-

Tathmini Ifanyike kwa wanaojihusisha na malezi ya watoto

WADAU wanaojihusisha na malezi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na yatima na watu wanao ishi na VVU wametakiwa kufanya tathmini mara kwa mara juu ya huduma hiyo wanayo itoa lengo likiwa ni kuifahamisha jamii juu ya changamoto wanazo kumbana nazo katika utoaji huduma hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Ignas Sanga wakati akizungumza na wadau hao juu ya kujadili namna bora ya kutoa huduma bora kwa watoto waishio katika mazingira magumu yatima pamoja na watu wanao ishi na maambukizi ya vvu.

Aidha kaimu mkurungezi huyo ameongeza kuwa kuna kila sababu ya kukaa wadau mbalimbali watoto na watu waishio na vvu lengo ni kuweza kujadili namna bora ya kutoa huduma hiyo kwa jamii.

Kwa upande wake mwakilishi kutokea kituo cha kulelea watoto ya tima kilicho chini ya Taasisi ya The Islamic Foundation Ustadhi Nuru Muhamad amesema kuwa kituo cha Imaan Orphanage Center kilionzisha kwa lengo la kusaidiana na serikali namna ya kupunguza watoto wa mitaani na waishio katika mazingira magumu.

Wakiwasilisha ripoti zao mbele ya kaimu mkurugenzi  wadau mbalimbali wa masuala ya watoto waishio katika mazingira hatarishi pamoja na wale wa utoaji elimu juu ya watu wanaoishi na vvu wamezitaja baadhi ya changamoto ambazo ni kikwazo katika kazi zao.

Mkutano huo uliyo andaliwa na shirika lisilo la kiserikali la  (SJI) na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya watoto waishio katika mazingira magumu yatima pamoja na vituo vya kutoa elimu juu ya watu waishio na maambukizi ya vvu ulikuwa na lengo la kuwa kumbusha wadau hao juu ya kufanya Tathimini wa kazi wanao ifanya.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close