4. Darasa La Wiki

Muovu zaidi, anaweza kuwa mwema!

Kuna habari unapokutana nazo unajikuta tu unatabasamu, huku ukibubujikwa na machozi ya furaha na mshangao. Miongoni mwa habari hizo, ni asiyekuwa Muislamu anapotamka Shahada na kuukubali Uislamu. Lakini hali, inavutia zaidi unapofahamu kuwa mtu huyo aliyesilimu alikuwa mpinzani mkubwa wa dini ya Mwenyezi Mungu, aliyekuwa akikebehi, akikashifu na akiponda mafundisho yake.

Alhamdulillah, mwanasiasa wa Uholanzi Joram Van Klaveren, alitangaza hadharani kusilimu kwake miezi michache iliyopita, baada ya kubadili dini mwishoni mwa mwaka


Imam Ghazali (Allah amrehemu) alipata kusema: “Kuwa mlinganiaji, na usiwe Jaji.” Imam Ghazal akayachambua zaidi maneno hayo kwa kusema: “Kujiona wewe ni bora zaidi kuliko mtu yeyote ni kibri cha wazi kabisa.” Allah ‘Azza wa Jalla’ anasema: “Wala usitembee katika ardhi kwa majivuno.” (Qur’an, 17:37).

Kinachovutia katika kusilimu kwake, kama ilivyo kuwa kwa wengi kabla yake, ni kuwa, njia ya mwanasiasa huyu kuelekea kwenye nuru ya Uislamu, haikuwa rahisi. Van Klaveren alikuwa ni mbunge kutoka chama cha mrengo wa kulia, Freedom Party, na pia alikuwa mkosoaji mkubwa wa Uislamu, mpaka pale alipojiondoa kwenye chama hicho na kuacha rasmi siasa mwaka 2014.

Kama alivyoiweka mwandishi wa Imaan, Van Klaveren alitumia muda mwingi kufanya utafiti wa Uislamu ili kuandika kitabu cha ‘kuubomoa.’ Hatimaye bwana mkubwa huyu aliishia kujiondoa katika njia ya mchepuko ya chuki na ukafiri; na kurejea katika njia kuu, aliyoiridhia Allah, Muumba wetu Aliyetukuka. Hebu sasa tuangalie baadhi ya mafunzo ambayo tunaweza kuyachota kutokana na kisa hiki cha kusisimua.

Yule anayeongoza
Kumshawishi asiye Muislamu kuukubali Uislamu ni kazi ngumu sana. Kumshawishi asiye Muislamu ambaye ameshatamka mara nyingi tu hadharani kwamba, “Uislamu ni uongo”, “Muhammad ni mchawi” na “Qur’an ni sumu” ni kazi ngumu zaidi kwa mtu yeyote yule.

Lakini Allah ‘Azza wa Jalla’ ni ‘Al-Ha’di’ (Yule anayeongoza), na mwenyewe anasema wazi ndani ya Qur’an, akielezea muongozo wake: “Kwa hakika wewe humuongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humuongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao.” (Qur’an, 28:56). Muongozo wa Van Klaveren ulikuja wakati alipokuwa akiandika kitabu cha kuubomoa Uislamu. Amesema: “Wakati wa andiko lile, nilikutana na vitu vingi zaidi na zaidi, ambavyo vilifanya mtazamo wangu mkali kuhusu Uislamu kuanza kupungua nguvu.”

Ndugu zangu katika imani, hakuna mtu anayejua ‘hidaya’ itatokea wapi na katika sura gani. Inaweza kuwa, kupitia maneno yanayoingizwa kwenye moyo wa mtu au yaweza kuwa kwa kuona ‘akhlaq’ (tabia njema), ambayo kamwe haitaondoka kichwani mwake.

Van Klaveren, bila ya kudhamiria, amejifunza ukweli wa dini ya Mwenyezi Mungu kupitia kuandika kitabu cha kuibomoa dini hiyo! Ajabu ya ‘Rahman’ hiyo ndiyo njia iliyosababisha moyo wake kukaa sawa na kuona ukweli! Hiyo ndiyo sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema za Allah na amani zimshukie) amesema: “Nyoyo ziko kati kati ya vidole vya Allah. Anazigeuza upande wowote anaotaka.” (Sunan al-Tirmidhiy). Usidharau jema lolote hata likiwa dogo kiasi gani, kwani hujui wakati gani maisha ya mtu yanaweza kubadilika.

Usimdharau mtu yeyote
Hakuna Muislamu yeyote, vyovyote awavyo, mwenye haki ya kuwahukumu au kuwadharau watu wengine. Ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye atakayehukumu Siku ya Kiyama. Kama Waislamu, tuna wajibu wa kuwajali na kuwathamini binadamu wengine.

Imam Ghazali (Allah amrehemu) alipata kusema: “Kuwa mlinganiaji, na usiwe Jaji.” Imam Ghazal akayachambua zaidi maneno hayo kwa kusema: “Kujiona wewe ni bora zaidi kuliko mtu yeyote ni kibri cha wazi kabisa.” Allah ‘Azza wa Jalla’ anasema: “Wala usitembee katika ardhi kwa majivuno.” (Qur’an, 17:37).

Mtu huyo unayemdharau, yule muovu wa dhahiri kabisa, anaweza akawa ni rafiki Mwenyezi Mungu au muda mfupi ujao anaweza akapata daraja hiyo. Na wewe kwa upande mwingine, unaweza hata usife Muislamu.

Kwa hiyo, ndugu zangu wapendwa katika Imani, chukueni kama kanuni kwamba, Uislamu haujawahi kuhamasisha kudharau wale wanaoonekana kuwa watu wabaya, wakiwemo wasio Waislamu, licha ya njama zao za nyuma ya pazia, kuvuruga ujumbe wake.

Bila ya shaka, Joram Van Klaveren aliogolea matusi mengi kutoka kwa Waislamu, hatua ambayo ilidhalilisha Kitabu chetu, Dini yetu na Mtume wetu (rehema za Allah na amani zimshukie). Lakini sasa tunashangilia amerejea kwetu, na hiyo inatupeleka kwenye funzo la mwisho ninalotaka tuakisi pamoja…

Muovu zaidi anaweza kuwa mwema
Kwa kawaida, watu wanaofanya juhudi kubwa za kuupiga vita Uislamu, baada ya kusilimu kwao, wanakuwa watu madhubuti sana katika kuupigania Uislamu. Tukirejea historia ya Mtume wetu (rehema za Allah na amani zimshukie), ambaye ndiye aliyekuwa jemedari wa kupigania Uislamu wakati wake, kazi yake ilirahisishwa zaidi na watu waliomzunguka.

Mmoja wa watu hao, ni yule ambaye hatasahaulika, Umar bin Al-Khattab (Allah amridhie), aliyekuwa ni mtu mashuhuri, aliyeheshimika sana miongoni mwa Makuraish. Kwa hiyo, Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie), aliomba dua hii: “Ewe Mwenyezi Mungu! Upe Uislamu nguvu kupitia mmoja wa watu unaowapenda zaidi, Abu Jahl au Umar bin Al-Khattab.” (Sunan al-Tirmidhiy).

Kwa hiyo, tunampongeza ndugu yetu Van Klaveren, huku tukimuomba ‘Allah Azza wa Jalla’ amuwezeshe kufuata nyayo za Umar bin Al-Khattab, na atumie nafasi yake kuwa nguzo ya taa kwa ajili ya kuuangazia umma wa Kiislamu. Na inaonekana Van Klaveren ana nia ya kuutetea Uislamu, kwani alipoulizwa: “Waislamu wengi wamechoshwa na kujieleza kila wakati…”. Alijibu: “Mimi bado mpya, kwa hiyo nataka kufanya vizuri miaka inayokuja. Kwa mapenzi yote.” Mwenyezi Mungu audumishe moyo wake kwenye Uislamu na awaongoze wengine wengi zaidi kwenye njia ya haki. Amin.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close