-

TAARIFA YA MUANDAMO WA MWEZI WA RAMADHANI ( 1440 H )

BARAZA KUU LA JUMUIYA ZA ANSWARU SUNNAH TANZANIA (BASUTA )

الحمد لله و الصلاة و السلام علي رسول الله و علي آله و صحبه و بعد .

Ndugu zangu Waislam popote mlipo Ndani na Nje ya Nchi , napenda kuwajulisha Rasmi kwa Niaba ya Kamati ya Mwezi muandamo ya Baraza la Jumuiya za Answaru Sunnah Tanzani kwamba leo ni Mwezi 29 Shabani 1440 H Siku ya Jumamosi , tumekalifishwa Waislam wote kuuangalia na kutafuta Habari za Muandamo wa Mwezi kwa mujibu wa maamrisho aliyotupa Mtume wetu Muhammad Swallallahu alayhi wa Sallam, aliposema :

” صوموا لرؤيته و أفطروا لرؤيته فإن غم عليكم غٱكملوا عدة شعبان ثلاثين “.

“Fungeni kwa kuonekana Mwezi na Fungueni kwa kuonekanwa na pindipo utakapofichakamana kwenu basi kamilisheni Hesabu ya Mwezi Shaaban siku Thalathini” (Bukhari) .

Kamati hiyo baada ya kufuatilia Habari za Mwandamo wa Mwezi kwa kina Ulimwengu mzima, mpaka tukitoa Tangazo hili hakuna Mtu yoyote hapa Nchini aliyetoa Habari za kuandama kwa Mwezi wala hakuna Nchi yoyote Ulimwenguni iliyotangaza kuonekana kwa Mwezi hivyo basi Kamati inawatangazia Waislam wote kwamba kesho tunakamilisha Thalathini ya Mwezi wa Shaabani na Tarehe 1 ya Mwezi wa Ramadhani itaingia mara baada ya Magharibi ya Usiku wa kuamkia Siku ya Jumapili na Swaumu itaanza Siku ya Jumatatu Tarehe 6 May 2019.

Baraza linawapa Waislamu popote walipo Pongezi za kufikiwa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwatakia Swaumu na Matendo yote Mema yenye kukubaliwa .

Wa Billahi-ttawfiiq .

Ni mimi Ndugu yenu,

Salim Abdulrahim Barahiyan,

Mwenyekiti wa Kamati ya Mwandamo BASUTA .

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close