4. Darasa La Wiki

Kuelewa udhaifu wetu kutufanye madhubuti katika kuitafuta Akhera

Moja yafunzomuhimuambalokirusi cha Corona kimeufundisha ulimwenguni kwamba, mmoja wa wakazi wake wadogo mno ameweza kuvuruga maisha kwa kiasi kikubwa kama tunavyoyajua.

Kirusi hiki chenye wastani wakipenyo cha takriban ‘nanometre’ 120 hakikubagua kati ya mataifa masikini na yale yaliyoendelea, au matajiri, walioelimika, warembonakadhalika.

Kilichofanya ni kutulazimisha kupiga hatua moja kubwa nyuma kutoka kwenye maisha tuliyokuwa tukiyaendesha na kutufanya tutathmini upya malengo yetu tuliyoyapanga, ya muda mfupi na mrefu. Ghafla, maisha tunayoishi yamekuwatetemno.

Namna gani mtu anashughulikia tatizo katika maishai na tegemea na imani na maadili yake ambayo hushawishi mawazo na vitendo vyake. Kama Waislamu tumebarikiwa muongozo wa MwenyeziMungu, Mola wa vitu vyote vinavyotuzunguka, kikiwemo kirusi cha corona.

Kwa hiyo, wakati sisi Waislamu tukitafakari udhaifu wa maisha na vipi tunahitaji kuunganisha dhana hii kwa usahihi wakati tunapofinyanga maisha yetu, tutageukia Qur’an na Sunna ilikupata muongozo sahihi wakutusaidia kufanya maamuzi sahihi. Kwa mfano, Allah ‘AzzawaJalla’ anajua kwamba malengo yetu mengi ya maisha yanahusiana na tamaa yakujilimbikizia mali. Kwahiyo anatuonya kuhusu hilindani ya Qur’an:

“Mali na watoto ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayobakia ni bora mbele ya Mola wako kwa malipo, na bora kwa matumaini.” [Qur’an, 18:46].

Mwenyezi Mungu anasema tena: “Siku ambayo mali haya tofaa kitu wala watoto. Isipokuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi.” [Qur’an, 26-88:89].

Aya hizo za Qur’an zinatukumbusha na kufinyanga mawazo yetu na vitendo kiasi kwamba tusipuuze masuala muhimu zaidi. Kwa mfano, tusipuuze kujipinda katika kutenda mema kwa kuendekeza matamanio yetu ya duniani, kama vile kukusanyamali.

Kadri tunavyokumbushwa kwamba uhalisia wetu wasasa nidhaifu;  na ndivyo tutakavyo elekea kuwekeza kwenye mambo yasiyona kikomo (yaani Akhera) ambayo yanauzidi udhaifu huo.

Kwa maneno mengine, wakati tunapoishi katika maisha haya tukijua fika kwamba si yakudumu nanimtihani tu kwaajili ya kile kinachokuja, hatutajisahau n akuponda raha tukipuuza mipaka ambayo Allah ‘AzzawaJalla’ ameiweka.

Abu Huraira (Allah amridhie) amemripoti Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema za Allah na amani zimshukie) akisema: “Allah haangalii nyuso zenu wala malizenu isipokuwa anaangalia nyoyo zenu na matendo yenu.” [Muslim].

Na ufahamu sahihi wa udhaifu wa maisha haya unatusaidia kushughulikia majanga wakati yanapotukabili. Mfano mzuri tunaoweza kujifunza ni pale alipofariki Saad bin Muadh (Allah amridhie). Mama yake alipokuwa akilia, Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) alimwambiahivi:

“Machozi yako yatapoona huzuni yako kupungua iwapo utajua kwamba mtoto wako n imtu wa kwanza ambaye Allah ametabasamu kwaajili yake n aArshi yake imetetemeka.” [AtTabarani].

Kufikiria kuhusu udhaifu wa maisha kunapaswa kutufanya tutake kurekebisha maisha yetu, kwa kuelewa lengo letu hasa katika maisha.

Kufikiria kuhusu udhaifu wetu kunapaswa kutuhimiza kuisoma dini yetu ili kuelewa kwa kina wajibu wetu kwa Allah ‘AzzawaJalla’, na hivyo tuwezekufanya kila kitu ndani ya uwezo wetu kukaambali na makatazo yake.

Pia, kufikiria kuhusu udhaifu kunapaswa kutufanya tutamani kuona kila ‘hukmu’ ambayo Allah ‘AzzawaJalla’ ameileta inatekelezwa kikamilifu na sisi tukiwa sehemu ya harakati za kuurejesha Uislamu katika nafasi yake ya juu.

Mwenyezi Mungu anasema: “Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache.” [Qur’an, 9:38].

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close