-

VPN yaja na mkakati kuendeleza vipaji vya watoto wa kiislamu

Ili kufanikisha malengo ya wato- to wenye vipaji, wazazi nchini wamehimizwa kuwalea vijana wao katika nidhamu ya kumtam- bua Allah kwani kufanya hivyo ndiyo njia ya kukuza na kuhuisha vipaji vyao. Dkt. Hassan Mshinda, Mkuru- genzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia amebaini- sha hayo wakati wa hafla ya futari na kuwachangia wanafunzi wenye vipaji iliyoandaliwa na Mtandao wa Kuendeleza Vipaji (VPN) na kufanyika kwenye Ukumbi wa Masjid Istiqama uliopo manispaa ya Ilala jijini Dar Es Salaam. Dkt. Mshinda alisema, taifa lina vijana wengi wa Kiislamu wenye vipaji na uwezo mkubwa lakini wamekosa malezi ya ku- wawezesha kufikia malengo yao kwa sababu ya kuishi kwenye mazingira yasiyo rafiki. Mkurugenzi huyo aliitaja changamoto ya kukosekana kwa maadili ya dini kwa baadhi ya wa- zazi na walezi kama kikwazo dhidi ya maendeleo ya watoto wenye vi- paji na hivyo kusababisha wakose muelekeo. Aidha, Mshinda alibainisha kuwa, fani nyingi katika ulimwen- gu wa sasa zikiwemo za utafiti, udaktari, uhandisi na uhadhiri ka- tika vyuo vikuu zinahitaji vijana wenye vipaji, hivyo taasisi na mtu mmoja mmoja wanapaswa ku- saidia ufadhili kwa watoto wenye vipaji. “Hii itakuwa fursa nzuri ya mimi kupata nafasi ya ‘kuta- baruku’ katika shughuli nzuri mnayoifanya kwani moja ya kazi yangu ni kuendeleza vipaji vya wabunifu, na kwa sababu mmen- iomba niwe balozi wenu naahidi kulifikisha suala hili kwa wadau ili tuweze kufanya kazi vizuri na kwa pamoja,” alisema, Dkt. Mshinda. Naye mtoa mada katika hafla hiyo, Sheikh Yusuf Kidago ali- wasihi wazazi, walimu na wasi- mamizi wa vituo vya kukuza vipaji vya watoto kuwapa malezi mema sambamba na kuwaonya wasimuasi Allah kwa kuwa kufan- ya hivyo kutapelekea vipaji vyao kupotea. Sheikh Kidago alisema, msingi mkubwa wa kumpata mtoto mwenye kipaji ni mzazi kuwa na ukaribu wa kimalezi na mtoto wake hivyo jitihada zinahi- tajika ili kuwalea watoto katika misingi ya dini. Akitoa taarifa ya utendaji kazi, Meneja mradi wa VPN Haji Mrisho, alisema wazo la kuanzish- wa mradi huo lilitokana na kuwe- po vijana wanaohitimu masomo na kufaulu vizuri lakini wakabaki kutangatanga mitaani kwa sababu ya kukosa uwezo wa kujiendeleza. Aidha Mrisho alisema: “Tunaz- ingatia kuwaandaa watoto kiima- ni, kiutendaji, kimafunzo na ma- husiano mema ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila kijana wa Kitanzania anapata elimu bila kujali hali ya kiuchumi ya familia anayotoka. “VPN ni kama daraja la kuwaunganisha wale wote wanaohi- taji kuwasaidia watoto wanaohi- taji msaada na hadi sasa tumefan- ikiwa kuwawezesha wanafunzi 47 wa kidato cha kwanza hadi cha nne na tatu wa shule za msingi kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora na Dar es Salaam,” aliongeza Mrisho. Kuhusiana na malengo ya baa- dae ya VPN Mrisho alisema, kati- ka mwaka 2017/2018 wamepanga kufadhili wanafunzi 100, kati ya hao 70 ni wa kidato cha kwanza hadi nne huku 30 wakitoka kidato cha tano na sita. Hata hivyo Mrisho alikiri kuwepo kwa idadi ya kubwa ya watoto wanaohitaji msaada ukilinganisha na uwezo mdogo wa mfuko. Vipaji Promotion Netwok (VPN) ni mtandao ulioanzishwa mwaka 2015 ukiwa na wajumbe 40 kwa lengo la kuwasaidia wa- nafunzi wa Kiislamu wenye vipaji lakini wana changamoto ya kupa- ta mahitaji yao ya kielimu.

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close