-

Nama Foundation Yatembelea Tif

TAASISI ya Kiislamu ya NAMA Foundation yenye Makao yake Makuu Mjini Kuala Lumpa nchini Malaysia pamoja na Taasisi ya An-Nahl Trust ya Dar es salaam, zimefanya ziara katika  Taasisi ya The Islamic Foundation ya Mjini Morogoro, na kujionea kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo.

Katika ziara hiyo, Taasisi ya NAMA Foundation imeongozwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dakta Saleh Bazaed, na kwa upande wa Taasisi ya An-Nahl Tust iliongozwa na Mwenyekiti wake Engineer Ally Kilima, pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Musa Nyasingwa.

Msafara wa ziara ya Taasisi hizo mbili, umepokelewa na Viongozi wa Taasisi ya The Islamic Foundation, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIF, Sheikh Ibrahim Twaha, Kiongozi wa Kitengo cha Daawa Sheikh Ismail Kundya, Afisa Mipanga Musa Buluki, Mlezi wa Taasisi Mzee Salum Mdula, pamoja na Watendaji wa Imaan Media.

Baaada ya kutembelea Studio za Matangazo ya Radio pamoja na TVImaan, Afisa Mipango wa Taasisi ya The Islamic Foundation Mussa Buluki amewaeleza Viongozi wa Taasisi hizo za NAMA Foundation na An-Nahl Trust, kazi mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NAMA Foundation Dokta Saleh Bazaed amesema kuwa Taasisi hiyo na NAMA inafanya kazi kwa kushirikiana na nchi mbalimbali Dunia, na pia imeiopongeza Taasisi ya The Islamic Foundation kwa kumiliki Vituo vya Habari vya Radio, Tv na Gazeti Imaan, ambavyo vimekuwa na msaada mkubwa katika jamii.

Hali kadhalika, Mjumbe wa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu iliyochini ya Taasisi ya The Islamic Foundation  Jumanne Mpinga amewaeleza Viongozi wa Taasisi hizo sababu ya Taasisi ya TIF kuanzisha Bodi hiyo, ikiwemo kuwasaidia Wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kujiendeleza na masomo yao.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close