-1. Habari1. TIF News

TIF yagawa misahafu 20,000 toka UAE

Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) imesambaza jumla ya misahafu 20,520 katika misikiti mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Misahafu hiyo imetolewa na wafadhili wawili kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Muhammad Feisal Al Gassimi pamoja na mkewe Sheikha Raudhat bint Maktoum al Maktoum.

Akiongelea zoezi hilo lilivyoenda, mmoja wa maafisa wa TIF, Abubakar Nkungu amesema kipaumbele katika ugawaji wa misahafu hiyo ni misikiti yenye uhitaji mkubwa wa Kitabu hicho cha Allah.

Pia, zoezi hilo lilisimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIF, Sheikh Ibrahim Twaha ambaye alisema taasisi ya TIF ilipewa jukumu la kusambaza na imetekeleza jambo hilo, kwa ufanisi kama ambavyo imekuwa ikifanya katika miradi yote iliyowahi kuitekeleza.

“Siye The Islamic Foundation (TIF) tulipewa jukumu la kusambaza misahafu hii, Alhamdulillah, tumegawa misikitini, niseme tumetimiza jukumu letu kama tulivyoaminiwa,” alisema Sheikh Twaha.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close