-

Sheikh Kishk akemea faraka

Wakati Waislamu ulimwenguni kote wakiendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Imam na Khatib wa msikiti wa Vetenari uliopo Temeke jijini Dar es Salaam, Sheikh Nurdin Kishk amewataka Waislamu kuondoa ikhtilafu zao katika suala la mwanadamo wa mwezi na badala yake waungane katika kuwaletea Waislamu maendeleo.

Sheikh Kishk aliwaambia Waislamu katika msikiti wa Vetenari kuwa, suala la ikhtilafu ya mwandamo wa mwezi ipo kwa muda mrefu na wala hakukuwa na mifarakano yoyote miongoni mwa wanazuoni walio
pita. Alisema pamoja na kutofautiana kwao mitazamo, waja wema waliopita hawajawahi kutuhumiana, kutusiana au kunyoosheana vidole bali walijadiliana na kukubaliana kila mmoja afunge kulingana na madhehebu yake.

Kwa mujibu wa Sheikh Kishk, Waislamu waliotangulia kufunga swaumu ya Ramadhan mwaka huu hawajakosea kwani wamefuata rai za Maimamu. Kadhalika, waliofunga siku iliyofuata nao hawajakosea kwani wamefuata kauli za Maimamu.

Sheikh Kishk alisema mtu yeyote atakayezitia doa kauli za Maimamu wanne wa Ahlus Sunnat Waljama’ah kuhusu mwanadamo wa mwezi, huyo atakuwa amefanya kosa kubwa.

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close