2. Aliyeslimu

Kumtendea wema mzazi kulinifanya nisilimu

Morgan Alfred Mdete, baba wa familia ya mke na mtoto mmoja alifunga ndoa na kuishi maisha ya familia ya Kikirsto, lakini aliihama imani yake akitafuta uhuru wa kumtendea wema mzazi.

Mwenyezi Mungu anatueleza ndani ya Qur’an: “Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila yeye tu na ameagiza kuwafanyia wema mkubwa wazazi kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe au wote wawili basi usiwaambie hata Ah! Wala usiwakemee na useme nao kwa msemo wa hishima kabisa.” [Qur’an 17:23].

Mdete amabye ni mzaliwa wa Wilaya ya Morogoro Mjini, mtaa wa Mwigole, ni mtoto wa mwisho kati ya saba kwa Bw. Alfred Mdete na mtoto wa tatu kati ya watoto wanne wa Bi. Nuru Ali.

Katika Ukristo Mdete alikuwa akiabudu katika dhehebu la Roman Katoliki (RC), ambako alibatizwa, akapewa Kimaimara na hata kufunga ndoa. Kanisa alilokuwa akihudhuria ni lile la Roho Mtakatifu (Kwa Winga) lililopo maeneo ya Kiwanja cha ndege, Morogoro Mjini. Mdete alikuwa mhufhuriaji mzuri wa ibada na pia ametembelea makanisa mengi. amesali makanisa
mengi.

Kusilimu

Mdete alisilimu baada ya mama yake mzazi kupata maradhi yalimfanya asiweze kufanya jambo lolote bila msaada.

Siku moja, baada ya Mdete kutoka kazini, mama yake alimuomba amletee
maji ya kunywa, lakini mkewe alimkataza asimpe.

Hapo Mdete alianza kujiuliza maswali na kuingiwa na mawazo: Kwa nini mke wangu anikataze kumpa mama maji? Hioi amelifanya nikiwepo, je nisipokuwepo anafanya mangapi? Aliwaza kwa nini Uislamu unaruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja? Aligundua kuwa, falsafa ya mke mmoja ina udhaifu kwani hali ya kumfunga mume inampa jeuri mwanamke.

Baada ya kujiuliza na kutafakari sana, Mdete alifanya maamuzi ambayo yalimuwezesha kumuhudumia mama yake na pia asimpoteze mke wake aliyempenda mno.

Ingawa Mdete anakiri kuwa sio kila anayeoa mke wa pili katika Uislamu ana matatizo na mke wake, yeye aliona kwake kuongeza mke ni jambo sahihi zaidi ili apate fursa ya kumfanyia ihsani mzazi.

Ilikuwa ni mwaka 2015 Mdete alipotamka Shahada, akikiri hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na Muhammad (rehema za Allah na amani zimshukie ni Mtume wake).

Mdete aliingia katika imani inayomruhusu kuwa na wake zaidi ya mmoja ili mke wa pili akamfanyie wema mama yake.

Mke wa kwanza hakukubali uamuzi wa Mdete kuongeza mke wa pili, hivyo akaamua kwenda kumshitaki mumewe kwa kiongozi wa dini aliyewafungisha ndoa kanisani. Kosa aliloshtakiwa Mdete ni kubadili dini na kuongeza mke wa pili.

Kiongozi wao aliwashauri warudi kuzungumza katika familia, lakini baadae mambo yakafika Mahakamani. Mdete alikiri kusilimu na kuoa mke wa pili na hivyo basi, ndoa ilivunjwa.

Hadi sasa Mdete ni Muislamu, baba wa familia mwenye mke mmoja. Licha ya mwezi uliopita kuondokewa na mama yake mzazi ambaye amekuwa akiumwa kwa karibu miaka minne, Mdete anamshukuru Mwenyezi Mungu kwani anasema baada ya kuoa alishirikiana vema na mke wake kumhudumia mzazi wake hadi mauti yalipomfika. Allah amfanyie wepesi.

Baada ya Kusilimu

Mdete anasema hajawahi kujutia uamuzi alioufanya. Mdete anasema ukilinganisha na alipotoka, anapendaibada za Kiislamu kwani mwanaume na mwanamke hawakai sehemu mmoja. Pia anapenda mavazi ya stara ya wanawake. Kwa Mdete, anaona Uislamu ni mfumo wa maisha, unaoelekekeza namna ya kufanya kila kitu, hata jambo doho kama dua ya kuingia chooni.

Katika Ukristo, mtu anaenda kuungama kwa kiongozi na kumueleza dhambi zake za siri ili amsamehe; lakini katika Uislamu toba ni kati ya mja na Mola wake. Katika Uislamu, Mwenye uwezo wa kusamehe ni Mwenyezi Mungu na mtu anatubu kwa siri kwa Mola wake sio kwa Sheikh.

Nasaha

Mdete anawanasihi Waislamu kuwapenda wake zao ila upendo huo usiwe sababu ya mtu kujisahau na kutowatendea haki wazazi wake.

Pia Mdete anawakumbusha Waislamu kumcha Allah kutokana na neema mbalimbali alizowajalia ikiwa ni pamoja na kutoa fursa kwa wanaume ya kuoa mke zaidi ya mmoja kwa wenye uwezo jambo ambalo anasema hekima yake ni kubwa na huwezi kuipata ila katika Uislamu.

Kwa wasiokuwa Waislamu, Mdete anawaambia kuwa Uislamu ni dini nzuri, waingie ili waone uzuri wake au wawaulize wajuzi wawaambie ubora wa Uislamu.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close