4. Darasa La Wiki

Tutumie Ramadhani kujifunza kusameheana

Kutubia makosa na kukithirisha ‘istigh- faar’ yaani kumuomba msamaha Allah, ni ngao mbili muhimu zinazoweza kum- kinga muumini kutokana na dosari za kibin- adamu. Mwezi wa Ramadhani ni fursa muhimu ya kutekeleza amali hizi kikamilifu. Pamoja na umuhimu huo, baadhi yetu tu- mekosa utayari wa kutekeleza ibada hii kuto- kana na kuipa thamani ndogo, na ndiyo maana kila mwaka tunafunga lakini hatuoni matunda ya funga. Kadhalika, miongoni mwetu tumekuwa wepesi wa kutenda maovu lakini wazito wa kutubia tukitumai kuwa, Allah ni mwingi wa kusamehe hivyo hakuna shaka atatusamehe. Hii ni itikadi potofu na yenye kuangamiza ambayo Muislamu hapaswi kuwa nayo. Jambo muhimu kwa mfungaji ni ku- muomba msamaha Allah kadiri awezavyo. Mja anaposhikama na jambo hili Mwenyezi Mungu humbadilishia madhambi yake na kuwa thawabu. Allah anasema: “Isipokuwa atayetubu na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusamehe, mwenye kurehemu,” (Qur’an, 25:70). Pamoja na faida hii, wapo baadhi yetu am- bao katu hawaoni umuhimu wa kujishu- ghulisha na kuomba msamaha. Huu ni utovu wa nidhamu na ni katika alama ya mtu kuwa na kiburi na majivuno. Kushindwa ku- muomba Allah msamaha ndiyo sababu ya wengi wetu kuugua maradhi ya nafsi hivyo kuathiri mahusiano ya kibinadamu hasa linapokuja suala la kuombana msamaha.

Ni muhimu tuwe na utaratibu wa ku-wasamehe pamoja na kuwafanyia wema wa- naotudhulumu na kutukosea. Allah anatuambia ndani ya Qur’an: “Na wasamehe, na waachilie mbali. Je nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa msama- ha (na) mwingi wa rehema. (Basi nyinyi sifik- eni kwa sifa hizi),” (Qur’an, 24:22). Ni kwa sababu hii, mfungaji wa swaumu ya Ramadhani anatakiwa awe mwingi wa kusamehe na mkarimu kwa watu. Zaidi, tunapaswa kutambua kuwa, wan- adamu ni viumbe waliokadiriwa na Allah Ta’ala upungufu mwingi wa kimaumbile likiwemo suala la kukoseana. Hivyo, kitendo cha mtu kukataa kusamehe baada ya kuom- bwa msamaha hakikubaliki kisharia. Pia, kukataa kusamehe kunapingana na asili ya maumbile ya mwanadamu ambayo ni kukosea. Kwa sababu ya asili hiyo, tunalaz-imika kusameheana kwa sababu hatukuitwa wanadamu ila ni wenye kukosea. Kwa maana nyingine, kuvunja kanuni ya kusamehe, ni sawa na kuvunja kanuni ya maisha, na ndiyo maana nasisitiza juu ya kila mmoja kuliwajibikia suala la kusamehe. Kushindwa kulitekeleza hili, ni kujivisha kiburi ambacho kwa hakika si katika sifa za Waumini. Imesimuliwa katika kahadithul Qudsiy kutoka kwa Abu Huraira ya kwamba, Mwenyezi Mungu anasema: “Kiburi ni (mfano wa) vazi langu la chini, na utukufu ni (mfano wa) vazi langu la juu atakaye ( jaribu) kuninyang’anya moja kati ya hizo, nitamtupa motoni na wala sijali,” (Muslim).

Kutokusamehe ni kikwazo

Bila shaka wengi tunapenda kustawisha imani zetu lakini jitihada hizo zinashindwa kuzaa matunda kwa sababu ya kutokusame-he. Kadhalika,wengitunashidambalimbali ambazo kwazo tunamuomba Allah lakini hatupati majibu. Hii ni kwa sababu kutokusamehe ni kik- wazo na kizuizi kikubwa kinachosimama baina ya mtu na majibu ya maombi yake kwa Allah Ta’ala. Utakubaliana nami kuwa, samahani ni neno dogo ambalo lau jamii ya wanadamu wangezingatia umuhimu wake lingeweza kusaidia kuokoa kutoka kuangamia maelfu yawatu. Nenosamahanilinaimarishaundu- gu pamoja na kuepusha chuki baina ya wa- najamii. Ukweli ni kwamba, wengi hatutaki kuwaomba msamaha wale tunaowakosea kwa sababu ya kuhisi kudharaulika na kuonekana duni mbele yao jambo linalopele- kea mifarakano na chuki kati ya mkosa na ali- yekosewa. Hapa,inafaakujiulizanikwanini Waislamu wanafikia hatua ya kuchukiana na kuhasimiana kwa kigezo cha tofauti za kimi- tazamo ya kifiqhi. Siyo hao tu, wapo pia waliochupa mipaka ambao kufarakana kwao, kunatokana na ushabiki wa timu za mpira pamoja na vyama vya siasa. Hali hii imekuwa ikisababisha maafa makubwa kiasi cha baadhi yetu kushindwa kusemezana, kusaidiana na hata kuzikana. Ni dhahiri makosa tunayomfanyia Mwenyezi Mungu ni makubwa zaidi ukilin- ganisha na yale tunayotendeana baina yetu. Pamoja na ukubwa huo wa madhambi yetu, bado Allah huyasamehe huku akiendeleza mapenzi yake kwetu kama anavyosema: “Naye (Allah) ni mwenye kusamehe, mwenye mapenzi,” (Qur’an, 85:14). Ikiwa ukweli ni huo basi tujiulize, ni kwa nini tunashindwa kusamehe makosa mado- go madogo na wakati huo tunatamani kusamehewa na Mwenyezi Mungu mad- hambi yetu makubwa makubwa? Mwezi wa Ramadhani ni fursa ya wau- mini kujifunza kusameheana, kukirimiana na kuishi kwa salama, mapenzi na amani baina yao. Hivyo, tumuombe Mwenyezi Mungu atu- wezeshe katika hayo, atukubalie amali zetu na atulipe badala.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close