-1. Habari1. TIF News

Mwenyekiti TIF azuru Malaysia

Mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) yenye Makao yake makuu mjini Morogoro, Aref Nahdi, amefanya ziara ya kikazi kutembelea taasisi ya NAMA yenye makao yake makuu jijini Kuala Lumpur Malaysia. Akiwa katika makao makuu ya NAMA, Aref alipokewa na mwenyeji wake ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dkt. Saleh Mbarak Bazed.

Dkt. Bazed aliwahi kuitembelea TIF mwaka 2017 na 2018. Katika ziara hiyo iliyolenga kukuza uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya TIF na NAMA, Mwenyekiti Nahdi amepangiwa kutembezwa kuona shughuli mbalimbali za NAMA na pia kufanya mazungumzo na viongozi wake. NAMA na TIF wana makubaliano ya ushirikiano katika nyanja za elimu na huduma nyingine za kijamii. Pamoja na ushirikiano na TIF, NAMA pia wana ushirikiano na taasisi ya An-Nahl Trust na Pamoja Foundation za hapa nchini.


Taasisi ya NAMA ilianzishwa kwa lengo la kutoa misaada katika sekta ya elimu na kuzijengea uwezo taasisi za Kiislamu duniani kote

Hivi karibuni, NAMA kwa ushirikiano na An-Nahl Trust, imeanzisha mpango wa kutoa mikopo ya elimu isiyo na riba kwa wanafunzi wa Kitanzania waliopata nafasi za masomo kwa ngazi ya shahada, shahada ya uzamili na shahada ya uzamivu lakini wakakosa uwezo. Taasisi ya NAMA ilianzishwa kwa lengo la kutoa misaada katika sekta ya elimu na kuzijengea uwezo taasisi za Kiislamu duniani kote. Wanafanya hivyo kwa kutoa misaada na mikopo kupitia taasisi washirika.

Hadi sasa, watu wapatao 12,000 wameshafaidika na ufadhili na misaada kupitia miradi mbalimbali ya NAMA ipatayo 213 duniani kote katika program tofauti 76. Taasisi hiyo pia ina watu wa kujitolea 1,500 wanaofanya kazi mbalimbali za NAMA.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close