-

TIF yafuturu na wabunge

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akipata futari iliyoandaliwa na Taasisi ya Islamic Foundation (TIF) kwa ajili wa Waheshimiwa Wabunge, Wafanyakazi wa Bunge na wageni wengine. Katikakati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Aref Nahdi na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mheshimiwa Abdallah Ulega.Hafla hiyo ilifanyika katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma hivi karibuni
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega (katikati) akizungumza mara baada ya kumaliza kufuturu. Kulia ni MwenyekitiwaTIF,ArefNahdi na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Vyombo vya Habari vya Taasisi hiyo, Sheikh Mohamed Issa

Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) yenye makao yake makuu mkoani Morogoro imeuaga Mwezi Mtukufu wa Ra- madhani kwa kuwafuturisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanza- nia. Katika kuheshimu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao umejaa kila aina ya ma- funzo ikiwamo kuheshimiana, kujenga umo- ja, tabia njema, ukarimu, upendo, lugha nje- manaibadakadhaawakadhaa, TIFiliwaleta wabungewavyama,maeneonadini mbalim- bali pamoja katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma baadayasikundefuyaswaumu. Baadhi ya waliohudhuria katika futari hiyo ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jam- huri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Joakim Mhagama, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigu- lu Nchemba na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwal- imu, Naibu Waziri wa Afya, Khamis Kigang- wala na Naibu Waziri wa Fedha, Ashatu Kijaji. Wakizungumza katika hafla hiyo, viongozi wa bunge na mawaziri mbalimbali waliiponge- za taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) kwa kuweza kuwaleta wabunge pamoja katika Mwezi wa Ramadhani na kusisitiza kuwa jam- bo hilo linadhihirisha wazi kuwa taasisi hiyo inazingatia maslahi mapana na taifa. Mmoja wa mawaziri hao, Mwigulu Nchemba alisema kuwa Serikali itashirikiana na TIF kuhakikisha jamii ya Watanzania inapata maendeleo katika nyanja mbalimbali. Naye Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangwala, aiitaka TIF kuendeleza harakati zake zenye faida kwa jamii na kuongeza kuwa kazi za utoaji matibabu bure zinazofanywa na taasisi hiyo zimeleta faida kubwa kwa Watanzania. Aidha, Kigwangwala alisisitiza kuwa TIF inastahili kupongezwa kwa sababu imekuwa inatoa huduma zake bila kubagua watu kwa kigezo chochote, iwe dini, kabila au jinsia. Kwa upande wake, Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea, alisema, TIF ni mfano wa kuigwa na kwamba wao kama watunga sharia wataishau- ri serikali ili iweze kuisaidia taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuipa ruzuku ili iweze kufanya shu- ghuli zake kwa uweledi na kuwafikia Watanza- nia wengi. Akizungumzia lengo la hafla hiyo, Mwenyekiti wa TIF alisema lengo la hafla hiyo ni kuwafahamisha wabunge shughuli za taasisi na kwamba TIF ipo tayari kushirikiana na wabunge katika kuwasaidia Watanzania wote. “Hatua hii ikifanikiwa itawasaidia wabunge kutatua kero za wananchi kupitia taasisi ya TIF ambayo imekuwa ikifanya shughuli mbalim- bali za kijamii ikiwemo ujenzi wa madarsa, uchimbaji visima na utoaji matibabu”, alisema Nahdi.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close