-

Sherehe za Idd zafana Dar, mikoani

Kufuatia kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Waislamu nchini wametakiwa kudumisha ukarimu, mapenzi, huruma san- jari na kuendelea na utekelezaji wa ibada walizokuwa wakizifanya ndani ya mwezi huo kwa kuzifanya ndani ya miezi mingine isiyokuwa Ramadhani.

Hayo yamebainishwa na masheikh mbalimbali walipokuwa wakiwahutubia mamia ya wau- mini wa dini ya Kiislamu kupitia khutba ya ibada ya Swala ya Idil- Fitri iliyoswaliwa jana katika mikoa mbalimbali nchini.

Aidha, katika khutba zao, masheikh mbalimbali pia walike- mea utovu wa maadili wa baadhi ya watumishi wa serikali na katika sekta binafsi ambao hujihusisha na vitendo vya ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi.

Masheikh vilevile waliwahimi- za Waislamu kuendelea kuhuru- miana na kusaidiana katika miti- hani mbalimbali inayowasibu ka- tika kutekeleza dini yao.

Morogoro

Morogoro, Waislamu wame- himizwa kuendelea kufanya ma- tendo mema kama ilivyokuwa wakati wa mwezi mtukufu wa Ra- madhani kwani hiyo ndiyo njia bora na pekee ya kunufuika na ibada ya funga ya Ramadhani.

Wito huo umetolewa na Sheikh Yahya Khamis kupitia khutba ya Swala ya Idil Fitr iliyoswaliwa ka- tika viwanja vya taasisi ya The Is- lamic Foundation (TIF).

Katika khutba yake, Sheikh Yahya alisema njia bora ya Waisla- mu kunufaika na funga ya Ram- adhani ni kutoyarejea madhambi waliyokuwa wakifanya kabla ya mwezi huu, na kwa ajili hiyo ali- wataka Waislamu watafute radhi za Mola wao kwa kudumu katika kufanya ibada mbalimbali ikiwemo sita katika mwezi huu wa Shawwal.

Aidha, Sheikh Yahya alitumia fursa hiyo kuwakumbusha Wais- lamu juu ya umuhimu wa kuende- lea kusaidiana na kuhurumiana: “Umuhimu wa kusaidiana katika kheri pamoja na kulishana ndiyo namna bora ya kunufaika na Swaumu ya Ramadhani,” alisema Sheikh Yahya.

Dar es Salaam

Yusuph Amin anaarifu kutoka Dar es Salaam, kwamba Amiri wa Jumuiya ya Ansaar Sunnah Tan- zania (JASUTA), Sheikh Juma Poli ameitaka jamii ya Kiislamu kuunga mkono juhudi zinazofan- ywa na Rais wa Jamhuri ya Mu- ungano wa Tanzania katika kupambana na watumishi wazembe pamoja na kuwashu- ghulikia wale wote wanaohusika na biashara haramu ya uuzaji wa dawa za kulevya.

Sheikh Poli aliyasema hayo wakati wa khutba ya ibada ya swa- la ya Idil-fitri iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na ma- mia ya Waislamu kutoka viunga mbalimbali vya jiji hilo. Sheikh Poli alionekana kuchukizwa na vi- tendo hivyo viovu ambapo aliwa- taka viongozi wengine wa serikali na dini kuvalia njuga vitendo hivyo

vinavyokwenda kinyume na maadili ya dini na taifa ukiwemo ujambazi.

Kuhusiana na nini Waislamu wafanye baada ya kumalizika Ra- madhani, Kiongozi huyo alitoa wito kwa Waislamu kuchukua athari za mwezi huo na kudumu nazo katika miezi mingine kama walivyokuwa wakifanya waja wema waliopita ambao licha ya kufanya mambo mengi ya kheri ndani ya Ramadhani bado waliko- sa uhakika wa matendo yao kuku- baliwa na Allah.

“Ramadhani ni shahidi kwa mema tuliyoyatenda na kwa ajili hiyo kila mtu anatakiwa ajikague na kujiuliza ni kwa namna gani Ramadhani imemuathiri,” ali- bainisha Sheikh Poli.

Pia Sheikh Poli alitumia fursa hiyo kuwakumbusha masheikh, maimamu, walinganiaji na Wais- lamu wengine kutumia hekima, maneno mazuri na laini katika ku- walingania watu dini ya Allah kwani kufanya hivyo ndiyo msingi bora wa kupata mafanikio katika kazi ya ulinganiaji.

Naye, Sarah Zuberi anaripoti kuwa, Ustadh Rashid Rajabu ameitaka jamii ya Waislamu nchi- ni kuendelea kufanya toba hata baada ya mfungo wa Ramadhani

kwani Allah ameamrisha kufanya hivyo muda wowote ule.

Ustadh Rajabu alibainisha hayo wakati wa ibada ya swala ya Idd el Fitri iliyoswaliwa huko Boko jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka Waislamu kuendelea kufanya toba hata baada ya ku- malizika kwa Mwezi wa Ramad- hani. “Kumekuwa na tabia ya Waislamu wengi kuacha kufanya toba baada ya Ramadhani kumal- izika”, aliongeza kusema Ustadh Rajabu.

Singida

Na kutoka Singida Hassan Nin- ga anaarifu kuwa katika swala ya Idd iliyofanyika katika viwanja vya viwanja wa Shule ya Alfur’qan Manispaa ya Singida Waislamu wametakiwa kuendeleza matendo mema waliyokuwa wakiyafanya katika Mwezi Mtukufu wa Ram- adhan sambamba na kujiepusha na maovu. Nasaha hizo zilitolewa na Sheikh Abdul-Aziz Swaleh am- bapo aliwataka Waislamu kuwa mfano wa kuiga katika kudumisha amani na utulivu nchini na kuongeza kuwa, Ramadhani ili- kuwa fursa muhimu kwa waumini hivyo jamii ya Kiislamu haina budi kudumu na matendo mema katika muda wote wa maisha yao.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close