2. Aliyeslimu

STELLA NJAMA; Bibilia Ilivyotumika Kumbadilisha Hadi Kusilimu

Kwa wafuatiliaji wa safu hii, tunayemzungumzia leo ni ndugu wa Mariam Njama ambaye kisa chake tumekieleza wiki chache tu zilizopita. Mdogo wake huyu alizaliwa kwa jina la Stella Wildbad Njama lakini sasa anaitwa Jamila. Jamila alizaliwa Moshi kijiji cha Kikavu mwaka 1992, na alipata elimu yake huko katika shule ya Kikavu chini, akitokea katika familia ya waumini wazuri wa dini ya Kikristo katika dhehebu la Lutheran. “Katika familia yetu, asilimia kubwa ni viongozi katika Makanisa, kwa hiyo tulilelewa katika misingi ya kiimani sana. Baba yangu akiwa baba kiongozi kanisani, na mama pia alikuwa kiongozi”, anasema Jamila. Kwa sababu ya kutokea katika familia iliyoshiba Ukristo na huku wazazi wakiwa ni viongozi, Jamial anasema alibatizwa akiwa mdogo. Nilimuuliza Jamila ikiwa alijua chochote kuhusu Uislamu kabla ya kusilimu, lakini kwa mujibu wa Jamila kanisa lake lilikuwa tofauti na makanisa mengine ambayo huwamezesha waumini wao sumu kuwa Waislamu wanaabudu mashetani. Jamila anasema yeye hakujua chochote kuhusu Uislamu kwa sababu kanisa lake halikuwa na maelekezo yoyote kuhusu imani nyingine. Moja ya kazi kubwa ambayo aliwahi kuifanya wakati akiwa kinda la Kikristo ni kufundisha katika Sunday School, ambako watoto wa Kikristo hukusanyika kwa ajili ya ibada na mafunzo ya dini yao. Kusilimu Safari yake ya kusilimu ilianza takriban miaka miwili mara baada ya kuhamia jijini Dar es Salaam mwaka 2010, akijishughulisa na kazi yake ya ufundi nguo. Mwaka 2012, Jamila alikutana na kijana wa Kiislamu na kuanza kufanya naye mazungumzo ya kidini mara kwa mara. Kijana huyu alimshauri Jamila kubadili dini, lakini naye aligoma kutokana na umadhubuti wa imani yake ya Kikristo aliokuwa nao wakati huo. Kwa mujibu wa Jamila: “Kubadili dini lilikuwa ni jambo gumu sana kulingana na imani ambayo nilikuwa nayo na mazingira ambayo nililelewa. Nilikuwa nimeiva kiimani kiukweli”. Baada ya kugoma kusilimu, kijana yule akawa anayahamishia mazungumzo yao na kuyapeleka katika vitabu vyote viwili, kwa maana ya Bibilia na Qur’an. “Mungu alimjaalia kijana yule kuwa na uwelewa mzuri wa Bibilia na Qur’an, kwa hiyo akawa ananielewesha kuhusu upotofu wa baadhi ya niliyokuwa nikiyaamini”. Jamila anakiri kuwa mengi kati ya aliyokuwa akiyaamini hakuwa na hoja ya kuyatetea. Aliamini kibubusa tu. “Wakati kijana yule ananielezeka, alikuwa akitumia zaidi Bibilia na kunipa usahihi wa vifungu ambavyo nilikuwa nimefunzwa tofauti katika kanisa langu . Mfano wa jambo moja ni ndoa na talaka ambapo Jamila alikuwa akiwashutumu Waislamu kwa kuachana kwa sababu alijua katika Ukristo hakuna jambo la kuachana. Hata hivyo, kijana yule alimueleza kuwa talaka ipo hata katika Bibilia, huku akimnukuu Yeremia 3:8, “Nami nikaona, wakati nilipokuwa nimemwacha Israeli mwenye kuasi, nikampa hati ya talaka kwa sababu hiyo ya kuzini, dada yake, Yuda mwenye hiyana, hakufanya hofu; bali yeye naye akaenda akafanya mambo ya ukahaba”. Pia, Mathayo (1: 19) inasema: “Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri”. Hapo ndipo Jamila alipojifunza kuwa ndoa inavunjika kwa misingi ya dini zote kwa sababu Bibilia nayo imeruhusu talaka, na kwamba ni Wakristo wenyewe tu ndiyo walioamua kuyabatilisha baadhi ya mambo. Yapo mengi ambayo yapo katika vitabu vyote alielezwa usahihi wake, ikiwemo pia kufunga na kusherehekea Idi. Jamila anasema: “Ikawa kila ambalo mimi nampinga yeye alikuwa ananifunulia katika Bibilia, vingine ni vitu ambavyo nilikuwa sijawahi kuvijua”. Jamila anasema wakati fulani alikuwa akitamka jambo katika Biblia lakini anashindwa kujua imeelezwa wapi katia Bibilia, lakini kijana yule akawa anamueleza ipo kitabu gani na kifungu cha ngapi. “Hapo ndiyo mwanzo wa kujua kuwa kumbe nilikuwa ninapotea, na nikaanza kupata wasiwasi na imani yangu. Nilianza kugundua kuwa kumbe napingana na mambo ambayo yapo hata katika Bibilia,” anasema Jamila Jamla anasema akagundua kuwa kuna mambo mengi ambayo makanisa wamebatilisha ambayo yameandikwa na yapo. “Baada ya kuridhika na hoja zake, n i k a s i l i m u Ma c h i , 2 0 1 3 ”, anasimulia Jamila. Wiki moja baada ya kusilimu, Jamila akaanza madrasa lakini anasema haikuwa changamoto kubwa kwake kujifunza dini hiyo tukufu kwa sababu alikuwa anafanya jitihada nyingi binafsi zilizokuwa zikimpa unafuu anapokutana na mwalimu. Miongoni mwa jitihada alizokuwa akizifanya ni panoja na kutumia kitabu, ‘Mafundisho ya swala’, kujifunza nyumbani jinsi ya kuswali kabla ya kwenda darsa. Kwa sasa Jamila bado anaendelea kuusoma Uislamu na habari njema ni kuwa yule kijana ambaye alikuwa chanzo cha yeye kusilimu, kwa sasa ndiyo mume wake wa ndoa. Ujumbe wake kwa Waislamu ni kuisoma dini ya Allah kwa sbabau anasema kusoma si hiyari ya mtu ila ni lazima na anawataka Waislamu wadumu katika swala tano kwa sababu ni moja ya nguzo katika Uislamu. Jamila pia ameomba Waislamu hasa walinganiaji, kuzidi kuwa kuwarai Wakristo na kuwapa dawa ili nao waifahamu njia ya Allah iliyo ya haki.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close