1. TIF News2. Aliyeslimu

Aaron Petro na Jinsi Alivyohama Ukristo

Aaron Petro Show alizaliwa JanuarI 9, 1978 Mkoani Kilimanjaro katika Wilaya ya Hai Kijiji cha Kilanya, akiwa mtoto wa kwanza kati ya jumla ya watoto nane wa baba na mama mmoja. Aaron alipata elimu yake ya msingi huko huko, lakini hakubahatika kuendelea mbele kwa sababu ya migogoro ya kifamilia. Familia ya Aaron ilikuwa ni waumini wazuri wa Ukristo kutoka dhehebu la Lutheran. “Kiukweli, walikuwa na mpaka sasa wamebobea katika Ukristo, isipokuwa mimi peke yangu tu ndiyo nimesilimu,” Aaron alisema. Wakati wa utoto na kukua kwake, ilikuwa ni kawaida kwa Aaron kwenda kanisani, ambako alibatizwa na kusomea mafundisho ya Ukristo kwa miaka miwili hadi akapata kipaimara. Nilikutana na Aaron ambaye hivi sasa ni Muislamu hivi karibuni na kunipa mkasa wa maisha yake hadi kusilimu.

Kusilimu

Baada ya kuacha shule na miaka ikasonga, katika harakati zake za kutafuta ajira, alipopata kibarua cha kulima na kutafuta chakula cha mifugo kwa mzee mmoja Muislamu nje kidogo ya kijiji alichokuwa akiishi. Akiwa na umri wa miaka 19, Aaron alikuwa Mkristo pekee katika kibarua kile lakini anasema hakuwahi kutengwa. Wafanya kazi wengine walienda msikitini au madrasa na yeye Jumapili alipewa mapumziko na ruhusa ya kwenda kanisani. “Kiukweli alikuwa ni mzee mwenye roho nzuri sana, alikuwa ananilipia sadaka. Siku ya Ijumaa tulikuwa hatufanyi kazi yoyote, na ikitokea shughuli inayohusu watoto wa madrasa alikuwa ananiruhusu niende nyumbani na mshahara wangu uko pale pale. Ukweli namshukuru sana na kumuomba Mungu amsamehe makosa yake,” alisema Aaron. Ijumaa moja Aaron alienda shamba ambako ni karibu na msikiti akiwa amebaki peke yake huku wenzake wote wakiwa wameenda msikitini. Aaron hakukaa sana shambani kutokana na kuwa peke yake. Wakati akirudi akiwa amebeba mgomba alipita karibu na ule msikiti wakati mawaidha ya kabla ya Khutba ya Ijumaa yakiendelea na kuamua kupumzika kigodo nje ya uzio wa miti ya msikiti ule uliopo eneo la Mkwawanja. Akiwa amepumzika, akawa anasikiliza kile kinachosemwa. Anasema mada ilikuwa inahusu Mtume Isa bin Maryam. “Akiongea Kiarabu kisha akitfsiri Kiswahili, kwa yale machache niliyoyasikia kutoka Sheikh niliondoka nikiwa na kitu kipya cha kiimani kilichoniingia sawa sawa,” alisema Aaron. Alipofika nyumbani, Aaron alingia katika dimbwi la mawazo akitafakari mawaidha yale yaliyomvutia sana. Haikuisha wiki alirejea nyumbani kwao siku ya Jumamosi. Alipofika, aliitwa ofisini kwa mchungaji kujibu kesi kwa nini haonekani kanisani. Kwa msukumo wa mawaidha aliyoyasikia, Aaron alimgeuza kikao kile kuwa ni cha maswali kwa mchungaji wake, akianza kwa kumuhoji kuhusu picha ya Maria/ Mariamu: “Alionekana wapi hadi akapigwa picha na hatimaye zikasambaa ulimwenguni na kuwekwa makanisani?” Aaron anasema mchungaji wake alishindwa kujibu. Pia alimuuliza, kuhusu mavazi ya kuabudia: “Kanisani ni sehemu takatifu kwa nini sisi tunaingia na viatu lakini wenzetu (Waislamu) wanavua viatu wanapoingia msikitini kuswali?” Swali jingine likawa: “Wenzetu wana swala za vipindi kwa nini sisi tunaswali Jumapili tu?” Mchungani alijibu kwa kusema kuwa hilo linatokana na madhehebu tofauti. Mjadala uliendelea na Aaron akasema ikiwa binadamu wote tumeumbwa na Mungu mmoja na kitabu ni kimoja kwa nini tumekigawanya mara mbili, na kwa nini tusifuate lile agano la kale? Akaendelea kumuuliza: “Inakuwaje wewe tu mchungaji ndiyo unavaa kanzu”, Mchungaji akajibu kwa kusema: “Hilo ni vazi la Yesu Kristo,” Aaaron akamuuliza: “Ni kwa nini nasi waumini tusifuate mwendo wake na sisi tukavaa kanzu?” Aaron alisema Mchungaji wake hakuwa na majibu yenye mashiko. “Baada ya maswali mengi, mchungaji wangu akachukia na kuniambia kuwa mimi ni mpinga Kristo, lakini nikamwambia kuwa sijapinga ila ni maswali tu, ukweli nilishindwa kuendelea naye na kumuacha kwa sababu alikuwa amekasirika,” alisema Aaron Mvuto wa mawaidha ya msikitini na kukosa majawabu ya baadhi ya maswali aliyomuuliza Mchugaji wake, vikisindikizwa na tabia njema ya familia ya babu yake aliyemuajiri ambaye ni Muislamu, vilimsukuma Aaron kusilimu. Akarudi kazini kwa tajiri yake akamwita na kuzugumza naye kuwa anataka kusilimu. Baaada ya kuhojiwa kama anataka kusilimu kwa hiyari na hakuna aliyemlazimisha, mzee yule akamwita Ustadhi ambaye alimuuliza maswali muhimu ya kuhakikisha anasilimu kwa hiyari, kisha akasilimishwa na kuwa Muhamed.

Changamoto

Baada ya kusilimu, familia yake haikupendezewa hata kidogo. “Paliwaka moto kati yangu na wazazi, wakinambia kuwa kama sitorudi katika Ukristo kitachotokea kitakuwa ni mimi na dini yangu, wao wakijitoa kwa lolote linalohusu mimi,” alinambia Aaron. “Kutengwa kupo na potelea mbali na mwamuzi atakuwa ni Mungu,” ndiyo fikra ya Aaron baada ya kukutana na upinzani mkali kutoka kwa ndugu. Hata alipooa familia yake iligoma kumsaidia, na badala yake aliwatumia baba zake wakubwa ambao walimsaidia. Hata hivyo, Aaron anashukuru kuwa sasa anaishi vema na familia yake baada ya wazazi wake kumuelewa na kumkubali kama alivyo. Baada ya kusilimu alianza kusoma madrasa akikumbana na changamoto ya kutojua kusoma Kiarabu, lakini anajivunia kuwa taratibu na sharia, vibaya na vizuri na halali na haramu anavijua.

Maisha yake sasa

Aaron ni b a b a w a w a t o t o wawili na kwa sasa a n a i s h i Rundugani huko Kilimajaro akijishughuisha na kili

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close