-1. Habari1. TIF News

TIF Yatoa Matibabu Bure kwa Wagonjwa 2,600

TAASISI ya The Islamic Foun- dation (TIF) imefanikiwa ku-toa matibabu bure ya maradhi mbalimbali kwa zaidi ya wagonjwa 2,600 wilayani Sengerema, mkoa- ni Mwanza.

Naibu Mkurugenzi wa taasisi hiyo mkoani Mwanza, Mbaraka Saidi, amekiambia kipindi cha ‘Sayari ya Imaan’ kinachorushwa na Televisheni ya Imaan kuwa kambi hiyo ilidumu kwa siku mbili na kufanyika katika Shule ya Se- kondari ya Sengerema Islamic.

Mbaraka aliongeza kuwa TIF iliandaa matibabu hayo ili kuone- sha jamii kuwa Dini Tukufu ya Ki- islamu ni nzuri, inahimiza ukar- imu na kusaidia wanyonge; kiny- ume na maadui wanavyopotosha.

Katika kambi hiyo ya matibabu, Watanzania wanaoamini katika itikadi za dini tofauti walijitokeza kutibiwa bure na bila ubaguzi wowote.

Akizungumzia kuhusu mikaka- ti ya kupeleka huduma zaidi za afya vijijini, Mbaraka alisema wam- emuomba Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahdi, kuwapatia gari maalu- mu kwa ajili hiyo.

Alibainisha kuwa gari hilo am- balo litakuwa na vifaa vya tiba lita- zunguka vijijini na kutoa huduma za afya kwenye maeneo yenye changamoto kubwa za matibabu.

Naye Mkurugenzi wa TIF, mko- ani Mwanza, Abdulhakim Abeid alisema kuwa pamekuwa na mui- tikio mkubwa katika matibabu hayo na kumpongeza Mwenyekiti Nahdi kwa kusaidia jamii ya mkoa huo.

Naye msimamizi wa madaktari katika kambi hiyo ya matibabu ya bure, Dkt Ahmed Mohammed amesema kuwa muitikio wa watu ulikuwa mkubwa ingawa baadhi ya wagonjwa wamekuwa wagumu kutumia dawa.

Dkt Ahmed aliishauri jamii ku- jenga tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kuweza kupata tiba mapema badala ya kusubiri hadi waumwe. Madaktari wengine walioshiriki katika kampeni hiyo walitoka katika hospitali mbalim- bali za mkoa huo, ikiwemo Bugan- do na CF.

Nao, baadhi ya viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wilaya ya Sengerema walielezea kufurahishwa kwao na msaada huo wa TIF.

Sheikh wa Bakwata wilayani

humo, Hassan Nuhu, alisema mat- ibabu hayo yalipelekwa wakati muafaka na kuitaka TIF irejee wakati mwingine na misaada zaidi. Naye Katibu wa Bakwata katika Wilaya hiyo, Madaraka Zubeir, ali- iomba TIF kuongeza muda katika matibabu yao kutokana na wingi wa watu waliojitokeza kupata hu- duma hiyo.

Kwa upande wake, mwenyeji

wa eneo lilipofanyika matibabu hayo, Mkurugenzi wa Sengerema Islamic Center, Alhaj Khamis Ta- basam, aliishukuru TIF kwa kuwa taasisi ya kwanza kutoa matibabu bure Sengerema.

Tabasam alisema kuwa toka kuanzishwa kwa wilaya hiyo haku- na taasisi iliyowahi kutoa matiba- bu bure kama TIF ilivyofanya laki- ni aliomba uongozi wa TIF, waki-

leta tena msaada kama huo, waongeze muda kwani wilaya hiyo ina wakazi wengi.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Ibisabageni, Jumanne Ally Masunga, licha ya kuishukuru TIF, alitaka mashirika mengine kuiga mfano huo katika kutoa matibabu bure. Nao baadhi ya wafaidika wa matibabu hayo waliishukuru TIF kwa matibabu hayo ya bure.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close