidha Sheikh Ibrahim Twaha ameongeza kuwa ni vyema waislamu kuhakikisha wanapinga yale wanayo fanyiwa waislamu wa nchi hiyo kwani kwa kufanya hivyo itakuwa ni moja kati ya njia za kutetea maslahi ya dini hiyo.

Katika hatua nyingine Sheikh Ibrahim hakusita kuwataka waislamu kuendelea kudumisha amani ya nchi yetu ya Tanzania ili kuwezesha viongozi wa serikali kuendelea kufanya kazi kwa moyo na kwa uadilifu mkubwa ili viongozi wa dini waendelee kufanya kazi ya kulingania kwa uhuru.

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close