3. Akisi Ya Aya

“Allah-hapana Mola ila Yeye aliye hai, Msimamia mambo yote milele…

Assalam Alaykum wap- endwa wasomaji wa safu hii adhimu ya Akisi ya Aya. Leo Insh’Allah tuendelee kuakisi ‘Ayat Kursi’ pale tulipoachia wiki iliyopita. Aya tunazoaki- si ni kutoka Surat Baqara kuanzia Aya ya 155.

Aya hizo zinasema: “Allah – hapa- na Mola ila Yeye aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na us- ingizi wala kulala.Ni vyake peke yake vyote vilivyomo mbinguni na dun- iani.Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake?Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, wala wao hawajui chochote katika vilivyo katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani, wala haemewi na kuvilinda hivyo.Na Yeye ndiye aliye juu, na ndi- ye Mkuu,” (Qur’an. 2:55).

Wakati Mtume Mohammad (re- hema na amani ya Allah zimshukie) alipofariki dunia, Seyyidna Umar (Al- lah amuwie radhi) alisema: “Nikimsi- kia yeyote anasema Muhammad amekufa nitamkata shingo yake kwa upanga.” Lakini Abubakr (Allah amridhie) alikwenda nyumbani kwa Mtume (rehema na amani ya Allah zimshuk- ie) na akambusu kwenye paji la uso na kuumbia umma uliokusanyika

pale: “Yeyote aliyekuwa akimuabudu Muhammad basi Muhammad amek- ufa, na yeyote anayemuabudu Allah, basi Allah yuko hai na hawezi kufa.”

Kisha Abubakr (Allah amuwie ra- dhi) akasoma Aya hii: “Kwa hakika wewe (Muhammad) utakufa, na wao (Maswahaba) watakufa” (Qur’an, 39:30). Sababu halisi ya kwa nini wa- shirikina wa Kisufi nchini India, Pa- kistan, Bangladesh, Uturuki nk, wa- naeneza itikadi kwamba Mtume (re- hema na amani ya Allah zimshukie), bado yuko hai kwenye kaburi lake ni kwa sababu wao ni waabudu maka- buri.

Wanaamini kabisa kwamba Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie) anaweza kujibu maombi yao kutokea kaburini. Itikadi hii mbovu na anafahamu kikamilifu ki- nachoendelea katika umma wake, ni kupindukia mipaka na inakwenda kinyume na Aqida halisi ya Kiislamu. Ni rahisi sana kufutilia mbali hoja potofu za washirikina hawa kwa saba- bu ni majahili kwa asilimia 100.

“Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala..”. Allah ‘Azza wa Jalla’ anatumia kauli hii kuthibitisha kwamba yeyote anayelala hawezi kuwa Mungu, kwani Mungu halali. Kama akilala, ulim- wengu wote utasimamama mara moja. Wakristo kwa sababu ya ujinga na kibri wanadai kwamba Yesu ni Mungu, ingawa Biblia inasema: “Yesu alilala na wakati aliolala alikuwa hatarini” (Luka 8:28)

Mungu anawezaje kulala? Nani anadhibiti ulimwengu wakati Mungu anapolala?! Isitoshe, Mungu anawe- zaje kuwa hatarini kutokana na vi- umbe wake mwenyewe?! Yeyote aliye hatarini hawezi kuwa Mungu. Haki- ka ‘Ayat Kursi’ inatumika kufutilia mbali uungu wa Yesu ambao ni itika- di ya kipagani ya Wakristo. Allah ‘Azza wa Jall’ awaongoze wale waadil- ifu miongoni mwao kwenye tawhid halisi. “Ni vyake peke yake vyote vilivyomo mbinguni na duniani..” Sentensi hiyo katika Aya inabainisha kwamba Mwenyezi Mungu ni ‘al Ghani’ (tajiri) wakati sisi ni ‘fuqaraa’ (masikini). Mvua ni ya Mwenyezi Mungu na bila ya mvua watu watapa- ta ukame na baa la njaa.

Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Katika siku za mwisho, watu watakuwa waovu na kugoma kutoa Zaka, ambayo ni ngu- zo ya Uislamu. Isingekuwa kwa ajili ya wanyama, Allah asingeleta mvua.”

Allah ‘Azza wa Jalla’ anamiliki vyo- te vilivyomo ardhini, na sisi ni watu- mishi wake. Kwa hiyo, wake zetu ni mali ya Mwenyezi Mungu na siyo mali zetu tunazomiliki kama tunavy- omiliki magari na nyumba. Wake zetu ni amana. Ni dhamana tuliy- opewa kuitunza ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu. Mwanaume yeyo- te anayeshindwa kusimamia dhama- na hii, hastahili kuwa na mke.

Mwenyezi Mungu pia anamiliki wanyama na wakati fulani anawatu- mia kama majeshi Yake kuwaadhibu makafiri .Katika Surah al-Fil Allah ‘Azza wa Jalla’ aliwatumia ndege kumsambaratisha Abraha na jeshi lake. Hawa walikuja kutoka Yemen mwaka aliozaliwa Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) kwa lengo la kubomoa Ka’aba, nyumba ya Mwenyezi Mungu.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close