4. Darasa La Wiki

Wanafunzi Wakiislamu watakiwa kushiriki semina za Kiislamu

Wanafunzi wa Kiislamu hususani wale wa shule za serikali wametakiwa kuwa na tabia ya kuhudhuria semina zinazoandaliwa na jumuiya mbalimbali za Kiislamu ili waweze kupatiwa elimu ya jinsi ya kuishi shuleni na kufanya vizuri katika mitihani yao.

Akizungumza katika semina maalum ya kuwafunda wanafunzi hao, mlezi wa wanafunzi wa Kiislam shuleni, Mzee Mikidadi Khalfani, amesema mara nyingi semina hizo huandaliwa ili kuwajenga vijana hao kisaikolojia pamoja mambo muhimu kwao.

Mzee Khalfani ambae alikuwa anaongea na wanafunzi wa kidato cha pili na tano hivi karibuni katika msikiti wa Lilah uliopo Buza Changuru jijini Dar es Salaam, pia aliwatolea wito wazazi wakiislamu kuwahimza vijana wao kuhudhuria semina hizo.

Pia Mzee Mikidadi aliwahimiza wazazi wa Kiislamu wawapatie vijana wao elimu ya dini ili kujenga kizazi kilicho bora kwa kuwa elimu ya dini ndio muongozo bora hapa duniani na akhera.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa elimu katika Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu nchini (TAMSYA) Mkoa wa Dar es salaam, Mustafa Zuberi, amewataka wanafunzi hao waache kupoteza muda katika kufanya mambo yasiyofaa badala yake wajikite katika kufanya mambo ya msingi.

Nao baadhi ya Wanafunzi walioshiriki katika semina hiyo akiwemo Amirat wa shule ya Sekondari Keko, Rahma Msuya, ameeleza kunufaika na semina hiyo hususani katika suala la kuzingatia maadili na nidhamu kama moja ya misingi ya kufanya vizuri katika matokeo shuleni.

Kwa upande wake Athumani Salum toka shule ya sekondari Buza ameeleza kuwa semina hizo ni muhimu na kuomba ziendelee kutolewa kwa wingi ili vijana wapate elimu.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close