-1. Habari1. TIF News

TIF yaishukuru Al-Hikma kwa tuzo

Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) imeishukuru taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa tuzo ambayo taasisi hiyo imeipa TIF kutambua mchango wake, hususan katika kuunga mkono Mashindano ya 20 ya kuhifadhi Qur’an ya Afrika.

Shukran hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa TIF, Sheikh Haruna Rajab Jumanne, ambaye alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya TIF katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Katibu huyo alisema, tuzo hiyo ni ishara kuwa TIF ina mchango muhimu katika kuunga mkono shughuli za taasisi ya Al-Hikma Foundation yenye makao yake makuu Temeke jijini Dar es Salaam.

“Sisi TIF tunaishukuru Al-Hikma Foundation kwa tuzo hii. Hii ni ishara ya kuwa TIF ina mchango muhimu katika Taasisi hiyo ambayo imekuwa ikifanya mambo mengi ya dini, yakiwemo mashindano ya Qur’an Afrika,” alisema Sheikh Jumanne.

Sheikh Jumanne ambaye alitoa shukrani hizo kwa niaba ya Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahid, alisema TIF itaendeleza ushirikiano na taasisi ya Al-Hikma Foundation katika mambo mbalimbali, hususan Da’awah na elimu ya dini, hususan kuhifadhisha Qur’an Tukufu.

Al-Hikma Foundation kama ilivyo taasisi yetu ya TIF, hatutofautiani sana katika huduma tunazotoa. Sote tunaitangaza Uislamu na kuwahudumia Waislamu na jamii kwa ujumla. Hivyo ushirikiano wetu huu tutauendeleza ili tufike mbali zaidi,” alisema Sheikh Jumanne.

TIF ilikabidhiwa tuzo hiyo kutokana na vyombo vyake vya habari kurusha Mashindano ya Qur’an ya Afrika mubashara, tukio ambalo linatajwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya elfu 60 tangu lianze kuendeshwa uwanjani.

Ukiacha taasisi ya TIF, Al- Hikma Foundation pia iligawa tuzo kwa taasisi na kampuni nyingine zilizofanikisha Mashindano ya 20 ya Kuhifadhi Qur’an Barani Afrika yaliyofanyika Mei 19 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close