10. Ramadhan

Faida ya funga ya Ramadhan kitiba

(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hesabu katika siku nyengine. Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakayefanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua.” [Quran 2:184].

baada ya siku kadhaa za funga ya Ramadhan, homoni kadhaa za mwili kama vile endorphins huanza kuongezeka ndani ya damu na hivyo kuimarisha afya ya akili.

Kuhusu hitimisho la Aya hiyo, Sayyid Qutb [Rejea, tafsiri yake: ‘Fii dhwilaalil-Qur’an] amesema: “Pamoja na kutoa elimu na mafunzo ya utayari utakaowafanya Waislamu kufanya juhudi ya kufunga Ramadhan, pia inatubainishia kwa uwazi kabisa kuwa funga hii ya Ramadhan ina faida kubwa kiafya/kitiba.”

Kujadili faida za kiafya za funga, hususan hii ya Ramadhan tunayoendelea nayo hivi sasa, ndilo hasa kusudio la makala hii.

Kifiziolojia, mwili huishiwa glukosi masaa takribani nane au zaidi baada ya mlo wa mwisho. Glukosi ni sukari ya mwisho inayopatikana baada ya mmeng’enyo wa vyakula vya kabohaidreti. Sukari hii ndiyo inayotegemewa na mwili kuzalisha nishati.

Glukosi ya mwili ambayo huhifadhiwa kwenye maini na misuli, kama nilivyodokeza, ndiyo chanzo kikuu cha nguvu/nishati ya mwili. Baadae, wakati wa funga, hazina ya glukosi ikiwa imeisha, mafuta hugeuka kuwa chanzo mbadala cha pili cha nguvu/nishati ya mwili.

Ni wakati mwili umekosa chakula kwa siku nyingi, mpaka wiki mathalan, ndiyo mwili huigeukia protini kwa ajili ya kuzalisha nishati. Muda huu, glukosi na mafuta huwa tayari vimeisha. Hii ndiyo huitwa janga la njaa, na kamwe siyo hali salama kabisa kwa afya ya mwili.

Kwa kuwa, funga ya Ramadhan huanzia unapobainika weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku (saa 12 Alfajiri) – kama ilivyobainishwa kupitia Qur’an [2:187] mpaka Jua linapozama (saa 12 jioni); basi unapofika muda wa kufuturu, mwili hupata nafasi ya kufidia hiyo glukosi na mafuta yaliyotumika wakati mwili ulipoishiwa kuwa glukosi (kuanzia saa 7-12).

Hii hutoa nafasi kwa mwili kuhama taratibu kutoka kwenye kutumia glukosi kama chanzo kikuu cha nguvu/nishati, kwenda kwenye kutumia mafuta kama chanzo mbadala cha pili cha nguvu/nishati; na hivyo kuuzuia mwili kufika kwenye uvunjwaji wa protini (chanzo mbadala cha tatu cha nishati ya mwili). Uvunjaji wa protini ungepelekea kutokea janga la njaa.

Matumizi/uvunjwaji wa mafuta kama chanzo mbadala cha pili cha kuzalisha nguvu/nishati una faida kadhaa, ikiwemo kupunguza uzito wa mwili, kuilinda misuli na kupunguza sumu mwilini ambazo huhifandhiwa kwenye mafuta. Kadhalika, baada ya siku 29/30 za funga ya Ramadhan, hata lehemu (cholesterol) ya mwili huwa imepungua.

Kwa nyongeza, kupungua kwa uzito hupelekea usimamizi mzuri wa kiwango cha sukari ya mwili (hususan kwa wenye kisukari). Kuongezeka kwa uzito humfanya mtu awe kwenye hatari ya kuugua kisukari cha aina ya pili (type 2 diabetes) ambacho hutokana na kupotea kwa uwezo wa kawaida wa tishu (seli) za mwili kuchukua homoni ya insulini inayosimamia kiwango cha sukari mwilini, au ukinzani wa insulini. Vile vile, kupungua kwa uzito hupelekea kupungua kwa shinikizo la damu.

Katika faida zaidi, baada ya siku kadhaa za funga ya Ramadhan, homoni kadhaa za mwili kama vile endorphins huanza kuongezeka ndani ya damu na hivyo kuimarisha afya ya akili. Matokeo yake,
Muislamu hupata amani ya moyo, utulivu, furaha, upendo, kujali/kuthamini n.k

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close