4. Darasa La Wiki

Kila la kheri washiriki, waandaaji mashindano ya Qur’an

Mwezi wa Ramadhani ni mwezi bora kuliko miezi yote, na moja kati ya saba- bu ya ubora wake ni kule kuter- emshwa katika mwezi huu Qur’ an Tukufu kama ilivyothibiti ndani ya Qur’an:“Mwezi wa Ra- madhani ndio ambao imeterem- shwa Qur’ an ili iwe uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uon- gofu na upambanuzi (wa baina ya haki na batili)”(2:185). Bila shaka hii ni heshima kubwa kwa Waislamu na dini yao na ni kwa ajili hii, kila un- apoingia mwezi wa Ramadhani, taasisi na vituo mbalimbali vya Kiislamu huandaa hafla za mashindano ya kuhifadhi Qur’an ambayo baadhi tayari yameshafanyika huku mengine yakitarajiwa kufanyika siku za karibuni. Mashindano haya kwa nam- na moja au nyingine ni darasa muhimu katika kuwashawishi Waislamu wa makundi tofauti kujifunza na kuhifadhi Qur’an. Sisi Gazeti la Imaan tuna- wapongeza washiriki wote wa mashindano ya mwaka huu pamoja na walimu wao walio- weza kuwafundisha, kuwahifa- dhisha hadi kufikia kiwango walichopo, llah awalipe kheri duniani na akhera. Ukweli ni kwamba, kuna vija- na wengi wa Kiislamu ambao hujiingiza kwenye mambo ya upuuzi na maasi ambayo ni har- amu katika dini.Ikiwa hali ni hiyo, hatuna budi kujitolea kwa kuwasaidia vijana wetu walioa- mua kujishughulisha na kuhifa- dhi Kitabu cha Allah (Qur’an) ili kuhakikisha wanafikia malengo yao. Allah anatuambia ndani ya Qur’an: “Na saidianeni katika wema na uchamungu.Wala msi- saidiane katika dhambi na uad- ui,” (Qur’ an, 5:2). Aya hii inatufunza juu ya kuyawajibikia mambo ya kheri ikiwemo kuwaunga mkono na kuwasaidia washiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an kwani wamekuwa wakionesha umahiri mkubwa katika kuhifadhi Qur’an Tukufu. Pia tunatumia fursa hii kupongeza na kutoa shukrani zetu za dhati kwa taasisi na vituo vinavyoandaa mashindano ya Qur’an pamoja na wale wanaoji- tolea ufadhili na zawadi.Tu- naamini wengine wataiga mfano wao. Tunalazimika kuzipongeza taasisi hizo kutokana na juhudi kubwa wanazozifanya kwani kuna taasisi na vituo vingi am- bavyo hutumia neema ya mali waliyopewa na Mwenyezi Mun- gu katika mambo yasiyo na manufaa na dini huku vingine vikiishia kufadhili mashindano ya kishetani. Tunawatakia maandalizi mema washiriki pamoja na waandaaji wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur’an, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ibada ya funga ya Mwezi Mtuku- fu wa Ramadhani. Mwisho tunatoa wito kwa taasisi za dini, watu binafsi pamoja na makampuni mbalim- bali yenye mapenzi na Uislamu kufadhili mashindano ya Qur’an kwani kufanya hivyo kuna fadhi- la na malipo makubwa mbele ya Allah.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close