-

TIF yaahidi zaidi ya Millioni 5 kuisaidia shule ya Answar Islamic primary school

Taasisi ya The Islamic Foundation yenye makao yake Makuu Mjini Morogoro imeahidi kutoa zaidi ya shilling million tano kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Shule ya Answar Islamic primary school ya jijini dar as salaam

Ahadi hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi akiwa ni mgeni rasmi katika mahafali ya sita ya shule hiyo ya Answar Islamic Primary School iliyopo Kinondoni jijini Dar as salaam

Licha ya ahadi hiyo pia Mwenyekiti wa Taasisi the Islamic foundation ameahidi kumnunulia baskeli ya kutembelea kijana mlemavu anayesoma katika shule hiyo.

Kwa upande wake Amiri wa Jumuiya ya Answar Sunna Sheikh Juma Poli ameishukuru Taasisi the Islamic Foundation pamoja na Mwenyekiti kwa jitihada za kuuendeleza uislamu pamoja na kutekeleza ahadi ambazo hutolewa na taasisi hiyo

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close