-1. Habari1. TIF News

Tif yawajengea msikiti mpya waliosali banda la nyasi miaka 7

Waumini wa dini ya Kiislamu katika kijiji cha Bituntu, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, wameishukuru taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) kwa kuwajengea msikiti mpya unaowawezesha kufanya ibada zao katika hali tulivu.

Wakielezea furaha yao wakati wa hafla ya kukabidhi msikiti huo, Waumini hao wamesema sasa wameondokana na adha ya kuswali katika msikiti ulioezekwa kwa nyasi na unaovuja wakati wa mvua.

Adha, nyingine ilikuwa ni paa la msikiti huo kuezuliwa pale upepo mkali unapovuma, ila kwa sasa wanasema mambo yamekaa vizuri na wanawashukuru viongozi wa TIF kwa msaada huo. Kwa upande wake Mkurugenzi wa TIF, mkoani Kagera, Sheikh Hamdani Kagaruki amewataka Waislamu kuutumia msikiti huo kwa ajili ya ibada, na sio kwa mambo mengine.

Niwaombe ndugu zangu Waislamu msikiti huu usiwe wakufungwa bali utumike kwa ajili ya ibada na sio mambo mengine yanayokwenda kinyume na mafundisho ya Mola wetu,” alisema Sheikh Kagaruki.

Sheikh Kagaruki aliongeza kuwa TIF inaendelea kujenga msikiti mingi na huduma zingine ndani ya mkoa huo ili kuhakikisha Waislamu na jamii kwa ujumla inapata huduma mbalimbali.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close