4. Darasa La Wiki

Taratibu na misingi inayoimarisha ndoa katika uislamu

SEHEMU YA 4 Katika makala iliyopita tulizungumzia kuhusu suala la kuposa mwanamke aliyekuwa katika eda. Katika makala hii tutaangazia hukumu ya mke aliyeolewa kupitia posa ya haramu. Tumeshabainisha katika makala zilizopita kwamba ni haramu kwa mujibu wa makubaliano ya pamoja ya wanawazuoni kutumia lugha ya dhahiri kumposa mwanamke aliye katika eda, sawasawa eda yenyewe ilikuwa ni ya ku wa na mume, kutengana kudogo au kukubwa, eda ya talaka rejea eda ya uvunjaji wa ndoa.

Aidha tulibainisha kwamba inafaa kuposa kwa kutumia lugha ya ishara, kwa mwanamke aliye katika eda kwa kuzingatia hali fulani, na uharamu unakuwepo kwa nyakati fulani.

Swali la msingi la kujiuliza katika shauri hili, ni ipi hukumu ya mwan- amke aliyeolewa kwa kupitia mchaka- to wa posa ya haramu? Jibu la swali hili ni kwamba, kwa kauli sahihi ya wa- nazuoni, ndoa inakuwa sahihi, lakini mhusika hupata madhambi kwa saba- bu jambo la haramu alilolitenda ha- likuleta dosari katika kiini cha mkata- ba wa ndoa.

Hukumu ya kuposa mahali alipoposa mwenzako

Hakika Uislamu umehifadhi haki ya Muislamu, na hii ni adabu ya juu kabisa. Na miongoni mwa adabu hiyo ni Muislamu kuacha kuposa mahali

alipoposa ndugu yake hadi ataka- poshindwa kwa sababu kitendo hicho kinaleta chuki katika nafsi ya mtu, na pia huzalisha chuki kwa mwengine.

Imekuja Hadithi kutoka kwa Abuu Huraira (Allah amridhie), kwamba Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: ”Haitakikani mtu kuposa mahali ambapo ndugu yake amekwishaposa ima akamilishe ndoa hiyo au ashindwe,” (Bukhari)

Na imepokewa Hadithi kutoka kwa Ukba bin Amir, kwamba Mtume ame- kwishaposa amesema: “Muumini ni ndugu wa muumini mwingine, hai- takikani kwa muumini kuingilia manunuzi ya ndugu yake, wala asipose mahali alipokwisha kuposa ndugu yake hadi atakapoamua kuachana na jambo hilo” (Muslim)

Na Hadithi zote mbili hizi zinafa- hamisha ya kwamba ni haramu mtu kuposa mahali ambapo ndugu yake

ameshatanguliza posa. Wanazuoni wa sharia ya Kiislamu wamebainisha sharti zinazofanya posa ya pili iwe ni ya haramu. Miongoni mwa sharti hizo ni uhalali wa posa ya kwanza. Lau kama posa ya kwanza ilikuwa ni haramu, mfano mwanamke alichumbiwa wakati yupo katika eda, basi hakika posa ya pili inasihi kisharia, lakini baa- da ya kumalizika eda.

Aidha, inatakiwa posa ya kwanza iwe imeshakubaliwa, na kukubaliwa huko kuwe kunafahamika na upande wa posa ya pili. Na iwapo posa ya kwanza haikukubaliwa au hakuna jibu lolote lile. Katika hali hiyo, kauli iliyo sahihi kwa baadhi ya wanazuoni ni kwamba inaruhusiwa kupeleka posa nyingne.

Ushahidi katika hili ni kauli ya Fat- ma binti Kaisi (Allah amridhie): ”Alini- posa Muawiya na Abuu Jahmi, Mtume hakuchukizwa na uposaji wawawili hao, bali na yeye alimposea Us-

ama ibn Zaid,” (Bukhari)
Vilevile, katika uharamu wa kuposa

sehemu aliyoposa mwezako, mposaji wa kwanza asiwe amemruhusu mposaji mwengine kupeleka posa ya pili, au asiwe ameachana na kadhia hiyo. Kama mposaji wa kwanza atari- dhia kupelekwa posa ya pili, au aliach- ana kabisa na suala la uchumba huo, katika hali hiyo uharamu utakuwa umeondoka.

Lakini wanazuoni wamebainisha ya kuwa ruhusa ya mposaji wa kwanza isiwe imesababishwa na hofu na woga au aibu. Iwapo mposaji wa kwanza ameitoa ruhusa hiyo kutokakana na mawili hayo, uharamu utabaki pale pale.

Aidha wanazuoni wamebainisha kuwa ruhusa itakayotolewa na mposa- ji wa kwanza, inajumuisha mposaji wa pili na mwingne.

Nani anayezingatiwa katika kuridisha jibu la posa?

Tumeshabainisha ya kuwa jibu la kukubaliwa posa linapotolewa ni har- amu kwa mtu mwengine kupeleka posa mahali hapo. Swali la msingi la kujiuliza hapa, ni je, ni nani hasa mwenye mamlaka ya kukubali posa hiyo au kuikataa, ni muolewa mwenyewe au mzazi wake?

Jibu la swali hili, linatofautiana ku- fuatana na hali ya mwanamake anaye- taka kuolewa. Iwapo ni mwanamke mtu mzima, ‘Thayyibu’ mwenye utambuzi, jibu la kuikubali posa au kuikataa litatoka kwake yeye mwenyewe. Hii ni kwa sababu yeye ndiye anayeitambua vizuri nafsi yake kuliko mtu mwengine.

Iwapo mzazi wake anamlazimisha kuolewa na mtu asiyemridhia mwenyewe, sharia inazingatia kauli yake na wala haizingatii kauli ya mzazi wake. Na iwapo ndoa itafungwa na huku akiwa hakuridhia ndoa hiyo si sahihi kwa mujibu wa sharia ya Kiisla- mu.

Mwanamke kumchumbia mwanaume

Katika sharia ya Kiislamu, mwan- amke anayo haki ya kumposa mwa- naume. Mwanamke kumposa mwa- naume ambaye anafahamika ubora wake katika maadili ya dini, ni jambo linakubalika na sharia na wala hakuna kipingamizi katika jambo hilo. Hata wanazuoni wamesema hili ni jambo la kisunna.

Ushahidi wa jambo hili ni Hadithi ya mwanamke aliyekuja kwa Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) akamuomba Mtume amuoe. Licha ya kwamba Mtume hakumuoa, pia hakuchukizwa na ombi la mwanamke huyo. Lau Mtume angechukizwa na kauli hiyo angemkataza, kwa kuwa Mtume siku zote hayanyamazii mam- bo yasiyofaa katika dini. Aidha, mzazi wa kiume anayo haki ya kumshauri biniti yake kuposwa na mwanamume anayemuona kuwa ana maadili mazuri. Umar ibn Khattwab (Allah amridhie) al- imchumbia binti yake Hafsa kwa Uthmani ibn Affan. Uthmani aliposhundwa kutoa jibu, alimweleza Abu- bakar (Allah awari- dhie wote).

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close