-

Mwenyekiti TIF aahdi Polisi Kisima cha Milioni 20

TAASISI ya The Islamic Foundation imeahidi  kuchimba kisima chenye thamani ya shilingi milioni 20 katika makazi ya Jeshi la Polisi Mjini Morogoro kutokana na jitihada zao za kuimarisha ulinzi na usalama katika Mkoa huo

Ahadi hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Saimon Sirro katika kikao maalum cha harambee ya kuchangia jeshi hilo Mjini Morogro. Mwenyekiti Aref amemueleza Mkuu wa jeshi Hilo kuwa vyombo vya habari vya Imaan media vimekuwa mdau muhimu kwa kushirikiana na jeshi la polisi nchini Mkoani Morogoro katika kuelimisha jamii kulinda amani

Aidha amesema kuwa kutokana na  ushirikiano huo na Jeshi la Polisi Taasisi ya The Islamic Foundation itachimba kisima chenye thamani ya shilingi milioni 20,Kwa upnde wake Mkurugenzi wa Vyombo vya habari vya Imaan Ahmed Bawazir ameahidi kutoa shilingi laki tano kwaajili ya kuchangia jeshi hilo. Hata hivyo katika harambee hiyo wafanyabiashara mbalimbali waliweza kutoa ahadi kwaajili ya kuboresha makazi ya polisi mjini Morogoro

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa wa Morogoro ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dokta Kebwe Steven Kebwe amewataka wadau mbalimbali kushirikiana na jeshi hilo ili kuboresha makazi yao

Nae Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Ulrich Matei amesema kuwa makazi ya Polisi Mjini Morogoro yakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na kujenga muda mrefu hali iliyosababisha baadhi ya nyumba kuvuja kipindi cha Mvua

Akizungumza na Vyombo vya habari mara baada ya harambee hiyo Mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP Saimon Sirro amesema kuwa endapo wadau mbalimbali watashirikiana na jeshi hilo wataweza kuondoa changamoto za maaskari . Hata hivyo IGP Sirro amesema kuwa jeshi hilo halitosita Kumchukulia hatua yeyote Yule atakae bainika kuvunja sheria za nchi

Katika harambee hiyo zaidi ya shilingi milioni mia moja zinataraji kupatikana ili kuboresha makazi ya jeshi la Polisi Mjini Morogoro

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close