-

MUKHTASARI WA DIRA YA HABARI 21.10.2015 RADIO IMAAN F.M

VIONGOZI wa Dini ya Kiislam Wilayani Sikonge Mkoani Tabora wamewataka Wananchi wa Mkoa huo na Watanzania kwa ujumla, kuendelea kudumisha amani hapa nchini.
Viongozi hao wa dini wametoa kauli hiyo katika Mkutano uliowakutanisha Wananchi na Viongozi mbalimbali Wilayani humo na kumuomba Allah S.W. kuweza kuidumisha amani na utulivu nchini.
****************************

BARAZA Kuu la Waislam Wilayani Arumeru Mkoani Arusha limeanzisha Makakati wa uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha elimu ya maarifa ya Uislam kwa Shule za Msingi na Sekondari.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Wilayani Arumeru Ustaadh Harua Hussen ametoa taarifa hiyo katika hafla ya uchangiaji wa fedha hizo kwa ajili ya kufungua furusa ya kuendeleza na kukuza elimu kwa vijana wa Kiislam
Aidha Ustaadh Haruna amesema kuwa wanampango wa kujenga vituo vitano vya kisasa kwa ajili ya kusimamia elimu ya dini ya Kiislam na elimu ya maarifa ya Uisla
****************************

SERIKALI ya Mkoa wa Kilimanjaro imewataka Wakazi wa Kijiji cha Bendera Wilayani Same Mkoani humo kuacha Mgogoro wa Mpaka kati yao na Wakazi wa Kijiji cha Mkomanzi cha Wilayani Koronge Mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Amasi Makalla ametoa kauli wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji hicho na kuwataka Wananchi hao kuacha masuala ya siasa kutokana na Mgogoro huo.
****************************

KIMATAIFA

****************************
KIONGOZI wa Chama cha Siasa kali za Mrengo wa kulia nchini Ufaransa – National Front – Marine Le Pen, ameshtakiwa kwa makosa ya kuchochea chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Le Pen ameshtakiwa kutokana na hotuba aliyoitoa mwaka 2010 katika mji wa Lyon, alipolinganisha uhamiaji wa Waislamu na ukaliaji Ufaransa kimabavu na Wanazi wakati wa vita kuu vya pili vya dunia.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Le pen aliondolewa kinga yake ya ubunge wa Ulaya mwaka 2013 ili akabiliwe na kifungo cha hadi mwaka moja gerezani, pamoja na faini ya euro 45,000.
****************************

ZAIDI ya Watu Ishirini na mbili wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa, kaskazini mwa Ufilipino baada ya kuibuka Kimbunga Kopp, ambapo kimeanda kutua katika Bahari ya China Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kimbunga hicho kimesababisha mafuriko katika vijiji vipatavyo 200 katika eneo hilo, na kuvifunika baadhi ya Vijiji chini ya maji ya kina cha karibu mita 1.5.
****************************

MKUU wa Sera ya Kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini, ametoa wito wa kuheshimiwa Wakimbizi wanaohatarisha maisha yao wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterrania kuingia barani Ulaya.
Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, limesema Watu Elfu tano hukimbia kila mwezi kutoka Mataifa Maskini, kutokana na utumikishwaji wa lazima jeshini na ukiukaji wa haki za binaadamu.

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close