4. Darasa La Wiki

Tuendeleze somo la kusamehe, kuvumilia tulilolipata ndani ya Ramadhani

Kwa hakika ngao pekee inayoweza kum- kinga muumini kutokana na dosari za kibinadamu ni kutubia makosa pamo- ja na kukithirisha ‘Istighfaar’ yaani ku- muomba msamaha Mwenyezi Mungu. Mwezi wa Ramadhani ni fursa muhimu ya kutekeleza amali hizi kikamilifu.

Pamoja na umuhimu huo, bado mion- goni mwetu hatuna utayari wa kuitekeleza ibada hii kutokana na kuipa thamani ndo- go, na ndio maana kila mwaka tunafunga lakini hatuoni matunda ya funga.

Kadhalika, baadhi yetu tumekuwa wa- tenda maovu huku tukiwa wazito wa kutu- bia kwa matumaini kuwa, Allah ni mwingi wa kusamehe hivyo hakuna shaka atatuse- mehe. Hii ni itikadi potofu na yenye kuan- gamiza ambayo Muislamu hapaswi kuwa nayo. Jambo muhimu kwa muumini ni kui- wajibikia ibada ya Allah Ta’ala sanjari na kuomba msamaha kadiri awezavyo.Mja anaposhikamana na jambo hili Mwenyezi Mungu humbadilishia madhambi yake na kuwa thawabu.

Hii ni kwa kauli yake Allah Ta’ala pale anaposema: “Isipokuwa atakayetubu na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha mao- vu yao yawe mema.Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusamehe, mwenye kurehemu,” (Qur’an, 25:70).

Pamoja na faida hii, bado kuna baadhi ya Waislamu ambao katu hawaoni umuhimu wa kuomba msamaha. Huu ni utovu wa nidhamu na ni katika alama ya mtu kuwa na kiburi na majivuno.

Si hivyo tu, bali kitendo hiki cha kuto- jishughulisha na kumtaka Allah msamaha ndio chanzo cha wanadamu wengi kuugua maradhi ya nafsi hivyo kuathiri mahusiano ya kibinadamu hususan linapokuja suala la kuombana msahama.

Kwa mfano, wapo wanaodiriki kusema: “Katu siwezi kukusamehe, na hata ni- kikusamehe siwezi kukusahau,” Vilevile wapo wanaofikia muafaka kwa kuwaambia waliowakosea: “Tufanye yameisha,” hali ya kuwa bado wana vifundo kwenye nyoyo zao.

Katika hili, tunapaswa kutambua kuwa, wanadamu ni viumbe waliokadiriwa na Al-

lah Ta’ala upungufu mwingi wa kimaumbile likiwemo suala la kukoseana, hivyo kitendo cha mtu kukataa kusamehe baada ya kuom- bwa msamaha hakikubaliki katika dini.

Pia kufanya hivyo kunapingana na asili ya maumbile ya mwanadamu ambayo ni kukosea, na kwa msingi huo, tunalazimika kusameheana kwa sababu hatukuitwa wa- nadamu ila kwa kuwa na sifa ya kukosea.

Kwa maana nyingine kuvunja kanuni ya msamaha ni sawa na kuvunja kanuni ya maisha, na ndio maana nasema, tunawa- jibika kujifunza kusamehe.Kushindwa ku- litekeleza hili ni kujivisha kiburi ambacho kwa hakika si katika sifa za muumini.

Imesimuliwa Hadithul Qudsiy kutoka kwa Abu Huraira (Allah amridhie) ya kwamba, Mwenyezi Mungu anasema:“Kiburi ni (mfano wa) vazi langu la chini, na utukufu ni (mfano wa) vazi langu la juu atakaye ( jaribu) kuninya’nganya moja kati ya hizo, nitamtupa motoni na wala sija- li,” (Muslim).

kutokusamehe ni kikwazo

Bila shaka wengi tunapenda kustawisha

imani zetu lakini jitihada hizo zinashindwa kuzaa matunda kwa sababu ya kuto- kusamehe. Wengi pia tuna shida mbalim- bali ambazo kwazo tunamuomba Allah la- kini hatupati majibu. Hii ni kwa sababu kutokusamehe ni kikwazo na kizuizi kikubwa kinachosimama baina ya mtu na majibu ya maombi yake kwa Allah Ta’ala.

Utakubaliana nami kwamba, samahani ni neno dogo ambalo lau jamii ya wanada- mu wangezingatia umuhimu wake lingewe- za kusaidia kuokoa maelfu ya watu kuanga- mia, kuimarisha undugu na umoja pamoja na kuepusha chuki na visasi baina ya wana- jamii.

Ukweli ni kwamba wengi hatutaki ku- waomba msamaha wale tunaowakosea kwa sababu ya kuhisi kudharaulika au kuoneka- na duni mbele yao jambo linalopelekea mi- farakano na chuki kati ya mkosa na aliyeko- sewa.

Hapa inafaa kujiuliza ni kwa nini Wais- lamu wanafikia hatua ya kuchukiana na ku- hasimiana eti kwa sababu tu ya tofauti zao za kimitazamo ya kifiqhi.

Siyo hao tu lakini pia wapo waliochupa

mipaka ambao kufarakana kwao, kuna- tokana na ushabiki wa timu za mpira pamo- ja na vyama vya siasa. Hali hii imekuwa iki- sababisha maafa makubwa kiasi cha baadhi yetu kushindwa kusemezana, kusaidiana na hata kuzikana.

Ni dhahiri makosa tunayomfanyia Allah Ta’ala ni makubwa zaidi ukilinganisha na yale tunayotendeana baina yetu. Pamoja na ukubwa huo, bado Allah huyasamehe huku akiendeleza mapenzi yake kwetu kama ana- vyosema: “Nae (Allah) ni mwenye kusame- he, mwenye mapenzi,” (Qur’an, 85:14).

Ikiwa ukweli ni huo basi tujiulize swali hili: Ni kwa nini tunashindwa kusamehe makosa madogo madogo na wakati huo tu- natamani kusamehewa na Mwenyezi Mun- gu madhambi yetu makubwa makubwa?

Katika hali ya kutusahihisha, Allah ali- yetukuka anatuzindua akisema: “Na wasamehe, na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita). Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mun- gu ni Mwingi wa msamaha (na) mwingi wa rehema. (Basi nyinyi sifikeni kwa sifa hizi),” (Qur’an, 24:22).

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close