3. Akisi Ya Aya

“Enyi Mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (Swaumu) . . .”

Assalam Alaykum wap- endwa wasomaji wa safu hii adhimu ya Akisi ya Aya. Kwanza niwa- take radhi kwa kushindwa kuwaletea safu hii wiki iliyopita kutokana na sababu zi- lizokuwa nje ya uwezo wangu. Lakini leo Insh’Allah tuakisi pamoja Aya hizo za Mwenyezi Mungu tuli- zozitaja kutoka Surat Baqara ambazo zinase- ma: “ Enyi Mlioamini! Mmelaz- imishwa kufunga (Swaumu) kama walivyolazimishwa wal- iokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu, “ (Qur’an, 2: 183) . Kufunga swaumu ni ibada yenye changamoto kidogo na inahitaji subira. Aya hiyo ya Mwenyezi Mungu inayoamri- sha kufunga imewekwa karibu na Aya kadhaa zinazohusu ugu- mu, changamoto na subira. Kabla ya Aya hiyo, Allah ‘Azza wa Jalla’ anasema: “ . . . na wanaovumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndiyo waliosadikisha (Uislamu wao) , na hao ndiyo wamchao Mungu” (Qur’an, 2: 177). Mwenyezi Mungu amesema mahali pengine: “ Enyi Mlio- amini! Mmepewa ruhusa ya kulipa kisasi katika waliouawa, “ Qur’an, (2: 178) . Allah Ali- yetukuka anaendelea zaidi: “ Mnalazimishwa – mmoja wenu anapofikwa na mauti, kama akiacha mali – afanye wasia kwa wazazi wake na jamaa zake kwa namna nzuri inayopendeza. Ni wajibu hAya kwa wamchao Mungu, “ (Qur’an, 2: 180) Aya zote hizo za Mwenyezi Mungu zina maamrisho am- bayo ni magumu na yanahitaji subira na kujipinda katika utekelezaji wake. Pia kuna Aya baada ya Aya zinazoamrisha ku- funga zinazohusiana na kupiga- na, jambo ambalo ni gumu na linahitaji subira. Allah Ali- yetukuka anasema: “ Na pigane- ni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui,” (Qur’an, 2: 190) Mwenyezi Mungu anasema tena: “ Na waueni popote mnapowakuta na watoeni po- pote walipokutoeni; kwani fiti- na ni mbAya zaidi kuliko ku- uwa. Wala msipigane nao

kwenye Msikiti Mtakatifu mpa- ka wakupigeni huko. Wakiku- pigeni huko basi nanyi pia wapi- geni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri, “ (Qur’an, 2: 191) . Mwenyezi Mungu anaende- lea kusema: “ Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiwepo uadui ila kwa wenye kudhulu- mu, “ (Qur’an, 2: 193) Kwa hiyo, kufunga na kupi- gana katika njia ya Mwenyezi Mungu kunahitaji subira na kuna Aya nyingi tu zinazohusi- sha mahitaji ya subira katika kupigana kwenye njia ya Mwenyezi Mungu. Kufunga pia ni jukumu gumu linalohitaji subira, na ndiyo maana Mtume rehema amani juu yake amese- ma: “ Kufunga ni nusu ya Subi- ra” (Tirmidhiy) . kuhusu amri ya kufunga bila ya kupitia kwa Mtume. Ameanza na tamko la “ Enyi Mlioamini” ili kusisitiza umuhimu wa ibada hii kongwe, ambayo hata waliopita kabla yetu waliamrishwa kuitekeleza. Kwa hiyo, ndugu zangu kati- ka Imani, kufunga ni jambo la wajibu na siyo rahisi, kwa kuwa kunahusisha kujizuia kula chakula, kunywa na kuacha vi- tendo vyote vinavyobatilisha Swaumu kutoka Alfajiri mpaka jua linapozama. Kufunga ni namna ya kupi- ma dhamira na uvumilivu wa Muumini na ni kipengele muhimu cha mahusiano kati ya binadamu na Mwenyezi Mun- gu. Ni nidhamu inayomfundis- ha binadamu jinsi ya kudhibiti matamanio yake na kuhimili mashinikizo ya vishawishi, ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu na malipo mema. mu watakayokabiliana nayo. Bila shaka kuna faida nyingi pia za kiafya, lakini lengo la ku- funga ni kubwa na pana zaidi kuliko faida za kiafya zinazopa- tikana. Lengo kuu la kufunga ni ku- muwezesha kwa kiasi cha kuto- sha binadamu kutekeleza kika- milifu nafasi yake hapa duniani na kujihakikishia mafanikio mema katika maisha yajayo. Ni jambo la wazi kabisa kwamba vitendo vyote vya ibada na maamrisho yaliyowekwa na Mwenyezi Mungu yanazingatia pia uwezo wa binadamu kuyat- ekeleza. Lakini hatupaswi kuhalali- sha vitendo hivyo vya ibada kwa kuzingatia ufahamu wetu peke yake au elimu zetu ndogo zina- vyotuonyesha. Upeo wa ufaha- mu wa binadamu unabaki kuwa na kikomo na hauwezi kujua kikamilifu hekima ya Mwenyezi Mungu nyuma ya ibada hizo. Binadamu anatakiwa afuate tu mfumo wa maisha ambao Mu- umba wake amemchagulia. Ndugu zangu katika Imani, ukiakisi kwa kina zaidi, utaona Aya zinazoamrisha kufunga, zimewekwa katikati ya Aya zi- nazohusu mambo magumu na yanayohitaji subira kuyafanya. Mwenyezi Mungu amewaam- bia moja kwa moja Waumini vishawishi, vikwazo na magu- Mtukufu wa Ramadhan. Amin. Katika kufunga, kuna vi- pengele muhimu sana vya nid- hamu na mafunzo kwa Wau- mini, ili waweze kubeba na kusambaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu, licha ya Mwenyezi Mungu azikubali swaumu zetu katika Mwezi huu

Show More

Related Articles

Back to top button
Close