4. Darasa La Wiki

Darasa za ramadhani zituongoze katika kumcha allah vilivyo

Darasa za Ramadhani ni moja ya vikao muhimu vinavyoweza kumbadilisha Muislamu kutoka kwenye maisha ya uchaji viumbe/vitu hadi UchaMungu. Dar- asa hizi ambazo nyingi hufanyika misikitini nyakati za jioni, zimekuwa na umuhimu mkubwa hususan katika zama hizi ambapo Waislamu hawana hima ya kusoma dini yao. Kuna mengi ya kujifunza kupitia darasa za Ramadhani ikiwa ni safari ya kuelekea kwenye maisha anayoyaridhia Allah Ta’ala. Miongoni mwa mambo hayo ni kumtii Al- lah kwa aliyoyakataza, kupendana, kukir- imiana, kuvumiliana, kusameheana, ku- saidiana na kuoneana huruma. Hata hivyo, changamoto za maisha kwa kiasi kikubwa zinachochea idadi ndogo ya Waislamu wanaohudhuria darasa za Ram- adhani. Hali hii imetokana na dhana potofu ya baadhi ya watu kuwa kujifunza elimu ya dini ni wajibu wa watu fulani fulani, jambo ambalo linaonesha tulio wengi hatujaipa elimu ya dini uzito unaostahiki kama tufan- yavyo katika elimu ya mazingira. Pamoja na changamoto hizo, Masheikh mbalimbali wamekuwa wakiendelea na darasa za tafsiri ya Qur’an, Tawhiid na Fiqhi misikitini, licha ya idadi ndogo ya wanao- hudhuria. Kitendo cha Waislamu kutohudhuria darasa misikitini ni sawa na kuikimbia jihad kutokana na ukweli kuwa, kujifunza elimu ni mojawapo ya vigawanyo vya jihad. Anas bin Malik (Allah amridhie) ameha- dithia kuwa Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Mwenye kuto- ka kwa ajili ya kutafuta elimu (basi atakuwa mtu) huyo yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka atakaporejea,” (Twabraniy). Na katika Hadithi nyingine, Mtume amesema: “Mwenye kwenda msikitini akawa hataki ila kujifunza kusoma kheri au kufundisha kheri atakuwa mtu huyo na ujira kama aliyehiji hijja yake iliyotimia,” (Twabraniy). Ikiwa Waislamu hawana utayari wa kuji- funza dini yao, kuna uwezekano pia baadhi yao hawatambui lengo na umuhimu wa ibada mbalimbali anazozifanya ndani ya Mwezi wa Ramadhani. Sababuhiinanyinginezondiyo inayow- afanya wengi wasifikie lengo la funga (Ucha- Mungu). Ili tuwe WachaMungu wa kweli hatuna budi kufanyia kazi yale yote tunayojifunza katika darasa za Ramadhani sanjari na kuachamambo yasiyotuhusu,nahuondiyo uzuri wa Muislamu. Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Katika uzuri wa Muislamuwamtuni kuachalisilokuhusu,” (Tirmidhiyy).Jambo jingine la kuzingatia ili kuufikia UchaMungu ni kujenga urafiki na watu wema watakaotuongoza katika mambo ya kheri kwani Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Mtu hufuata dini ya rafiki yake, kwa hivyo muangalie unayemfanya rafiki,” (Abu Daud na Tirmi- dhiyy). Kadhalika, mmoja wa wanachuoni ali- wahi kusema: “Kuweka uhusiano mzuri na watu wema, matokeo yake ni kupata elimu iliyo na faida, tabia nzuri, na matendo mema, ambapo kuweka uhusiano na walio- potoka, huzuia hayo mema yote.” Darasa za Mwezi wa Ramadhani zina mchango mkubwa katika kuhakikisha len- go la Ramadhani linafikiwa na pia athari ya maleziitumikekuwa chachukwawafungaji ili kuwaletea mabadiliko ya kitabia na mienendo katika miezi mingine. Ni vema Waislamu kuzingatia lengo la msingi la swaumu ambalo ni UchaMungu. Kitendo cha kufanya ibada katika Mwezi wa Ramadhani pekee huku tukiacha kufan- ya ibada miezi mingine kunajenga taswira yaushirikinakwaniAllah Ta’alahayupoka- tika Ramadhani tu bali yu hai siku zote na wala hafi. Hivyo, jukumu la ibada ni la siku zote. Allah anatuambia ndani ya Qur’an: “Enyi mlioamini, ingieni katika Uislamu wote, wala msifuate nyayo za shetani, kwa hakika shetani kwenu ni adui wa wazi,” (Qur’an, 2:208). Ni namna gani tutafaidika na Ramadha- ni? Swali hili haliwashughulishi watu isipokuwa wenye imani pekee. Kwani hao ni wenyekujuafadhila zinazopatikanakatika mwezi huo na hivyo basi huwa na pupa na hamu ya kuhakikisha wanafikia lengo kwa Tawfiki ya Allah Ta’ala. Allah anasema: “Hakika WachaMungu watakuwa katika mabustani ya mito. Katika makazi ya haki kwa Mfalme mwenye uwe- za,” (Qur’an, 54:55). Kumcha Allah ambao ndiyo msingi mkuu na sababu ya kuumbwa mwanadamu kunapaswa kuwepo siku zote za maisha yetu. Hata hivyo lengo hili halifikiwi na Waislamu wengi licha ya malezi ya kiimani na kiitikadi yatolewayo na Masheikh katika darasa za kila siku za Mwezi wa Ramadha- ni. Hivyo basi, mwezi huu uwe ni chachu ya mabadiliko kwa Waislamu kutekeleza amri za Allah ipasavyo na kuacha makatazo. Al- lah atujaalie tuwe miongoni mwa wenye kumuabudu yeye mpaka mwisho wa uhai wetu, atupe kheri za dunia na akhera, pia atuzidishie elimu na atufungulie milango ya fahamu. Aamin!

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close