4. Darasa La Wiki

Tukithirishe adhkar Ramadhan hii

Allah Mtukufu anatuambia: “Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (swaumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili muwe wachamungu.” [Qur’an, 2:183].

Maneno haya matukufu yana mafunzo makubwa matatu ambayo ni; mosi, kufunga ni amri na wala si hiyari, pili swaumu ya Ramadhan ina faida nyingi kiroho, kijamii, kiafya na kimaadili na tatu, funga inapelekea mtu kuwa mchamungu, lengo ambalo Allah amelibainisha ndani ya Qur’an Tukufu pale aliposema:

“Sikuwaumba majini na wanadamu ila wapate kuniabudu.” [Qur’an, 51:56].

Kwa hiyo, tunatakiwa kumuabudu/ kumcha Allah saa 24 kila siku na katika kila kipengele cha maisha yetu mwaka mzima. Na hii ndiyo maana halisi ya kufuata ‘Swiratwal Mustaqima’, yaani njia iliyonyooka ambayo katika kila rakaa ya sala tunamuomba Allah atuoneshe.

Ombi hili limo katika Suratul Fatiha (Qur’an, 1:6–7) ambapo kila mwenye kusali huomba:

“Tuongoze katika njia iliyonyooka. Njia ya wale uliowaneemesha, si ya wale walioghadhibikiwa wala waliopotea.”

Tunajifunza kutokana na aya hizi mbili kuwa kufuata njia iliyonyooka ni kutekeleza amri za Allah na kuacha makatazo yake katika maisha yetu ya kila siku.

Kwa hiyo kufuata njia iliyonyooka siyo tu kusema Al–hamdulillah baada ya kushiba au kufanikiwa kupata neema fulani bali pia kuhakikisha kile kilichokushibisha kimepatikana na kuliwa kwa mujibu wa muongozo wa Kitabu (Qur’an) na Sunna za Mtume Muhammad.

Mfano huu unadhihirisha jinsi ibada zinavyowachunga Waislamu wasitoke nje ya utaratibu wa maisha wa Kiislamu. Na hii ndiyo tafsiri sahihi ya kufuata njia ilinyooka. Hivyo, maana ya kufuata njia iliyonyooka siyo kuachana n a mambo ya dunia bali kufanya mambo yote ya dini na dunia kwa kuzingatia maelekezo ya Allah na Mtume wake.

Na miongoni mwa ibada tunazopaswa kuziendea kwa pupa na kwa shauku ya hali ya juu katika msimu huu wa Ramadhan ni kumtaja (kumdhukuru) Allah. Kumdhukuru Allah ni muhimu kwa sababu kunamfanya mtu abaki kwenye utaratibu wa maisha wa Kiislamu hata baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhan.

Dhikri humuepusha muumini na kutenda jambo lililoharamishwa na Allah, na pia humsukuma mtu kutubia haraka pale anapokosea na kufuatiza mambo mema badala yake.

Si hivyo tu, dhikri humjengea muumini msingi imara wa uadilifu kwani mtu amkumbukae Allah muda wote huweza kuepuka uovu hata akiwa peke yake chumbani, gizani, uchochoroni, kichakani, pangoni, msituni na kwingineko. Kwa ujumla tunaweza kusema, dhikri ni silaha madhubuti ya kupambana na matamanio ya nafsi yanayotiwa nguvu na vishawishi vya Iblis (shetani aliyelaaniwa).

Kwa hiyo kama tunataka kupambana na vishawishi vya shetani, hatuna budi kudumu katika kumdhukuru Allah. Maana yake ni kwamba, mtu hawezi kuwa mtulivu wa nafsi isipokuwa aishi kwa mujibu wa utaratibu wa dini. Allah anasema ndani ya Qur’an:

“Hakika kwa kumdhukuru Allah ndio nyoyo hutulia.” [Qur’an, 13:28].

Lakini kwa masikitiko makubwa, wengi wetu tumekosa wasaa wa kumtaja Allah nyumbani, matembezini, na pia kwenye maeneo ya kazi. Ni ukweli usiyo na shaka kuwa, vinywa vya baadhi yetu vina muda mrefu havijamdhukuru Allah Ta’ala, na badala yake vimetawaliwa na utajo wa mashetani kupitia hadithi za wanamichezo, nyimbo na muziki.

Hii ni dalili kwamba, umma umeghafilika na ibada ya kumtaja Allah ambayo kupitia kwayo ndiyo nyoyo hupata utulivu. Ni hasara iliyoje kwa Muislamu kupitwa na siku moja ya Ramadhan pasina kumtaja Mola wake walau kwa uchache.

Dhikri kama msingi wa ibada

Na kwa vile ibada ndio lengo na kusudio la kuwepo kwetu duniani, ni lazima tufanye hima ya kuleta adhkar mara kwa mara wakati na baada ya Ramadhan ikiwa tunahitaji kuridhiwa na Allah.

Na miongoni mwa faida za kumdhukuru Allah ni kwamba, mja akiteleza na kufanya dhambi huwa mwepesi wa kutenda amali njema, kuepuka yaliyoharamishwa na kuharakisha kufanya toba. Kimaumbile, kumdhukuru Allah siyo jambo nyepesi kwa sababu ndani ya nafsi zetu kuna shetani ambaye daima hutushawishi tumfuate yeye, na pia kuna mashetani wengine wengi wa nje ambao hutumia mbinu mbalimbali zenye hila kutushawishi kutenda dhambi.

Ndiyo maana Allah ametufaradhishia funga ya Ramadhan ili tudumu katika utumaduni wa kumcha Yeye na kumkumbuka muda wote. Changamoto kubwa iliyopo ni Waislamu wengi kudhani kwamba dhikri ni ibada inayofanywa zaidi wakati wa sala msikitini au katika msimu wa Ramadhan, jambo linalowafanya baadhi yao kuacha kumtaja Allah katika nyakati zisizokuwa hizo.

Tumtaje Allah kwa majina yake mazuri

Katika mwezi huu Mtukufu ni vizuri pia tukamtaja Allah kwa Majina yake Mazuri, pamoja na Sifa Zake Tukufu. Qur’ an inasema:

“Na Allah ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa kutumia majina hayo.” [Qur’an, 7:180].

Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) alimtaka Bi. Aisha (Allah amridhie) alazimiane na dua/ dhikri inayojumuisha maneno ya jumla. Bi Aisha akamuuliza Mtume, ni yapi hayo maneno ya jumla? Mtume akasema:

“Ewe Mola wangu wa haki, hakika mimi nakuomba kheri zote za sasa hivi na za wakati ujao, ninazozijua na nisizozijua. Na ninajilinda kwako na shari zote, za sasa hivi na za baadae, ninazozijua na nisizozijua…”

Mambo ya kutahadhari tunapofanya adhkar

Mwenye kufanya adhkaar atahadhari na mambo yatakayomuharibia dhikri yake, au yatakayomfanya aende kinyume na matakwa ya sharia. Hapa kuna jambo muhimu, inabidi tuliweke wazi. Ni kwamba yeyote anayemtaja Allah na huku anatamka ndani ya dhikri hiyo majina ya mawalii, waja wema na waliokufa mashahidi, kwa lengo la kujilinda au kutaka wokovu, bila ya shaka atakuwa amekufuru.

Huyu anaitakidi yule anayemtaja, kuwa ana uwezo wa kuruzuku, kuneemesha na kudhuru. Mtume aliwalaani washirikina wa Kiarabu waliokuwa wakiitakidi kwamba miungu yao wanayoiabudu na kuitukuza ina uwezo wa kuumba na kuruzuku, au kuratibu jambo la yule anayeomba.

Makafiri wale walikuwa wanajua fika kwamba mwenye uwezo wa kufanya yote hayo ni Allah Mtukufu peke yake, kama Allah alivyosimulia kupitia ndimi zao: “Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongea tu kumkar

“Hakika kwa kumdhukuru Allah ndio nyoyo hutulia.” [Qur’an, 13:28].

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close