1. Fahamu Usiyoyajua

Ukamilifu wa Aqidah ya Kiislamu

Ndani ya mwezi wa Ramadhan, Waislamu ulimwenguni kote wanafunga wakati wa mchana na kufanya ziada ya ibada nyakati za usiku ili kuwa karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. Hili ni kinyume na jamii nyingi wanazoishi Waislamu, ambazo zimedhibitiwa na ‘materialism’ (kupenda mali) na ubinafsi, ikiwa ni nyenzo yao kuu ya kutafuta utulivu katika maisha.

Inakuwaje Waislamu wanajizuia kula na kunywa mpaka saa 22 kwa siku (kutegemea na nchi gani wanaishi)? Hawa wanaitikia amri ya Mola wao. Allah Aliyetukuka anasema: “Enyi mlioamini! Mmeamrishwa Swaumu, kama waliyoamrishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.” [Qur’an, 2:183].

Aya nyingine zinazofanana na hiyo zinaangazia utukufu wa kufunga na vitendo vingine vya ibada kama kusali mara tano kwa siku, kutoa zaka na kutoa sadaka. Waislamu wanatekeleza vitendo hivi bila ya kusita kwa ajili ya kumuabudu Muumba wa wanadamu, Muumba wa maisha na dunia.

Sharia, kama msingi wa maadili ya Kiislamu.

Anapofanya jambo lolote katika jamii, msingi wa maadili (halali na haramu) kwa Waislamu unazingatia kigezo kile – Sharia ya Kiislamu na siyo utashi wa mtu wala matamanio ya nafsi.

Uislamu unafundisha Waislamu kwamba, vitendo vinavyopaswa kufanyika hadharani na faraghani vyote vinaongozwa na ‘Taqwa’ na matokeo yake ni tabia njema, haki, usawa na kuheshimu watu wengine bila ya kubagua rangi, kabila, dini au hadhi.

Mafundisho haya ni kinyume na yake ya jamii zisizo za Kiislamu, ambazo vigezo vyao vya kufanya mambo vina misingi ya kisekula isiyomtambua Mwenyezi Mungu. Katika vigezo vyao hivyo vya kikafiri, ni uti wa mgongo wa mafanikio na kuwa na mwenza wa kumpenda maishani ndiyo kilele cha furaha.

Maadili ya jamii za kisekula

Jamii za kisekula zimezalisha kujipendelea, ulafi, uchoyo, ubinafsi na kutafuta furaha kwa udi na uvumba katika maisha haya mafupi ya hapa duniani, hata kwa kuangamiza wengine! Hali hii inasababisha majanga katika ngazi ya jamii, kama vile mgawanyo mbovu wa mali, na kuzalisha pengo kubwa baina ya matajiri na masikini huonekana wazi.

Majanga mengine yanayozalishwa katika jamii za kisekyula ni pamoja na ubaguzi wa rangi na kukosekana usawa wa kijinsia, ambapo wanawake bado wanafanya kampeni za kupigania haki sawa, na bado wanatumika kama vifaa vya kuburudisha wanaume kwenye madanguro na matangazo ya biashara.

Jamii za kisekula zimesababisha majeraha makubwa ambayo binadamu amewahi kuyashuhudia ikiwemo kuvunjika kwa familia ambayo ndiyo kiini cha msingi cha jamii yoyote, uhalifu kama mauaji, wizi, udanganyifu, ghushi, utapeli, ubakaji, utumiaji wa madawa ya kulevya na kadhalika. Magereza yamefurika kiasi kwamba wahalifu wengi wanapewa adhabu za kulipa faini na kufanyakazi za kijamii kuliko kupelekwa gerezani.

Kama vile hiyo haitoshi, pia hakuna namna ya kushughulikia matatizo ya upotevu wa ajira, migogoro ya kifamilia au wagonjwa wasio na jamaa au waliotelekezwa. Ndiyo maana matatizo ya afya ya akili, ikiwemo sonono (depression) ni jambo la kawaida sana katika jamii za Magharibi!.

Ni sehemu ya maumbile ya mwanadamu kuabudu na kumtukuza Muumba na kutafuta muongozo wa jinsi ya kuishi vizuri kwa kadri inavyowezekana hapa duniani. Kwa Waislamu, hili linafanyika kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja, Anayestahiki pekee, Aliyetukuka, Aliyemkamilifu. Uislamu unawafundisha wanadamu jinsi ya kushughulika na matatizo katika maisha kama vile vifo vya wapendwa wao, umasikini na maradhi. Kwa kufanya hivyo, Waislamu wanafundishwa subira na hatimaye kujiandaa na Akhera kwa kuwa haya maisha ni mtihani kutoka kwa Muumba. Utaratibu huo ndiyo uti wa mgongo wa maisha ya Muislamu hapa duniani.

Haja ya kuabudu kitu kikubwa zaidi kuliko yule anayeabudu imekuwepo tangu kuumbwa kwa wanadamu na ndiyo maana baadhi ya watu wanaabudu nyota, wanyama, binadamu wenzao, masanamu na vitu vingine. Katika zama za sasa, inaweza kuonekana jinsi wanamichezo, waigizaji, wanamuziki na wengineo wanavyoheshimiwa na watu hata kufikia kiwango kinachokaribia kuwaabudu kwa kufuata vitendo vyao, muonekano wao na mitindo yao ya maisha. Hata kwa wanasayansi, wasioamini uwepo wa Mwenyezi Mungu, na wale wasioamini visivyoonekana, wanatamani kuwa kama mtu fulani, ambapo hiyo ni sehemu ya silka ya maumbile ya binadamu ya kuabudu kitu kikubwa zaidi kuliko yeye.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close