4. Darasa La Wiki

Funga ni zaidi ya kuacha kula na kunywa

Ramadhani ni mwezi ambao Allah ameufadhilisha na ku- upa hadhi ya kipekee. Mion- goni mwa fadhila zinazopatikana ndani ya mwezi huu mtukufu ni waumini kusamehewa mad- hambi, kufungwa milango ya moto na kufunguliwa milango ya pepo.

Pia, ndani ya Mwezi wa Ram- adhani, hupatikana usiku bora (Laylatul Qadr), usiku ambao Muislamu akidiriki kufanya iba- da hupata malipo ya miezi elfu (au miaka 84).

Kama inavyofahamika, Ram- adhani ni masiku machache laki- ni yenye thawabu na fadhila ny- ingi ambazo hazipatikani katika

miezi mingine. Hivyo, hatuna budi kufanya yale yote ambayo yatatupelekea kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kama ana- vyobainisha ndani ya Qur’an tukufu: “(Funga ni) katika masiku machache yenye kuhesa- bika…,”(Qur’an, 2:184).

Lakini, ili tuweze kuchuma neema mbalimbali na thawabu zitokanazo na swaumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ni muhimu kuchunga masharti ya swaumu kwa kuzingatia yale yote tunayopaswa kuyaacha.

Wengi miongoni mwetu Waislamu, tunadhani kuwa swaumu ni kujizuia kula na kunywa tu. La hasha! Swaumu si

kujizuia kula na kunywa tu. Ni zaidi ya hapo.

Ukiacha kujizuia kula na kunywa, tunapaswa pia kujizuia na mambo mengine ya maasi ikiwemo kusema uongo, kutuka- na, kusengenya, kufitinisha, kutazama haramu, na kadhalika.

Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie): “Yeyote am- baye hatoacha kusema uongo, kusengenya, kufitinisha, kutoa ushuhuda wa uongo, basi ajue kuwa Allah hana haja na swau- mu yake katika kuacha chakula chake na kinywaji chake,”(Bukhari na Muslim).

Ni jambo la kusikitisha kuwa wapo wanaokula rushwa na ku-

chuma riziki zisizo za halali. Baa- dhi ya wafanyabiashara wana- pandisha bei za bidhaa zitumika- zo kwa futari kwa kuona ndiyo fursa ya kujiongezea kipato .

Baadhi ya akinamama wa- natembea uchi barabarani na ku- jipamba kwa manukato na mapambo mengine ya haramu wakidhani kutokula na kunywakatika mchana wa Ram- adhani kumetosha swaumu zao kukubaliwa na Mwenyezi Mun- gu. Huko ofisini, watu wanafun- ga na huku wakijihusisha na uba- dhirifu wa mali za umma na kula rushwa kwa kudhani kuwa ku- fanya hivyo si dhambi.

Ni jambo la kusikitisha kuwa,

katika kipindi cha Mwezi wa Ra- madhani watu ndiyo huanzisha vikao vya vibarazani na kujihusi- sha na michezo ya pumbao kama karata, bao na michezo mingine isiyokuwa na faida, wakati tuna- chopaswa kufanya ni kushindana katika kufanya ibada.

Hayo, tuliyoyataja ni mach- ache kati ya mengi tunayoyafanya na kuharibu swaumu zetu. Hivyo ni wajibu tutumie mwezi huu ku- fanya yale yaliyo mema ikiwemo kusoma Qur’an kwa wingi, kuleta dhikri mbalimbali, kuswali swala za usiku, kuhudhuria darasa mbalimbali, kukaa itikafu, kutoa sadaka, kutubia na kumuomba msamaha Allah.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close