-

Naibu Waziri Ashatu ahimiza elimu ya Qur’an

Naibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Ashatu Kijaji amesisitiza suala la elimu ya Qur’an kwa vijana ili kujenga jamii yenye uadilifu.

Dkt Ashatu aliongea hayo wakati wa mashindano ya kwanza ya kuhifadhi Qur’an yaliyofanyika katika mji mdogo wa Pahi, Kondoa mkoani Dodoma na kuwakutanisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali. Pia, Dkt Ashatu ambaye ndiye aliyeandaa mashindano hayo, alisema kuwa, “kitabu cha Qur’an ni muongozo sahihi kwa maisha ya mwanadamu hapa duniani na akhera”.

 Naye Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amewataka wananchi wa Kondoa kuithamini elimu ili iweze kuwaletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Taasisi ya The Islamic Foundation(TIF), Sheikh Haruna Rajab Jumanne ambae alimuwakilisha Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Aref Nahdi, alisema kuwa TIF iko bega kwa bega na Dkt. Ashatu Kijaji katika harakati zake mbalimbali za kuwatumikia wananchi. Pia, amempongeza kwa kuwafuturisha Waislamu akimuomba aendelee na moyo huo huo wakusaidia watu.  Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu aliyemuwakilisha Mufti, Sheikh Abubakar Zubeir, aliwahimiza wazazi wa Kondoa na Waislamu kwa ujumla kuwapeleka watoto madrasa ili wapate elimu itakayowasaidia hapa duniani na Akhera.

Mshindi wa kwanza wa juzuu 30 katika mashindano hayo alikuwa Mize Abdallah kutoka Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) na alitunukiwa Shilingi Milioni moja za Kitanzania.

 

Show More

Related Articles

Back to top button
Close