-

Waathirika Maafa Pemba Wapokea Misaada

Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) imekabidhi jumla ya tani 22.5 za chakula kwa waathirika wa mafuriko katika kisiwa cha Pemba ili kuwapunguzia makali ya maisha waathirika hao. TIF ilikabidhi misaada hiyo iliyokusan- ywa kutoka kwa wadau mbalimbali, kwa waathirika katika mikoa miwili ya Kaska- zini Pemba na Kusini Pemba, huku wilaya zilizofaidika zikiwa ni pamoja na Mkoani, Chakechake, Wete, Micheweni. Misaada hiyo ilikabidhiwa kwa wakuu wa mikoa ya Kaskazini Pemba na Kusini Pemba. Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdallah alikabidhiwa tani 12.5 kutokana na mkoa wake kuathiri- ka zaidi na mwenzake wa mkoa wa Kaska- zini Pemba, Omary Khamis Othman, alik- abidhiwa tani 10. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Mipango wa TIF, Mussa Buluki, alisema hiyo ni awamu ya kwanza ya msaada na kwamba zaidi ya shilingi milioni 65 zilitumika katika kupe- leka msaada huo kwa waathirika wa mvua Pemba. Buluki aliongeza kuwa msaada uliope- lekwanipamojanamicheletani18, maha- rage tani 4.5, na kwamba katika ugawaji huo, kila mwathirika alipatiwa kilo 40 za michele na kilo 10 za maharage. Aidha, Buluki alisema kuwa kutokana na Wilaya ya Mkoani iliyopo mkoa wa Kusini Pemba kuathirika zaidi, jumla ya kaya 150 zimepatiwa msaada huo katika wilaya hiyo huku kaya 100 zikifaidika kati- ka wilaya ya Chakechake. Kaya 100 katika wilaya za Wete na ny- ingine 100 katika Wilaya ya Micheweni ka- tika mkoa wake Kaskazini Pemba zilipata misaada hiyo na kufanya jumla ya kaya zili- zofaidika Pemba nzima – wilaya zote nne na mikoa miwili iliyopokea misaada hiyo – kuwa 450. Mkurugenzi huyo wa Mipang alisema katika awamu ya pili ya msaada huo, kaya zitakazopewa kipaumbele ni zile ambazo hazijapata katika awamu ya kwanza. Akizungumza katika makabidhiano ya msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Wete, Al Haji Rashid Hadid, ali- ishukuru TIF kwa kuweza kuwakimbilia watu wenye mahitaji na kusisitiza kuwa msaada huo umefika wakati muafaka ambapo utawapunguzia makali ya maisha waathirika wa mafuriko ya mvua. Naye Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Al Haji Abeid Juma Ali, alisema TIF inapaswa kuigwa kutokana na huruma yake na kuguswa na maafa ya KisiwachaPembanakuamuakukusanyamichango kutoka kwa wahisani wa ndani ili kuwasaidia waathirika. “Sijawahi kuona taasisi yenye mapenzi ya dhati kama TIF. Wanawakimbilia watu wenye mahitaji. Suleiman Abdallah, ambaye wilaya yake imeathiri- Tumeona walivyowasaidia watu Kagera na sasa wametukimbilia sisi yatupasa kuishukuru,” alisema Abeid Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Bi. Salama Mbaruku Abdallah, alise- ma kuwa kutokana na watu kupoteza mali pamoja na chakula msaada wa TIF ulifika wakati muafaka na kwamba anashukuru taasisi hiyo imechukua jitihada kubwa ya kuwasaidia waathirika wa mvua Pemba. ka zaidi, ameiomba TIF kuwajengea wananchi misikiti na madrasa vilivyobomoka ili jamii ya kiis- lamu ipate sehemu ya kuswalia pamoja na kujifun- za elimu ya dini. Licha ya makazi ya watu, misikiti na madrasa; maafa hayo pia yaliharibu miun- dombinu ya barabara. Licha ya ombi hilo, Mkuu huyo wa wilaya wa Mkoani, aliitaka jamii kuzidi kuiunga mkono TIF kwa kuwa imejitoa katika kuwasaidia watu wenye mahitaji, na kusisitiza kuwa vyakula hivyo vimekuja wakati muafaka katika mwezi huu wa Ramadhani. Mwanajuma Majid Abdallah, aliliambia Gazeti Imaan kuwa TIF inafanya shughuli zake kwa muji- bu wa dini ya Kiislamu inavyotaka hivyo ameiasa jamii kuiga mfano wa taasisi hiyo ambayo inasaidia watu mbalimbali bila ubaguzi. Nao waathirika wa maafa hayo ya mvua waliopokea misaada wali- ishukuru TIF kwa kuwajali katika kipindi kigumu walichokuwa nacho. Kumalizika kwa awamu ya kwanza ndiyo kunatoa nafasi ya awamu ya pili ya kupeleka msaada kwa waathirika wa mvua kisiwani Pemba ambapo zaidi ya Milioni 55 zinatarajiwa ku- Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Hemed Naye Mkuu wa Mkoa wake Kusini Pemba, tumika.

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close