1. TIF News2. Aliyeslimu

Albert Alexender Ngalwa: Mestant aliyeamua Kumbwagia virago padri Kanisa Katoliki

Ngalawa ambaye kabla hajaiona nuru ya Uis- lamualikuwaakiitwaAlbertAlexender, alizaliwa miaka 38 iliyopita Wilayani Kilombero mkoani Morogoro akiwa ni mtoto wa nne wa familia ya mzee Alexender Ngalawa.

Maisha yake kabla ya kusilimu

Nilikutana na Bakari mtaa wa Karume mjini Morogoro ambapo aliniambia alianza shule ya msingi mwaka 1990 na kuhitimu darasa la saba mwaka 1996 katika shule ya msingi Nyanduo iliy- oko Kilombero. “Lakini nikiwa bado mwanafunzi wa shule ya msingi, nilitokeakuupendasanaUkristohaliiliy- osababisha kupewa mafunzo ya miezi tisa ya sakramenti ya komunio na nilipokea hekarist yangutakatifu”, Ngalawaalianzakufunguka. Mapenzi yake kwa Kanisa Katoliki pamoja na mafunzo aliyopewa yalimpandisha hadhi kiimani na kufanikiwa kuwa miongoni mwa wasaidizi wa karibu wa Padre ambaye ni kiongozi wa Ibada zote kanisani. “Niliteuliwa kuwa mmoja wa Mestant wa Pa- dri katika sala za kawaida kwa upande wa kwanza, na sala za siku za sikukuu kwa ujumla wake, ” al- isema na kufafanua: “Mestant ni wasaidizi wa ka- ribu wa Padri katika Kanisa Katoliki, ambapo kwenye ibada za siku za Jumapili tulikuwa wanne lakini siku za sikukuu tunakuwa 6-12”. Alipomaliza shule ya msingi, Ngalawa haku- fanikiwa kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, na hivyo Ngalawa alisafiri na kwenda Mavimba kuishi na mama yake. Wakatiakiwahapo, sikumojabibiyakemzaa mama alimuuliza mjukuu wake Albert, sasa Bakari, kwa nini hajamuona akienda kanisani tokea aje hapo kwa mama yake? “Nilimuuliza bibi, ‘KwanihapaKanisalipowapi, mbonamiye sijaliona toka nije’”? Bibi akanijibu kuwa wana- sali kule shule. “Ndipo nilimwambia, ‘Siwezi kwenda kusali huko sababu najua shule kazi yake ni kusoma siyo kusali, ” Ngalawa alihadithia kwa makini! Kutokea hapo, Ngalawa alisema alikaa kwa takriban mwaka mmoja bila kuingia kanisani mpaka mwaka 1998 alipofunga safari kwenda Dar es Salaam kuwatafuta ndugu zake aliodai wa- likuwa wakiishi katika jiji hilo kwa miaka mingi pasipo kujuana nao.

Kusilimu kwake

Ngalawa kabla hajasafiri kuelekea Dar es Sa- laam na kabla pia hajamaliza shule ya msingi, al- isema kuna kitu kilikuwa kikimfurahisha sana al- ipowaangalia Waislamu. “Kwanza nilijikuta nikipenda kanzu zao nye- upe wanazovaa hasa siku za Ijumaa wakielekea msikitini. Lakini, pili kitendo chao cha kushinda na njaa na kiu, kutwa nzima, bila kuwa na mtu pembeni anayewasimamia. Nilishangaza mno,” alibainisha Ngalawa, huku akimkazia macho mwandishi.Alipofika Dar es Salaam alipokewa na wenyeji wake katika maeneo ya Kimara Baruti, na kwa bahati nzuri anasema miongoni mwa hao ndugu zake walikuwa Waislamu. “Huruma, busara na ukarimu wa wale ndugu zangu, nikajikuta ghafla nashawishika kuingia katika Uislamu, ingawa kila ninapoyakumbuka mafundisho ya Kanisa Katoliki, nilipata hofu, ” alisema kabla hajaongeza. “Hata hivyo nilikata shauri mwaka uleule wa 1998 ndani ya msikiti uliopo Kimara Baruti nika- silimu bila kunilazimisha mtu, na kisha nikaanza kuhudhuria masomo ya dini kwenye madrasa ili-yopo pembezoni mwa msikiti huo. ” Lakini Ngalawa anakiri kwamba, ushiriki wa mchezo wa mpira wa miguu kipindi hicho ak- ichezea Abajalo FC ya Sinza iliyokuwa daraja la kwanza, ulisababisha mahudhurio kuwa hafifu katika masomo ya dini. Baada ya hapo, gazeti hili likataka kujua iwapo kuna jambo lolote litakalobaki kwake kama kum- bukumbu mara tu alipoingia katika Uislamu. “Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni jambo ambalo siwezi kulisahau. Siku ya kwanza kufunga nilihisi dhiki, shida na mbaya zaidi nili- tamani kurudi kwenye Ukristo. Lakini nikajiuli- za, kwani nani alinilazimisha? Nilipojipatia jibu mwenyewe nikajikaza mpaka mwezi wote ukamalizika, ” alisimulia huku akicheka. Kutokea hapo, Ngalawa anasema hakuona tabu tena siyo tu kufunga faradhi, bali hata sunna. Hata ibada nyingine zilimuwia nyepesi. Hata hivyo, Ngalawa anasema awali, haku- pendelea ifahamike kuwa alisilimu. “Hali hiyo ili- nikuta hasa mwaka 2004 niliporejea Morogoro ambako msikiti wangu wa kwanza kuswali ulikuwa wa Boma road, nadhani sababu kubwa, imani ilikuwa haijapanda bara-bbara”, anajise- mea huku akitikisa kichwa kwa masikitiko. Aidha, historia ya Bakari Ngalawa, imekuwa tofauti na ya watu wengine wengi wanapouacha Ukristo na kurejea kwenye Uislamu katika eneo lile la kutengwa na wazazi wake! Ngalawa kwa upande wake, ameliambia gazeti hili kuwa, siku alipomwambia baba yake kuwa aliamua kubadili dini na kuwa Muislamu, naye masikio yake yakapata habari mpya! “Baba hakuchukia, wala kushtuka kusikia hatua niliyoichukuwa ya kuingia kwenye dini to- fauti na ya kwake bali alinambia hata yeye haku- zaliwa Mkristo, alikuwa Muislamu na kutokana na masharti ya kusoma, ndipo alibadili na kuwa Mkristo. “Mimi baba yako awali nilikuwa naitwa Has- san Omar Ngalawa, baba yangu alikuwa mion- goni mwa masheikh waliosomesha Waislamu dini. Lakini nilipokwenda shule, Padre aliweka sharti kuwa ili nisome lazima niwe Mkristo, ndiyo nikawa hivi”, Ngalwa alibainisha. KwamujibuwaNgalawa, inamaanakablaya hapo alikuwa hana habari hata ya historia ya mzee wake kuwa alizaliwa kwenye familia ya Waisla- mu. Na hapo ndipo anapopata majibu ya sababu ya baadhi ya ndugu zake wa damu aliowaendea jijini Dar es Salaam mwaka 1998 kuwa ni Waislamu!

Maisha ndani ya Uislamu

Mwandishi alitaka kujua anayatofautishaje maishakatikadiniyakeyazamani, namaishaya sasa ndani ya Uislamu. “MaishakatikaUkristosiyauhakika, hasapale Muumini anapoonekana kutaka kujua mambo, haturuhusiwikusomawalakuhoji. Kilakitundi- yoMzee. NitofautinahukukwenyeUislamuam- bako unaruhusiwa kuhoji kila unachoona kina mashakamashakakatikadini. Uislamusiyodini yakwendakibubusa, nidiniinayofuatamaandiko hasa,” alisema. Mwisho mbali ya kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba kwa kumjaalia leo kuwa kwenye dini ya Uislamu, Ngalawa aliwaomba wale wa- naofikiria kusilimu lakini wanahofia kutengwa na ndugunajamaazao, waigeujasiriwake. Anasema yeye wakati anaamua kusilimu hakujua kama baba yake an- geliona tukio hilo ni la kawa- ida, balialisemaliwalonaliwe, lakini Uislamu ndiyo chaguo lake. Hivyo, Ngalawa anaamini ujasiri huo ndiyo uli- omfanya hata mzee wake apunguze ghadhabu. Bakari Alexender Ngalawa kwa sasa anaishi mtaa wa Sultan area, Manispaa ya Morogoro na ana mke na watoto wawili.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close