-1. Habari1. TIF News

TIF na Dubai Charity Association

Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) imeingia katika makubaliano ya ushirikiano na taasisi Dubai Charity Association (DCA) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Mkataba wa ushirikiano huu ulisainiwa jijini Dubai katika ofisi za DCA, wakati Aref Nahdi, Mwenyekiti wa TIF yenye makao yake makuu mjini Morogoro, alipotembelea katika taifa hilo la Falme za Kiarabu kikazi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Nahdi, ushirikiano wa taasisi hizi mbili kubwa na zenye mafanikio makubwa, utagusa Vile vile unaweza kuangalia TV Imaan kwa njia ya mtandao (online) kupitia www.ustream.tv/channel/radio-imaan-fm-2 maeneo muhimu ya huduma za kijamii, zikiwemo maji na elimu.

Wakati Mwenyekiti Nahdi alitia sahihi makubalino hayo kwa niaba ya The Islamic Foundation (TIF) ya Tanzania; kwa upande wa taasisi ya Dubai Charity Association (DCA) aliyetia sahihi ni Mkurugezni wake mkuu, Ahmed Musmaar. “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufanikisha hili. Utilianaji sahihi wa makubaliano haya ni hatua muhimu katika mafanikio ya jamii ya kitanzania,” Mwenyekiti Nahdi alisema baada ya utilianaji saini.

Taasisi zote mbili, TIF na DCA zina rekodi ya kupigiwa mfano katika kazi ya kuhudumia jamii. DCA ni taasisi iliyodhamini na bado inaendelea kudhamini miradi mingi ya ujenzi wa huduma mbalimbali za kijamii, ikiwemo shule na visima, katika nchi mbalimbali za Afrika na Asia.
Nayo TIF imejizolea umaarufu mkubwa kwa misaada ya kwa jamii mbalimbali kwenye uchimbaji wa visima, misaada kwa wahanga ya waathirika wa majanga na huduma za kiafya na kielimu.

Mwenyekiti Nahdi pia alipata fursa ya kubadilishana mawazo na viongozi mbalimbali sio tu wa DCA bali pia wa nchi hiyo kuhusu mambo ya maslahi kwa pande zote mbili.
  
Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close