1. Fahamu Usiyoyajua

Sheikh Ally Jumanne achambua anga za juu

Wakati wanadamu tukichukulia dunia kama kitu kikubwa, ukweli ni kwamba sayari yetu hii tunayoishi ndani yake ni tone tu la maji katika bahari ya Mwenyezi Mungu ya uumbaji wake.

Hayo yalijulikana kupitia mada iliyowasilishwa na Sheikh Ally Jumanne katika kongamano la Misk ya Roho 2018 lililofanyika katika ukumbi Diamond Jubilee jumapili iliyopita, ambapo Sheikh huyo wa Morogoro alichambua sayari za juu na nafasi ya dunia katika mpangilio wake.

Katika mada iliyosisimua hadhira, Sheikh Jumanne alionesha wazi kuwa hii dunia inaingia, kiukubwa, mara mpaka bilioni kwa baadhi ya nyota katika anga za juu, jambo ambalo linaifanya sayari hii kama punje tu iliyodondoka jangwani! Kama dunia ni punje, jiulize binadamu mmoja ni nani katika viumbe vya Allah Aliyetukuka.

Ukiacha uchambuzi wake juu ya sayari za juu, Sheikh Jumanne pia aliitaka jamii ya Kiislamu hapa nchini kuishi kwa kufuata mafundisho ya Qur’ an na Sunna za Mtume [rehema za Allah na amani zimshukie] muda wote wa maisha yao ya hapa duniani.

Sheikh Jumanne alisema jamii ya Kiislamu haina budi kujiepusha na ibada ya kuwatumikia viumbe kwa kuwa hilo ni jambo ovu, lenye kuangamiza. Sheikh Ally aliyekuwa akiwasilisha mada ‘Kanuni za Mwenyezi Mungu katika uumbaji wake’ alisema:

Watu wamekataa utumwa wa Allah na kinyume chake wamekuwa watumwa wa dunia, na mbaya zaidi Wanapokuwa katika harakati za kusaka maisha huwa hawaombi dua wakiamini kuwa mafanikio huja baada ya kufanya jitihada au kutumia akili na vipaji vya kuzaliwa.”

Na kwa sababu tunajifanya hatumtambui Allah, Allah ameamua kutushughulisha zaidi na kutafuta maisha ili hatimaye vile tunavyovihitaji visipatikane burebure bali kwa kuvihangaikia. Huu ni ushahidi kuwa mtu anaweza kukwepa ibada lakini huwezi kukwepa matokeo ya kuikimbia ibada,” alisema Sheikh Jumanne.

Ni kwa sababu hii, Sheikh Ally alitumia fursa ya kongamano hilo kuwataka waislamu kujisalimisha kwa Mola wao kwa kutekeleza ibada yake bila ya kumshirikisha na chochote, pia kukiri kuwa Allah ndiye Muumba wa kila kitu.

Kila siku tunaamka mapema asubuhi na kuelekea maeneo yao ya kazi kwa sababu tu tunaamini kazi ndio maisha yetu. Tumekuwa tunawanyenyekea mno mabosi wetu, kiasi cha kuukaribia utumwa, lakini katika ibada kama vile swala hatufanyi hivyo,” alimalizia kusema Sheikh Ally

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close