-1. Habari1. TIF News

TIF na UAE watoa msaada wa chakula

TAASISI ya The Islamic Foundation kwa kushirikiana Umoja wa nchi za falme za kiarabu UAE wametoa msaada wa vyakula, tani 29 kwa watu Zaidi ya 500 wasiojiweza kuanzia wazee, wajane pamoja na watu wenye ulemavu huku zaidi ya shilingi milioni 70 zikitumika kufanikisha zoezi la msaada huo.

huo ni moja kati ya miradi mbalimbali wanayo itekeleza kwa wanachi wa Tanzania lengo likiwa ni kuweza kutoa ushirikiano wa karibu kwa serikali katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania.

Ni mwezi mtukufu wa Ramadhan ambapo kupitia mwezi huu waumini wa dini tukufu ya kiislamu mjini Morogoro wamepata neema ya kupatiwa msaada wa kikapu cha chakula chenye mjumuisho wa mchele kg 20, unga wa sembe kg 20, maharage kg 10, sukari kg 5, pamoja na mafuta ya kupikia lita 3 ambapo msaada huo umekabidhiwa na balozi wa falme za kiarabu UAE Mohamed Ibrahim Al bahri ambapo balozi huyo ameongozwa na mwenyeji wake mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi.

msaada huo ni juhudi za taasisi ya The Islamic Foundation za utekelezaji wa miradi mbalimbali kutoka kwa wahisani na kufikisha kwa wahitaji.

Aidha akizungumza na wanahabari katika zoezi hilo la ugawaji wa msaada huo kaimu balozi huyo amesema kuwa msaada huo ni moja kati ya miradi mbalimbali wanayo itekeleza kwa wanachi wa Tanzania lengo likiwa ni kuweza kutoa ushirikiano wa karibu kwa serikali katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi amesema kuwa msaada huo ni juhudi za taasisi ya The Islamic Foundation za utekelezaji wa miradi mbalimbali kutoka kwa wahisani na kufikisha kwa wahitaji.

Mbali na hayo mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation alipata nafasi kumtembeza balozi huyo kwenye kituo cha cha kulelea watoto yatima kilicho chini ya Taasisi hiyo sambamba na kuwapatia msaada wa mavazi.

Katika hatua nyingine msaada wa futari umetolewa katika baadhi ya misikiti mjini Morogoro ikiwemo masjid Bukhari ambapo zaidi ya kaya 50 wamepatiwa msaada huo pamoja na masjid Muizz ambapo waumini wa msikiti huo wamepatiwa msaada wa kikapu cha chakula sambamba na kufunguliwa kisima cha maji.

Huu ni muendelezo wa ugawaji wa misaada mbalimbali kwa wahitaji zoezi ambalo limekuwa likitekelezwa na taasisi ya The Islamic Foundation mara kwa mara kupitia wahisani wa ndani na nje ya nchi ambapo mara hii imefanikiwa kugawa kikapu hicho cha chakula kwa ajili ya matumizi ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close