4. Darasa La Wiki

Umuhimu wa adabu za kijamii katika kuleta ustawi na maendeleo ya umma

Ubora wa maisha ya Waislamu unategemea kiwango chao cha tabia njema. Tabia njema ni muhimu mno katika Uislamu na ndiyo maana Mtume (rehema za Allah na amani zimshukue) alifupisha malengo ya utume kwa kusema: “Hakika nimetumwa kwa ajili ya kutimiza tabia njema.”

Tabia njema ndiyo kipimo cha kusanifisha mafanikio ya jamii, ambapo jamii bora yajulikana kwa watu wake kufuata maadili ya kibinadamu na tabia njema zikiwemo ushujaa, ukarimu, ukweli, huruma, rehema, uaminifu, uadilifu n.k.

Qur’an Tukufu inahimiza sifa na tabia njema kwa kusimulia visa kadha wa kadha kueleza ubora na utukufu wa tabia hizo. Kuhusu ushujaa wa Nabii Musa (amani imshukie) katika kutetea haki, Mwenyezi Mungu anasema:

“Na alipoyafikia maji ya Madyana alikuta umati wa watu wananywesha (wanyama wao), na akakuta karibu yao wanawake wawili wanawazuia wanyama wao. Akasema, ‘Mna nini?’ Wakasema, ‘Hatunyweshi sisi mpaka wamalize hao wachunga. Na baba yetu ni mzee sana.’”

Kisa kinaendelea: “Basi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema, ‘Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayoniteremshia’ Basi mmoja katika wale wanawake wawili akamjia, naye anaona haya. Akasema, ‘Baba yangu anakuita akulipe ujira wa kutunyweshea.’ Basi alipo mjia na akamsimulia visa vyake, alisema: Usiogope; umekwishaokoka kwenye watu madhaalimu. Akasema mmoja katika wale wanawake: Ewe baba yetu! Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumuajiri ni mwenye nguvu na muaminifu.” [Qur’an, 28: 23-26].

Pia, tunasoma kisa cha Nabii Yusuf (Allah amridhie) na tabia alizokuwa nazo na namna alivyoweza kujiokoa kutoka katika mtihani mgumu wa mke wa bwana wake aliyetaka kumlaghai. Hata hivyo, kwa sababu ya tabia na sifa yake nzuri, Mwenyezi Mungu alimwokoa.

Qur’an Tukufu inaeleza: “Na yule bibi wa nyumba aliyokuwamo Yusuf alimtamani kinyume cha nafsi yake, na akafunga milango. Akamwambia, ‘Njoo!’ Yusuf akasema, ‘Audhubillahi! Najikinga kwa Mwenyezi Mungu. Huyu bwana wangu kaniweka maskani nzuri, na hakika wenye kudhulumu hawatengenekewi.’” [Qur’an, 12:23].

Na kwa sababu ya tabia njema na maadili yake, Yusuf alipandishwa cheo akawa Msaidizi Maalum wa Mfalme baada ya kutoka kifungoni: “Basi mfalme akasema, ‘Mleteni kwangu, awe wangu mwenyewe khasa.’ Basi alipomsemeza alinena: ‘Hakika wewe leo umekwisha tamakani kwetu na umeaminika’. Yusuf akasema, ‘Nifanye mshika hazina za nchi. Kwani hakika mimi ni mlinzi mjuzi. Basi namna hivi tukampa Yusuf cheo katika nchi; anakaa humo popote anapopenda. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, wala hatupuuzi malipo ya wafanyao mema. Na hakika malipo ya Akhera ni bora zaidi, kwa walioamini na wakawa wachamungu.” [Quran, 12:54-57].

Mtume Muhammad na tabia njema

Mtume Muhammad (rehema za Allah na amani zimshukie) alikamilika na kusifika kwa sifa zote njema na alikuw aukamilifu wa kitabia. Mtume pia alikuwa mfano bora katika hali zake zote bora kitabia na kichamungu hadi makafiri wakamwita ‘As-Sadiq Al-Amiin’ (Mkweli na Mwaminifu).

Mwenyezi Mungu alimsifu Mtume wake (rehema za Allah na amani zimshukie) kwa kusema: “Na hakika wewe una tabia tukufu.” [Qur’an, 68:4]. Naye Bi Asha alipoulizwa kuhusu tabia ya Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) alisema: “Kwa hakika tabia yake zilikuwa ndizo Qur’an.” Hii maana yake ni kuwa alikuwa na tabia zinazotokana na mafunzo ya Qur’an Tukufu.

Hatuwezi kuzieleza kirefu tabia za ki-Qur’an katika makala moja, lakini ni tabia njema zikiwemo upole, uaminifu, ukweli, uadilifu, ukarimu, rehema na huruma. Hivyo, Mtume wetu ni mfano bora zaidi wa wenye tabia njema katika hali zote.

Mtume hakuwa na bughudha, chuki wala jeuri bali pia alipenda kuwafundisha tabia zake njema Maswahaba na wanadamu wote wakiwemo maadui. Isitoshe, alikuwa anawausia wawe wapole siyo tu kwa watu bali hata kwa wanyama.

Tabia njema ni kipimo cha kusanifisha jamii na kufanikiwa kwake, ambapo jamii bora ni ile ambayo watu wake wanafuata maadili ya kibinadamu na tabia zote njema kama vile; ushujaa, ukarimu, ukweli, huruma, rehema, uaminifu, uadilifu n.k.

Tabia njema na Ustawi wa dini

Je, tunatambuaje kuwa dini yetu adhimu inahimiza mno na kutegemea tabia na maadili mema katika ustawi wake? Qur’an Tukufu inatoa wito wa kutakasisha tabia na kuchunga maadili kwani ni sababu ya kutukuka kwa umma wowote. Mwenyezi Mungu amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu,na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, nauovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka” [Qur’an, 16:90].

Na tukifuatilia aya za Qur’an Tukufu, tutaelewa kuwa tabia njema ndiyo msingi muhimu wa umma wetu huu na hakika hakuna dalili iliyo wazi zaidi kuliko pale Allah Aliyetukuka alipomsifu Mtume: “Na hakika wewe una tabia tukufu” [Qur’an, 68:4]. Dalili nyingine ni pale Mtume alipobainisha lengo kuu la Utume wake: “Hakika nimetumwa kwa ajili ya kutimiza tabia njema.”

Kwa upande mwingine, Qur’an Tukufu imetuhadithia kuhusu hatima na matokeo ya tabia mbaya na ukosefu wa maadili na sifa nzuri. Jambo hili limekuwa sababu ya kuporomoka na kusambaratika kwa jamii nyingi katika historia ya ulimwengu.

Mwenyezi Mungu amesema: “Na pindi tukitaka kuuteketeza mji, huwaamrisha wale wenye starehe na taanusi, lakini wao huendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli huthibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa” [Qur’an, 17:16].

Qur’an na Sunna zimejaa visa vya umma zilizoangamizwa kwa sababu ya tabia zake mbaya. Mifano ni mingi ikiwemo kaumu/ watu za Manabii Hud, Swaleh, Lut, Shuaib na wengine ambao walichafuka kitabia wakastahiki kuadhibiwa duniani na huku wakisubiri adhabu ya Akhera ambayo ni kali zaidi.

Aya nyingi katika Qur’an zimesimulia visa vya umma hizo. Kuhusu kaumu ya A’d ambayo Hud aliletwa kwao, Mwenyezi Mungu anasema:

“Ama kina A’di walijivuna katika nchi bila ya haki, na wakasema, ‘Nani aliyekuwa na nguvu kushinda sisi? Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu aliyewaumba ni Mwenye nguvu kushinda wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu! Basi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku za ukorofi ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwa hizi katika uhai wa duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina hizaya zaidi, na wala wao hawatanusuriwa.” [Qur’an, 41:15-16].

Na kuhusu kaumu wa Nabii Swaleh, Mwenyezi Mungu amesema: “Na walikuwamo mjini watu tisa wakifanya ufisadi katika nchi wala hawafanyi la maslaha.” [Qur’an, 27:48].

Ama kaumu Lut, Mwenyezi Mungu amesema: “Na pale Lut alipowaambia watu wake, ‘Hakika nyinyi mnafanya uchafu, ambao hapana mmoja katika walimwengu aliyekutangulieni kwa hayo. Je! Nyinyi mnawaingilia wanaume, na mnaikataa njia? Na katika mikutano yenu mnafanya maovu? Basi haikuwa jawabu ya watu wake isipo kuwa kusema, ‘Tuletee hiyo

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close