-

WHO yakubaliana na Uislamu ubaya wa pombe

Hakuna ‘kunywa kistaarabu’ Hata glasi moja ina madhara!

Ripoti mpya inayozungumzia madhara ya pombe iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Afya Duniani (WHO), inaonesha kuwa zaidi ya vifo milioni tatu duniani kote vinatokana na matumizi ya pombe. Vifo hivyo ni sawa na kifo kimoja kati ya kila 20 vinavyotokea duniani kote. Taarifa hiyo ya WHO iitwayo, ‘Ripoti ya mwaka 2018 ya Hali ya Dunia ya Pombe na Afya,’ pia inaonesha kuwa idadi hiyo ya watu wanaokufa kwa kutokana na pombe ni kubwa kuliko vifo vinavyotokana na UKIMWI, ukatili na ajali kwa pamoja, huku wanaume wakiwa ndio wahanga wakubwa.

Wakati taarifa hiyo ikitoka, Qur’an ilishakataza pombe karne 14 zilizopita pale Allah aliposema: “Enyi mlioamini! Hakika si vinginevyo ulevi, kamari, kuabudu masanamu na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet’ani. Basi jiepusheni navyo ili mpate kufanikiwa.” (Qur’an 5:90)

Taarifa hiyo pia inasema, asilimia tano ya maradhi yote duniani inasababishwa na kinywaji hicho kilichoharamishwa katika Uislamu. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO amesema: “Watu wengi, familia zao na jamii wanaathirika na pombe kupitia ukatili, majeraha, matatizo ya akili, na maradhi kama kansa na kiharusi,” na kuongeza kuwa huu ni muda muafaka wa kuchukua hatua kuzuia tishio hilo dhidi ya afya ya jamii.

‘Vifo vyote vinavyotokana na pombe, asilimia 28 inatokana na majeraha yanayotokana na ajali za magari na kupigana, 21% yanatokana na matatizo ya mmeng’enyo wa chakula na 19% vinatokana na maradhi ya moyo huku mengine yakitokana na maradhi ya kuambukiza, kansa, maradhi ya akili na mengineyo. Kiulimwengu mzima, inakadiriwa wanaume milioni 237 and wanawake 46 wameathirika kutokana na matumizi ya pombe huku nchi tajiri zikiwa ndio zilizoathirika zaidi. Watu bilioni 2.3 duniani kote kwa sasa ni wanywaji. Pia inatajwa kuwa, zaidi ya nusu ya watu wote katika mabara ya Ulaya na Amerika ni wanywaji.

Hakuna kiasi salama

Wakati WHO ikitoa taarifa hiyo, kuna habari mbaya kwa wale wanaodai kuwa kunywa kiasi kidogo cha pombe au kunywa kistaarabu ni jambo zuri kwa afya kwani matokeo ya utafiti ambayo nayo yalitolewa hivi karibuni yanaonesha kuwa hakuna ‘kiasi’ cha pombe ambacho ni salama. Kuonesha ukweli wa Uislamu, karne 14 zilizopita Mtume Muhammad (rehema za Allah na amani zimshukie) amesema “Kinacholevya kwa wingi wake, hata kwa uchache wake ni haramu.” (Ibn Majah).

Wakati taarifa hiyo ikitoka, Qur’an ilishakataza pombe karne 14 zilizopita pale Allah aliposema: “Enyi mlioamini! Hakika si vinginevyo ulevi, kamari, kuabudu masanamu na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet’ani.

Kwa mujibu wa watafiti, matokeo ya ule utafiti wa kwanza ulioonesha kuwa unywaji kidogo hulinda moyo umepingwa vikali na matokeo ya utafiti mpya unoonesha kuna hatari kubwa zaidi ya kunywa hata kiasi kidogo kwani mnywaji anawekwa katika hatari ya kupata maradhi ya kansa na maradhi mengine.

Utafiti huo ulioitwa, ‘The Global Burden of Disease study’, kwa tafsiri isiyo rasmi Utafiti wa Mzigo wa Ugonjwa Ulimwenguni” ulitafiti viwango na athari za matumizi ya pombe katika nchi 195, ikiwemo Uingereza kati ya mwaka 1990 na 2016. Matokeo ya utafiti yalionesha kuwa kati ya watu 100,000 wasiokunywa, 914 waliathirika kwa kupata maradhi yatokanayo na pombe. Hata hivyo, kwa watu 100,000 wanaokunywa chupa moja tu kwa siku, watu wanne zaidi (yaani 914 + 4), waliathirika na maradhi hayo.

Hii ina maana hakuna kiasi salama cha unywaji. Utafiti unaonesha pia kuwa, kwa watu 100,000 wanywao chupa mbili kwa siku, 63 zaidi (yaani 914 + 63), waliathirika; na kwa wanaokunywa chupa tano watu 338 zaidi (yaani 914 + 338) waliathirika! Mmoja wa watafiti, Prof Sonia Saxena kutoka Chuo cha Imperial College London alisema: “Ingawa ongezeko la hatari kwa wanywaji chupa moja ni dogo, ukizingatia idadi ya Waingereza wote namba ni kubwa! Na ukweli ni kuwa wengi hunywa zaidi ya chupa moja.”

Kuonesha ubaya wa pombe, hivi karibuni Jaji mmoja huko Marekani, Bret Cavanaugh, aliyeteuliwa na Rais Donald Trump kuwa jaji wa mahakama ya juu kabisa (Supreme Court),  imeingia kashfani na kuingia katika hatari ya kukosa nafasi hiyo baada ya kutuhumiwa kumnyanyasa mwanamke kutokana na kulewa pombe, jambo linaloonesha kuwa pombe ina madhara mengi ya kijamii.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close