9. Khutbah

Abubakar Swidiq Khalifah wa kwanza wa Uislam

Tumekutana leo Tena katika sikuu hii Tukufu, Bwana wa Masiku Yaumul jumaa Tukiwa katika Mwendelezo wa Khutbah Yetu Toka ijumaa iliyopita ikienda kwa jina la Abubakar Swidiq Radhi za Allah zimuendee, Waislamu Tukiangalia Matendo ya Abubakar Swidiq (Allah amridhie).
Mtume wetu Muhammad Salaam na Amani ziwe juu lake, Alikaa na maswahaba katika masiku na akawaambia

“Kabla ya kuja mimi kuna amabao hawakutaka kuabudia masanamu na walikua wanaongea maneno mazuri mno ila siyakumbuki, Abubakar akajibu, ewe Mtume wa Allah mimi nayakumbuka tulikua tukisema kua Haiwezekani kweli tunaabudia masanamu? Na ilhali hapa kuna Nyumba Tukufu ambayo ilijengwa na Mtume wa Allah aliyepita, Basi Tufanyeni subrah Allah ataleta tu Mtume, Ambaye ni wewe Muhammad Mtume wa Allah”

Wakati wa makurayshi walipotaka kumuuwa Mtume wa Allah, basi Mtume wa Allah alimfuata Abubakar na kumwaambia

“Hali ya Makkah ishakua ngumu na hawa watu wanataka kuniua, Je, upo Tayari kuungana na mimi, Abubakar akajibu Naam siwezi kuiacha Fursa Adhim nitaungana na wewe”

Ndipo pale Wakamfuata Alli bin Abitwaalib na kumuambia yeye alale katika kitanda cha Muhammad Mtume wa Allah, wajue kua Mtume wa Allah amelala, Basi Alli Alikubali, Na Abubakar wakaondoka pamoja na Mtume wa Allah, Ndipo Asmah bint Abubakar Alipochukua Jukumu la kupeleka chakula kwa Baba yake pamoja na Mtume wa Allah wakiwa wamejificha katika pango, Ndipo Allah katika Quran Anasema

“USIHUZUNIKE! HAKIKA ALLAH YUPO PAMOJA NASI”

Baada ya Abubakar akiwa katika pango na Mtume wa Allah na akiwa Analia kwa kumuhofia Mtume atauwawa na Makurayshi, Analia pia wanahama kwa Huzuni, Machungu, Mawazo mengi katika vichwa vyao mpaka

“Abubakar anajisemea katika ulimi wake (Hisia) Mbona Mtume wa Allah Anateseka ikiwa mimi ni mjuzi wa makurayshi, nina heshimiwa na kusikilizwa na ndiye niliekua nikiwasaidia watu”

Abubakar Swidiq (Allah Amridie), wewe nani ambaye unayeweza kumtukana Abubakar, ALLAH anamtambua, Mtume anamtambua, Tunaishi nao na Tunawasikia hawa wakimtusi Abubakar, na sisi pia Tumewapa watoto wetu wawaoe hawa ambao sio waislamu, Basi jitazame kama Umemuozesha Mwanao kwa mtu kama huyu fanya liwezekanalo kumnyang’anya Binti yako mtu huyo.

Katika Hadith Ya Hishamambayo anaielezea Zeyd bin Aslam,Anasema Zayd bin Aslam

“Baba yangu alisema Hakika Nilimsikia Mtume wa Allah, Nilimsikia Omar anasema, Alituamrisha Mtume wa Allah siku Moja Tutoe sadaka, Nataka nione sadaka, Omar Bin khatab anasema Alimuambia nitatoa ewe Mtume wa Allah,na Leo katika Kutoa huku nafsi mwangu nikijisemea leo nitahakikisha Nashindana na Abubakar, Nilikuja mimk kifua mbele na Nusu ya Mali yangu niliyokua nayo, Mtume wa Allah akamuuliza Omar umebakizia nini watoto wako, Akasema Omar nimewaachia mfano wa mali niliokuja nayo, Mara Abubakar akaleta kila alichokua nacho, Mtume wa Allah akamuuliza Abubakar umewaachia nini watoto wako? Abubakar akamjibu nimewaachia ALLAH na wewe Mtume wa Allah, Omar alisema Naapia kwa ALLAH kwaanzia leo sitofanya mashindano na wewe”

Ulamaa wanasema kuna ishara nyingi zilizopelekea Abubakar kua Raisi wa waislamu, Ushahidi moja wapo ni Pale Mtume wa Allah alipopanda katika Jabal la Uhud na mpaka jabal likatikisika kwa woga, ndipo Mtume wa Allah aliposema “Tulia ewe Uhud Juu yako yupo Mtume wa Allah na Abubakar..” hapa yaonyesha Tosha alikua akianza kwa Abubakar Swidiq (Allah amridhie) kisha ndo anataja maswahaba wengine kwa mtiririko wa Makhalifa, kingine ulamaa wanasema ninkule kitendo cha Mtume wa Allah alivyokua akikaribia kufa ishara mbalimbali alitoa na akasikitika kwa Ndugu zake watakaokuja Baada yake yeye kufariki alipokua ameenda kuzuru Makabur ya Uhud na Baada ya Hali kua mbaya Muda wa swala ulipofika wa swala aliwaambia kua Cheo changu changu cha kutatua mambo na Kuswalisha Apewe Abubakar Swidiq, Maswahaba wanalia wanamuambia Mtume wa Allah njoo utuswalishe, Mtume wa Allah anawajibu Muamurudi Abubakar Swidiq aswalishe, Abubakar Swidiq akawaswalisha.

Waislamu Mtume wa Allah Amemuamrisha Abubakar Swidiq awaongoze watu Na baadae Mtume wa Allah alifariki, Omar amepata kiwewe anasema

“Yeyote atakayesema Mtume wa Allah amekufa Shingo yake Halali Yangu”

Abubakar Swidiq Anaenda kumfunua Mtume wa Allah anakuta Mtume wa Allah ameshafariki kisha anamfunika huku akilia na akiwa anamuombea Dua, anatoka na anawaambia watu “Omar acha kuwatisha watu ila nawaambia Nyie watu mmesahau kua Mtume wa Allah aliwaambia kua yeye ni Binadamu tu na akuoneni hukuma na akawapa mafunzo vipi Mtaenda kinyume”

Mtume akazikwa!
Maanswar wakatoka na kuelekea kwa Banuu saida , Muhajirin wakapata Taarifa kua Maansar wapo Mahala fulani na lengo lao sio Baya ila ni kupata Kiongozi wa Kuongoza Ummah, wao maanswar walimuona Miongoni mwao kuna Mtu wa kuwaongoza, Basi Muhajirin nao wakaongoza mpaka kwa Banuu saida, Omar bun khatab Hakuoendezewa na Hali ile akataka asimame ila Abubakar Swidiq akamtuliza Omar Bin khatab, Abubakar Swidiq alijua wao Maanswar wanamtaka Nani! Abu’ubayda Amirl Jaraha , Abubakar Swidiq akasimama akawaambia Answar na Muhajirin Mnatambua kua Mtume wa Allah alikupendeni Mno nyinyi, Kama mnataka hivyo Ataongoza tu, Abubakar Swidiq akamsimamisha Omar Bin khatab na Abu’umayda Mchagueni Mmoja wao awe kiongozi wenu!
Omar Bin khatab na Abu’umayda wote wanalia, Omar Bin khatab Akasema Hapana Swala hili tuwaachie Hawa waislam wajue nani wa kumchagua kati ya sisi watatu Na watu wote wakampigia Kura Abubakar Swidiq , Leo wanatokea watu wasiojielewa na kusema kua Abubakar Swidiq amehodhi Madaraka na Amefanya Dhulma toka enzi za Mtume wa Allah, Hawa wenye maimamu kumi na mbili wenye kuwatukana Maswahaba, mpaka wanamsingizia Malaika jibril amefanya Dhulma kumpatia Mtume wa Allah Utume, eti Utume ulitakiwa uende kwa Ali Bin Abitwaalib, Na tunaishi nao hawa hapahapa Tanzania.

Abubakar Swidiq baada ya kuteuliwa kua Rais Alihutubia watu baada ya Kumtukuza ALLAH na kumswalia Mtume wa Allah, akasema “Enyi watu leo nimechaguliwa kua kiongizi wa waislamu, ila Mimi sio Mbora kuliko Nyinyi,Nikifanya Uzuri basi nitiini, na nikikosea Niwekeni sawa, Ukweli ni Amana, Na uongo ni Khiyana, Napenda mfahamu, Nyinyi nyie mnaemuona ni dhaifu kwangu ndiye mwenye nguvu, Na mwenye nguvu kwenu kwangu ni dhaifu na kama alidhulumu nitarehesha kila akichokidhulumu”
Taarifa zinakuja kua watu wameritadi baada ya kusikia Mtume wa Allah amefariki na wengine kuzuia kutoa zakah, ndipo Abubakar Swidiq akasema “Kuanzia sasa hivi napenda mfahamu yeyeote asiyetaka kujitolea kuukomboa huu uislamu,kuhakikisha wote walioritadi wanarejea katika dini ya Allah na ambaye hatofanya atawaletea Udhalili juu yake” na akasema “Madhambi kukithiri katika Mji ni moja ya sababu Mabalaa kukithiri katika Mji, nakuambieni ya kua Niheshimuni na mnitii pale ambapo nimechukua kutoka kwa Allah na Mtume wa Allah, na Nikienda kinyume msinitii na simameni kwaajili ya Swala Ili Mpate kurehemiwa na Allah”

Abubakar Swidiq (Radhi za Allah ziwe juu lake)

Tags
Show More

Related Articles

Check Also

Close
Back to top button
Close