-

Waislamu Tuwe na Subira Katika Nyakati Ngumu: Faris

NA MRISHO TOZO DAR ES SALAAM

Muelimishaji wa Kimataifa wa Kiislamu, Mohammed Faris akitoa mada katika mhadhara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Muelimishaji wa Kimataifa wa Kiislamu, Mohammed Faris, maarufu Abuu Productive amewataka Waislamu nchini kuwa na subra katika mambo mbalimbali yanayowafika. Muelimishaji huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Productive Muslim aliyasema hayo katika warsha ya siku mbili iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kuhudhuriwa na waumini wa dini ya Kiislamu. Faris alisema kuwa hakuna jambo rahisi katika maisha ya mwanadamu hivyo ni vyema Waislamu wakawa na subra pindi wanapoomba dua kwa Allah na dua hizo zinapochelewa kujibiwa. “Inajulika na kila mmoja dua ni silaha kubwa ya mwanadamu lakini kwa sasa watu wamekuwa wakitaka maombi yao yajibiwe kwa haraka sana jambo ambalo ni gumu, hivyo ni muhimu kwa kila mmoja kujibiidiisha katika mambo mbalimbali na kisha kufanya dua huku wakiwa na subra Hivi ndivyo walivyofanya wema waliotangulia,” alisema Faris. Pia muelimishaji huyo alisema kuwa watu wema waliotangulia walikuwa na subra, tofauti na watu wa hivi sasa ambao wamekuwa wakitaka mambo kwa pupa. Aidha, Faris aliongeza kuwa Waislamu wanapaswa kupangilia muda wao vizuri kwa kufanya mambo ya kheri kwa kuwa kila mwanadamu atakuja kuulizwa na Allah ni kwa namna gani ametumia muda wake hapa duniani. Waliohudhuria mafunzo hayo wamesema kuwa ni muhimu kwa umma wa Kiislamu kuzingatia yaliyotolewa kwa sababu yatawawezesha kuandaa akhera yao kwa kupangilia mambo kwa wakati. Mmoja wa mshiriki Ally Suleiman alisema amejifunza kupangilia muda wake na na namna ya kuitumia dunia kama chumo la akhera yake.

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close