3. Akisi Ya Aya

Allah – hapana Mola ila Yeye aliye hai, msimamia mambo yote milele..

Assalam Alaykum wap- endwa wasomaji wa safu hii adhimu ya Akisi ya Aya. Kwa mara ny- ingine tena, leo Insh’Allah tuakisi ‘Ayat- ul Kursi’ ambazo zinap- atikana katika Surat Baqara kuanzia Aya ya 155. Ndugu zangu kati- ka Imani, ‘Ayatul Kursi’ ni Aya nzito kweli kweli ndani ya Qur’an. Kuto- kana na uzito huo, tut- aziakisi moja moja ili wasomaji wapate kufa- hamu maana hasa ya Aya hizo.

“Allah – hapana Mola ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingi- zi wala kulala. Ni vyake peke yake vyote vilivyomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awe- zaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, wala wao hawajui chochote ka- tika vilivyo katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani, wala haemewi na ku- vilinda hivyo.Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu,” (Qur’an, 2:55). “Allah – hapana Mola ila Yeye Aliye hai” Muislamu anapo- soma sentensi hii kwenye ‘Ayat-ul Kursi’, maana yake anarudia kutamka ‘Shahada’. Tufahamu kwamba Shahada ina masharti saba ambayo lazima yatekelezwe ili mtu akubalike kuwa kweli ni Muislamu. Sharti la kwanza la Shahada ni Elimu, yaani maari- fa ya msingi kuhusu Shahada ina maana gani. Kuna watu wamezaliwa Waislamu, wanatamka Sha- hada kila siku, lakini bado ni washirikina, wanaamini miz- imu na kuomba kwenye maka- buri ya wahenga wao, masheikh wao au masharifu. Vipi Muisla- mu anatamka Shahada na ana- soma ‘Ayatul Kursi’ na kutanga- za kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayepaswa kuabudiwa kwa haki, lakini bado anafanya upuuzi kama huo? Ndugu zangu katika Imani, ukiakisi kwa kina zaidi sentensi hiyo ya kwanza kwenye ‘Ayatul Kursi’, utaona watu wanaofanya hivyo wameshabatilisha Sha- hada zao kwa sababu hakuna kisingizio cha kumuabudu Mungu asiyestahili kuabudiwa. Allah ‘Azza wa Jalla’ amesema atasamehe uhalifu wowote ule isipokuwa shirki. Anasema Mwenyezi Mungu: “Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu basi huyo amepotea upotevu wa mbali,” (Qur’an, 4:116). Kwa hiyo, wale wanaoitwa Waislamu, lakini bado wanam- shirikisha Mwenyezi Mungu, iliyobaki. kwa maana zote za shirki, basi wajue hawatekelezi, “Laa ilaha Illa lllah” (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah).Wanasoma tu tamko hilo kwa sababu za kiutamaduni, la- kini si sababu za uchamungu. Yeyote anayetamka Shahada lakini hajui maana ya kile ana- chotamka basi hajawa Muisla- mu, kwa sababu sharti la kwan- za la Shahada ni elimu kuhusu maana ya tamko hilo. Tuendelee kuakisi sentensi ya pili katika ‘Ayatul Kursi’ inay- osema: “Msimamia mambo yote milele.” Mwenyezi Mungu Mtukufu anajirejea kama ‘al Hayy’ katika sentensi hii, yaani Yeye Peke Yake ndiye atakaye- dumu milele. Kuna baadhi ya washirikina wa kisufi wanampa sifa hii Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie). Wanadai bado yuko hai ndani ya kaburi lake na anafahamu kikamilifu masuala yote yanayoendelea ya umma wake. Ndugu zangu katika Imani, safu ya Akisi ya Aya haina lengo la kufungua mjadala mpana kuhusu jambo hilo, isipokuwa tutazungumzia kidogo ili waso- maji wetu wafahamu mambo haya. Ifahamike kwamba ni ‘Ij- maa’ ya Maswahaba kwamba Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amefariki, na kwenda kinyume na ‘Ijmaa’ ya Maswahaba ni kosa. Ufahamu wetu wote wa dini tunachukua kutoka kwao.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close