3. Akisi Ya Aya

Aina za maumivu ya tumbo na maana zake

Maumivu ni moja kati ya dalili muhimu sana inayoashiria tatizo ndani ya mwili. Kwa kawaida, maumivu hutengenezwa na mfumo wa fahamu wa mwili kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuungua, kuchanika, kujigonga au uwepo wa ugonjwa. Katika makala hii, tutajadili aina za maumivu ambayo hutokea katika maeneo mbalimbali ya tumbo na maana zake.

Aina za maumivu

Kwa upandecwa maumivu ya tumbo, yenyewe huja kwa namna tofauti na ambazo huashiria ni kiungo gani cha tumbo kinachotengeneza maumivu haya. Mfano wa namna za maumivu haya ni pamoja na maumivu ya kuvuta, maumivu ya kuwaka moto na maumivu ya kufukuta.

Ndugu msomaji, elewa kuwa, maumivu yote haya huweza kuanza ghafla au taratibu na pia yanaweza kuwa maumivu ya kuja na kuondoka kutegemea na chanzo.

Maeneo ya tumbo

Kitaalamu, tumbo limegawanyika katika maeneo makuu tisa ambayo ni eneo la kitovuni (umbilical area), eneo la juu ya kitovu (epigastric area), maeneo ya kushoto na kulia ya eneo la juu ya kitovu (hypochondriac regions), maeneo ya kushoto na kulia mwa kitovu (lumbar areas), eneo la chini ya kitovu (suprapubic area) pamoja na maeneo ya kushoto na kulia mwa eneo la chini ya kitovu (iliac fossae).

Maumivu ya eneo la juu ya kitovu

Kama tulivyoona ya kuwa eneo hili hujulikana kama ‘epigastric’ yaani juu ya tumbo. Maumivu ya eneo hili huweza kutokana na magonjwa mbalimbali ambayo ni pamoja na ugonjwa wa kiungulia, vidonda vya tumbo, ngiri ya tumbo na pia ugonjwa wa homa ya ini.

Maumivu ya eneo la kushoto ya eneo la juu ya kitovu

Eneo hili hujulikana kama ‘left hpochondrium’ na hutengeneza maumivu ikiwa viungo vinavyopatikana katika eneo hili vitapata maradhi. Maumivu haya hutokana na maradhi katika kongosho au maradhi ya kuvimba kwa kuta za tumbo. Pia maumivu ya eneo hili yanaweza kutokana na mmeng’enyo wa chakula usio mzuri (functional dyspepsia).

Maumivu ya eneo la kulia ya eneo la juu ya kitovu

Kwa lugha ya kidaktari eneo hili hujulikana kama ‘right hypochondium’ na ndipo maini na mfuko wa nyongo huanzia. Kwa maana hiyo, ugonjwa wa maini na mfuko wa nyongo huweza kutengeneza maumivu katika eneo hili. Pia maumivu haya yanaweza kusababishwa na kujaa mawe katika nyongo. Pia, muda mwingine maumivu ya vidonda vya tumbo huweza kutawanyika na kufika katika eneo hili.

Maumivu ya eneo la kitovu

Jina jingine la eneo hili hujulikana kama ‘umbilical area’. Maumivu ya eneo hili mara nyingi husababishwa na magonjwa kama vile vidonda vya tumbo, maambukizi katika utumbo, maambukizi ya kongosho, ugonjwa wa kidole-tumbo (appendicitis) na pia ngiri ya kitovu.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close