-1. Habari1. TIF News

TIF na UAE watoa msaada wa chakula Dar es Salaam

TAASISI ya The Islamic Foundation kwa kushirikiana Umoja wa nchi za falme za kiarabu UAE wametoa msaada wa vyakula wa tani zaidi ya 40 kwa watu zaidi ya 700 wasiojiweza kuanzia wazee, wajane, watu wenye ulemavu pamoja na watu wenye uhitaji.

Msaada huo umetolewa jijini Dar es salaam ambapo msaada umeshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum ambapo msaada huo umejumuisha mahitaji mbalimbali ikiwemo mchele kg 20 unga wa sembe kg 20 maharage kg 10 sukari kg 5 pamoja na mafuta ya kupikia lita 3 ambapo msaada huo umekabidhiwa na naibu balozi wa umoja wa falme za kiarabu UAE Mohamed Ibrahim Al bahri.

lengo likiwa ni kuweza kutoa ushirikiano wa karibu kwa serikali katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania katika masuala ya huduma za kijamii ikiwemo kutekeleza miradi ya kutibu moyo watoto wadogo.

Akizungumza na wanahabari katika zoezi hilo la ugawaji wa msaada naibu balozi wa umoja wa falme za kiarabu UAE Mohamed Ibrahim Al bahri amesema kuwa msaada huo ni moja kati ya miradi wanayo itekeleza kwa nchi ya Tanzania lengo likiwa ni kuweza kutoa ushirikiano wa karibu kwa serikali katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania katika masuala ya huduma za kijamii ikiwemo kutekeleza miradi ya kutibu moyo watoto wadogo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi amesema kuwa msaada huo ni juhudi za taasisi ya The Islamic Foundation za utekelezaji wa miradi wanayopatiwa na wahisani na wao kuwafikishia wahitaji kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza katika zoezi hilo liloandaliwa na Taasisi ya The Islamic Foundation yenye Makao yake Makuu Mjini Morogoro amewata viongozi wa dini kuzidi kusimamia Amani ya nchi.

Aidha amepongeza ushirikiano huo wa Falme za Kiarabu pamoja nchi ya Tanzania ambao unasaidia kuimarisha mahusiano

Huo ni muendelezo wa ugawaji wa misaada mbalimbali kwa wahitaji zoezi ambalo limekuwa likitekelezwa na taasisi ya The Islamic Foundation mara kwa mara kupitia wahisani wa ndani na nje ya nchi ambapo mara hii imefanikiwa kugawa kikapu hicho cha chakula kwa ajili ya matumizi ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani.

Kwa undani zaidi wa tukio hili endelea kufutilia vyombo vyetu vya Habari vya Imaan

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close