JUNAYNAT ALLY DAMA
IWAPO UCHAGUZI UNGEFANYIKA LEO, Utafiti mpya wa Baraza la Mahusiano kati ya Marekani na Uislamu (CAIR) unaonesha kuwa asilimia 29.4 ya Waislamu wa Marekani wamepanga kumchagua mgombea wa urais wa chama cha Democrats, Kamala Harris.
Katika utafiti huo, Trump wa chama cha Republican, mpinzani wa karibu wa Harris, anashika nafasi ya tatu kwa kuungwa mkono na wapiga kura Waislamu akipata asilimia 11.2 pekee.
Mgombea wa chama cha Kijani (Gree Party), Jill Stein, anaelekea kupata ungwaji mkono miongoni mwa Waislamu kwa asilimia 29.1%.
Kuelekea uchaguzi wa urais wa Novemba, asilimia ya uungwaji mkono kwa Harris kutoka kwa Waislamu inafufua matumaini ya Democrats ukizingatia kuwa mgombea wao wa awali, Rais Joe Biden alikuwa na uungwa mkono wa asilimia 7.3 pekee. Biden alijiengua kufuatia shinikizo la viongozi na wanachama wa Democrats waliokuwa na wasiwasi na afya yake.
Waislamu hawakumpenda Biden kwa sababu ya sera zake za kuitetea Israel katika mauaji ya kimbari inayoyatekeleza huko Gaza na Palestine kwa ujumla.
Matokeo ya utafiti huu yanaonesha namna Waislamu walivyogawanyika kutokana na kukosekana mgombea ambaye wazi anaonekana kusaidia ajenda zao, na hivyo kuonekana kama wanabahatisha au kuchagua mwenye nafuu.
Utafiti wa CAIR uliofanyika Agosti 25 hadi 27 ukihusisha sampuli ya Waislamu 1000 pia ulionesha asilimia 69.1% ya Waislamu kwa kawaida huchagua chama cha Democrats, lakini kwa sasa asilimia 59.7% wanapanga kuchagua vyama vingine katika uchaguzi wa mwaka huu.
Pia asilimia 94 hawakuafiki sera za Biden na Bunge la Congress, huku asilimia 98.2 wakichukizwa na mwenendo wao kuhusu Gaza.
Wakati asilimia 16.5 ya Waislamu wakionekana bado kuamua nani watampa kura, utafiti pia umeonesha kuwa masuala muhimu kwao haki za binadamu kimataifa, uhuru wa kuabudu, hduma za afya na uhalifu wa chuki. Kimataifa, suala la Palestina na Xinjiang yamepewa kipaumbele zaidi.
Hata hivyo, licha ya kutoridhishwa na sera za nchi hiyo kimataifa, utafiti unazidi kuonesha kuwa bado Waislamu wengi wanajihusisha na siasa huku asilimia 82.1 wakisema kuna uwezekano mkubwa wao wao kupiga kura.
Chanzo: 5pillars
I do agree with all the ideas you have introduced on your post They are very convincing and will definitely work Still the posts are very short for newbies May just you please prolong them a little from subsequent time Thank you for the post