-

Waislamu Wahimizwa Kuunga Undugu

Waislamu nchini wamehimizwa kuunga undugu ili kupata rehema za Mwenyezi Mungu na kuridhiwa katika maisha yao hapa duniani na kesho akhera. Nasaha hizo zimetolewa na Sheikh Suwedi Shemlugu alipokuwa akizungumza na Waislamu wa kijiji cha Mambo, kata ya Sunga, tarafa ya Mtae katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga walipokutana kwa ajili ya dua maalum ya kuombea amani ya Kijiji chao.

Sheikh Suwedi aliyataja baadhi ya mambo yanayopelekea kuunga undugu kuwa ni kuwajali na kuwatendea wema ndugu na jamaa wa karibu na wa mbali, kuwasiliana mara kwa mara kupitia njia ya simu na nyinginezo sanjari na kujenga utamaduni wa kutembeleana. “Amepata hasara na amelaaniwa yule mwenye kuukata udugu, tahadharini msije mkaukata undungu. Na yeyote atakayekuwa sababu ya kuukata undugu na asimjali nduguye atambue Allah atamkataa Siku ya Kiyama,” alisema Sheikh Suwedi.

Sheikh Suwedi alisema, kukata undugu ni kuvunja mkataba na maagano aliyoyachukua mja kwa Mola wake ya kwamba, hatamshirikisha na chochote na wala hatakata undugu.

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close