4. Darasa La Wiki

Funga na malezi ya nafsi

Allah ameifanya funga kuwa ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu, akaifanya kuwa ni faradhi kwa kila mwenye kulazimmika kisheria. Allah amewasemesha watu kwa sharia hii na akawaita wale wenye kuamini kwa sababu wao ni wepesi sana kuitikia wito wa Allah na kuufanyia kazi baada ya kuusikia.

Allah ameifanya funga kuwa ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uisla- mu, akaifanya kuwa ni faradhi kwa kila mwenye kulazimmika kisheria. Allah amewasemesha watu kwa shar- ia hii na akawaita wale wenye kuamini kwa sababu wao ni wepesi sana kuiti- kia wito wa Allah na kuufanyia kazi baada ya kuusikia.

Allah akasema: “Enyi mlioamini! Imewajibishwa juu yenu funga, kama ilivyowajibishwa juu ya wale walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha- Mungu,” (Qur’an 2:183)

Aya hii inatuonesha kuwa watu walioamini ndiyo ambao hutukuza amri ya Allah wakaipa uzito unaosta- hiki na kuifanyia kazi. Pia Aya hii ina- bainisha Allah amewajibishia funga umma huu, kama alivyoiwajibisha kwa umati zilizotangulia. Kwa hiyo funga si ibada ngeni. Kila umma ume- kuwa ukiitekeleza kutokana na faida yake.

Imebainishwa kuwa Allah amei- wajibisha funga si kwa sababu ya ku- wafanya watu washinde na njaa tu au kiu bali ni kwa malengo maalumu, kuitakasa nafsi, kuipamba na kuiten- geneza kwa ajili ya kumcha Allah.

Funga haisimami katika kuacha kula na kunywa peke yake bali ni ku- hakikisha kuwa viungo vyote vinaji- zuia. Ibada hii inamrithisha mja ucha- mungu na kumfanya asikosekane ka- tika yale aliyoamrishwa na Allah; na asipatikane katika yale aliyokatazwa.

ivyosema baadhi ya ulamaa, ni sawa na gulio ambalo limewekwa sehemu kisha likaondoshwa, wakawa wame- pata faida baadhi ya watu na wengine wamepata hasara.

Ramadhani ina faida nyingi, ikiwemo malezi ya kitabia ambayo yanaathari kubwa katika nafsi ya mja. Malezi hayo yanamwandaa Muisla- mu kuwa katika mazingira mazuri ya kumcha Allah wakati wote na kujenga misingi imara katika nafsi ya mtu ili kufikia malengo ya swaumu.

Hapa tutataja tabia ambazo mtu akiwa nazo anakuwa amepata faida katika mwezi wa Ramadhani.

Ikhlas

Amefuzu ambaye ameijenga nafsi katika tabia ya utakasifu wa nia na kuzifanya ibada katika hali ya kumta- kasa na kumkusudia Allah peke yake huku akitekeleza funga na kisimamo chake cha Ramadhani katika utakasi- fu wa nia.

Umefunga siku 29 au 30 na funga imekufundisha namna ya kuwa ma- kini katika kauli zako na matendo yako kiasi kwamba ukizungumza uzungumze yanayomridhisha Allah na ukifanya iwe ni kwa ajili ya kutaka radhi za Allah ukiamini wewe ni mtumwa wake.

Hakuna nafasi ya uongo au udan- ganyifu katika ibada ya funga. Hii ni ibada inayokufundisha namna utakavyomkusudia Allah katika ma- tendo, kumchunga na Allah katika kila jambo. Allah amesema katika Ha- dithul Qudsi: “Funga ni yangu mimi nami ndiye ninayeilipa” .

Ikhlas haionekani kwa macho wala haisikiki kwa masikio, bali athari yake huonekana katika matendo ya waja. Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie amesema: “Uchamungu upo hapa (akaashiria katika kifua chake mara tatu).” ni ishara ya wazi kuwa Ikhlas ni siri iliyofichikana kati

adhimu inajengeka vema na kuimari- ka kupitia ibada ya funga, ibada am- bayo ni siri kati ya mja na Mola wake.

Funga inafundisha uvumili- vu (subira) katika kumtii Allah

Ni hakika isiyojificha kuwa subira kubwa ni pale inapokuwa mja amesubiri na kuvumilia katika jambo ambalo nafsi inalipenda. Mengi am- bayo waja wametakiwa kujizuia nayo ndani ya funga ni mambo ambayo nafsi inayapenda.

Umar bin Al-Khattwab (Allah am- ridhie) amesema: “Tuliipata ladha tamu ya maisha yetu katika subira (uvumilivu).”

Wanazuoni wameigawanya subira katika vigawanyo vitatu, kusubiri juu ya kumtii Allah, kusubiri kutokana na maasi na kusubiri juu ya makadirio mazito (matatizo) aliyokukadiria Al- lah.

Funga inaingia katika sehemu kubwa ya aina hizi tatu za subra, kwani ndani ya funga nafsi inatakiwa kuvumilia katika kudumu juu ya utii wa mola wake, inatakiwa ivumilie kwa kuacha maasi na inatakiwa ivumilie machungu yanayotokana na funga yakiwemo njaa na kiu.

Kujizuia na machafu

Katika ibada ya funga mja anaji- zuia na baadhi ya mambo halali katika mchana wa mwezi usiokuwa wa Ra- madhani kama vile kula kunywa pamoja na kukutana na mke wake . Hii ni njia ya kuizoesha nafsi namna ya kujizuia na yale ambayo Allah am- eyakataza na kuyawekea mipaka kati- ka maisha ya mwanadamu.

Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie) amesema: “Mtu asiyeacha kusema uongo na kuufanyia kazi Al- lah hana haja na kuacha kwake mtu huyu kula na kunywa.” Na pia “Ikiwa

siku mmoja wenu amefunga asiongee Kwa hivyo mwezi huu, kama wal- ya mja na Mola wake. Tabia hii maneno machafu wala asipige

makelele wala asifanye vitendo vya ki- jinga na ikiwa mtu atamtukana au kumpiga basi amwambie mimi nime- funga.”

Haya ni malezi bora ambayo yana- patikana katika ibada ya funga, yak- ilenga kuidhibiti nafsi na kuzuia viun- go katika mambo aliyoyaharamisha Allah. Ni wajibu kuhakikisha kuwa viungo vyote vinafunga katika yale ali- yoyakataza Allah. Ikiwa umefunga katika vile alivyovihalalisha Allah, ni wajibu pia kufunga katika vile alivyo- viharammisha.

Fungandiyo ponyayamatamanio yote, ni ibada yenye taathira kubwa katika kuhifadhi na kulinda viungo, ndiyo nguvu ya ndani inayoweza kui- dhibiti nafsi na kudhibiti viungo kati- ka yale aliyoyakataza Allah.

Hata hivyo, hayawezi kupatikana hayaisipokuwa kwamambomatatu, kujizuia na matamanio ya tumbo na tupu, kuvumilia kwa kuacha maasi ya aina zote na kufunga kwa ajili ya kum- tii Allah kwa kumtakasia nia na wala si kufunga kwa ajili ya mazoea au kuiridhisha jamii.

Kulea nafsi katika kuvidhibi- ti viungo

Tuchukue mfano wa kiungo kimo- ja ambacho kinadhibitiwa sana katika funga, nacho ni ulimi. Mtume (rehe- ma za Allah na amani zimshukie) amekataza mwenye kufunga kutuka- na, kupiga makelele, kuzungumza mazungumzo ya kijinga, kusengenya na mengineo.

Haya yote ni matendo ya ulimi, ki- pande kidogo cha nyama ambacho Allah Aliyetukuka kwa uwezo wake amekipa uwezo wa kusema, lakini kinaweza kuwa ni sababu ya kuanga- mia kwa mja au kuokoka na adhabu za Allah.

Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie) amesema: “Muislamu wa kweli ni yule ambaye wamesalimika Waislamu kutokana na ulimi wake na mkono wake,” (Muslim) , na akasema tena: “Yoyote anayemwamini Allah na siku ya mwisho azungumze maneno mazuri au anyamaze,” (Bukhari na Muslim).

Kuilea nafsi katika tabia ya upole na kufanya wema

Ni katika mwezi huu wa Ramad- hani watu kuwahurumia na kuwa- saidia wanyonge ili waweze kuitekele- za ibada ya funga. Hili ni jambo am- balo linaacha taathira kubwa katika nafsi ya mja baada ya Ramadhani na kumfanya awe na huruma na mwenye kupenda kuwafanyia ihsani watu kutokana na mazoea mazuri aliy- okuwa nayo ndani ya Ramadhani.

Kudhibiti hasira

Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie) amesema: “Mwenye ngu- vu si yule mwenye kushinda kwa mieleka lakini mwenye nguvu ni yule anayeweza kuimiliki nafsi yake wakati wa kughadhibika.”

Katika ibada ya funga, nafsi inaji- funza namna ya kujidhibiti inapoka- sirishwa ikiwa ni sehemu ya kulinda malipo ya funga yasipungue.

Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie) anatufundisha kuwa iki- wa mmoja wetu atatukanwa au ku- pigwa basi aseme mimi nimefunga, na asilipize maneno hayo machafu au kumpiga yule aliyempiga. Haya ni ka- tika malezi yenye taathira kubwa tu- nayoyapata ndani ya ibada ya funga katika nafsi ya mja.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close